Mjumbe wa Bunge la Katiba,Hamad Rashid Mohammed
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, imevunja sheria kwa
kupendekeza muundo wa Muungano wa serikali tatu kwani haikupata theluthi
mbili za Wazanzibari na Watanzania Bara.
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Hamad Rashid Mohammed, aliyasema hayo jana na kuikosoa Tume kuwa Wazanzibari walitaka serikali ya mkataba siyo serikali tatu kama ilivyoeleza.
“Tume ilipata wapi mamlaka ya kusema Zanzibar inataka serikali tatu, walikaa nao wapi wakazungumza?," Alihoji.
“Ukichukua katiba na sheria ya mabadiliko ya Katiba iliyopitishwa na Bunge inasema ili kufanya badiliko la katiba ni lazima ipatikane theluthi mbili ya kura kwa Zanzibar na Tanzania Bara.”
Mohammed ambaye alivuliwa wadhifa na kufukuzwa uanachama wa CUF, alisisitiza kuwa kama Tume ya Warioba, haikupata theluthi mbili hizo imevunja sheria.
Alisema Tume ilitakiwa baada ya kupata theluthi mbili ya Bara irudi Zanzibar na kuwashauri kuangalia matatizo ya kurekebisha kwenye mfumo ulioko badala ya kupendekeza serikali tatu.
“Kwa kuwa Tume yenyewe ndiyo iliyoanza kuvunja sheria hiyo kwa sasa haina uhalali wowote hivyo wajumbe kutoka Tanzania Bara waliopo wakae wapate theluthi mbili na sisi kutoka Zanzibar tukae na kutengeneza theluthi mbili ili tupate Katiba mpya,” alishauri.
Akizungumzia serikali mbili, alisema ndizo mwafaka kwani tatu zitaongeza gharama zaidi.
Alisema Tume ya Warioba haikukokotoa namna ya kuwatunza viongozi wakuu wakiwa madarakani na wanapostaafu.
“Leo Rais akisafiri anatumia si chini ya Shilingi milioni 500, wakati mwingine hata bilioni moja,” alisema na kuongeza kuwa hizo ni gharama wakiwa madarakani na wakistaafu itakuwaje?
Alisema viongozi hao wakistaafu zaidi ya watatu kwa wakati mmoja utakuwa mzigo mkubwa wanabebeshwa wananchi.
“Tume haikuangalia gharama za miaka mingi ijayo,itakuwa gharama kubwa na kuhoji ni nani atazibeba?”

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment