Dar es Salaam. Ligi Kuu Bara
imefikia patamu huku Azam FC na Yanga zikipigana kufa au kupona kuwania
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, ambapo mechi zao za leo ndiyo zitakozotoa
picha ya ubingwa msimu huu.
Azam itaingia dimbani leo kukipiga na Mbeya City
kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya huku Yanga ikicheza dhidi ya JKT Oljoro
leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. Azam yenye pointi 56
itaingia uwanjani leo kutafuta pointi tatu muhimu na kutangazwa mabingwa
kwani ushindi wowote utawasaidia kufikisha pointi 59 ambazo
hazitafikiwa na timu yoyote katika Ligi Kuu Bara kwani Yanga yenye
pointi 52 ikishinda michezo miwili iliyobakiza ukiwamo wa leo itafikisha
pointi 58.
Mbali na mechi hizo pia Simba itacheza leo na
Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa, wakati Mtibwa itacheza na Ruvu
Shooting Uwanja wa Manungu na Mgambo itawakaribisha Kagera kwenye Uwanja
wa Mkwakwani, Tanga.
Katika mechi zilizochezwa jana, JKT Ruvu iliichapa
Coastal Union 1-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani wakati Rhino Rangers
ilichapwa na Tanzania Prisons 4-3 kwenye Uwanja wa Sokoine na hivyo
kushuka rasmi daraja. Imeandaliwa na Vicky Kimaro, Godfrey Kahango na
Bulhan Yakub
source: mwananchi
source: mwananchi
No comments:
Post a Comment