Wakati
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ipo katika mchakato wa kupata katiba mpya
baada ya tume ya Jaji warioba kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba mpya na
mheshimiwa Rais wa Jamuhuri kuwatangaza rasmi wajumbe zaidi ya 600 ambao ni wawakilishi wa wananchi
wa Tanzania katika upatikanaji wa Katiba hiyo Mpya.
Safari
hii ya maandalizi ya kuandaa katiba mpya kwa kweli imekuwa haionyeshi mwelekeo
mzuri ambao unaleta matumaini kwa taifa letu. Tunafahamu fika kuwa Mheshimiwa
Rais kupitia washauri wake ametuteua watu wazuri na ni tegemeo letu kuwa
wawakilishi hao ni watu wenye hekima na uwezo mzuri wa kutuandalia Katiba Bora
kwa vizazi vijavyo.
Kutangazwa
kwa bunge hili la katiba kwa upande mmoja iliamsha matumaini ya wananchi kuwa
kazi hii itakuwa nyepesi na yenye tija nzuri kwa maendeleo ya Taifa na wananchi
wake ndani ya miezi mitatu ambayo Bunge
hili limepewa ili kukamilisha kazi yake kuanzia February 2014.
Lakini
cha kushangaza mpaka niandikapo waraka huu, inasikitisha kuwa kuwa mwendo wa bunge hili ni wa kusuasua. Kwa maneno mengine hakuna mwelekeo mzuri
ambao bunge hili maalumu limeonyesha baada yake bunge limepewa majina ambayo
hayaendani na wadhifa wake.
Bunge
lililojaa mizengwe , malumbano, kashfa, mivutano na kadhalika.
Kama
wananchi tuna mengi ya kujiuliza hawa waheshimiwa wabunge wanafanya haya yote
kwa faida ya nani?
Je
waheshimiwa wajumbe wanaelewa nini wanatakiwa wafanye kwa faida ya Taifa hili?
Je
kupitisha kanuni za kuendesha bunge maalum ni lazima watukanane?
Ni
ukweli ambao haufichiki kuwa hata
Aristotle katika maelekezo yake kuhusu Demokrasia alikuwa anahimiza katika Majadiliano
ya hoja; na sio kuzomeana na kutukanana; lakini ukifilisika kifikra matokeo
yake ni kuzomea au kutukanana.
Na kutika kufikia hitimisho lazima kuwe na
mshindi ambaye atapatikana kwa uwingi wa kura kama kura itatumika kama kigezo,
hii ndio demokrasia; Lakini wachache wanaweza kuwa na hoja nzito ambazo
zinaweza kulegeza msimamo wa wengi. Lakini sio kufikia hitimisho kwa malumbano
na matusi.
Wajumbe
wanatakiwa wafahamu kuwa misimamo
binafsi na ya kichama hapa sio mahali pake; kama mwandishi mmoja alivyoandika
kuwa “Inasikitisha kuona baadhi ya wajumbe wakitoa kauli zisizo na staha,
wakishindana kwa hoja zisizo na mashiko na hata kusisitiza misimamo yao binafsi
kwa ajili tu ya kukomoana, kutokana na tofauti za kiitikadi”.
Kwa
kufanya hivi tuelewe fika kuwa waheshimiwa wajaumbe wa Bunge maalum watakuwa
hawajefanikiwa kukonga roho za watanzania ambao kiu ya kupata katiba mpya na Bora;
Ni
kweli kuwa wajumbe hawa walichaguliwa kutokana na ubora wao? Au wamechaguliwa
kutokana na misimamo yao na vitisho ambavyo wamekuwa wakivionyesha kwa serikali
ili kuwazima mdomo? Ndio maana tunashuhudia longo longo zaidi kuliko busara ya
kiutendaji? Tulitegemea kuwa wangeanza safari hii ya miezi Mitatu kwa busara na
hekima, kwa kuheshimiana na kwa kuzingatia zaidi hoja na kujadiliana kwa staaha
na undugu na sio longo longo..
Kinachoendelea Dodoma ni kutegemea sana busara
za wajumbe wachahce ambao wanaweza kulivusha bunge hili salama kama sio hivyo liataendelea na longo longo na kupoteza
mwelekeo.
Mwandishi mmoja aliwahi kuandika kuwa “Sisi kama
watanzania tunatamani kujua viongozi wetu wanasimaia wapi na tujue mitazamo yao
kisiasa.” Kinachopiganiwa na watanzania ni hiki
hoja ya wengi lazima iwe hoja yenye maslahi ya taifa na sio kunufaisha
itikadi Fulani au kundi Fulani tu.
Itakuwa vizuri kuwa wajumbe watakao simama
upande wa wengi wahakikishe kuwa wanantetea haki za wote na tuweke misingi
itakayohakikisha kuwa maslahi binafsi au ya kichama hayatawali. Kwaq msingi huu
nguvu ya walio wengi isiwe ya ubabe na dhuluma, bali iwe ni nguvu ya kweli na
yenye kujitambua inayotaka kujenga utaifa na kujali raia wote na haki zao.
Longo longo
hizi zitokanazo na wajumbe ambao sisi tunawaona kuwa wana busara
zinazoendelea kutolewa ndani na nje ya Bunge haziashirii mwisho mzuri.
Kauli ya mheshimiwa Freeman Mbowe, ambayo
aliitoa wakati longo longo na mabishano inaendelea imeonyesha busara “amesema
kwamba bado wataendelea kushiriki kwenye vikao, ingawa wataendelea kupigania
mageuzi ya msingi kwenye uendeshaji wa Bunge hilo ambalo linatakiwa kutoka na
Katiba Mpya itakayopigiwa kura ya maoni ndani ya kipindi kisichozidi miezi
miwili kutoka sasa”.
Tatizo la wanansiasa na vyama vyao kama mwandishi mmoja alivyoandika “Vyama vya
kisiasa vimekuwa vinafikia muafaka katika mambo mbalimbali na kutoa taswira
kwamba kuna muelekeo mzuri, lakini baadae wanasiasa haohao wanabadilika na
kuyabadili maridhiano hayo na kuanzisha mijadala mipya inayoturudisha nyuma.”
Waheshimiwa wajumbe tunawaomba sana achane hizi longo longo za kiitikadi ambazo hazina faida
kwa Taifa na Amani yetu ambayo imedumu kwa miaka 50 sasa.
No comments:
Post a Comment