TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
01/11/2012
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein amemteua Vuai Mwinyi Mohammed kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdul hamid Yahya Mzee imesema kuwa Rais Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 61(2) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984
Aidha Dkt. Shein amewateua Ameir Ali Khatib kuwa Mkurugenzi wa Huduma za Rais(Mnukulu) Ikulu katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar.
Pia Rais amemteua Makame Ali Makame kuwa Mkurugenzi wa Mipango,Sera na Utafiti katika Wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano, Zanzibar.
Halikadhalika Dkt Shein amemteua Mariyam Juma Abdalla Saadalla kuwa Mkurugenzi wa Mipango,Sera na Utafiti katika Wizara ya Kilimo na Maliasili,Zanzibar .
Vile vile Dkt Shein amemteua Mwalim Hamad Mbarouk kuwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani katika Wizara ya Ardhi,Makaazi, Maji na Nishati,Zanzibar.
Rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984
Uteuzi huo wote unaanza leo.
Pia Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzíbar amemteua Sebtuu Mohammed Nassor kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani ya Zanzíbar.
Rais maefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha Sheria ya Baraza la Mitihani la Zanzíbar namba 6 ya 2012
Uteuzi huo umeanza tarehe 31 Oktoba 2012
Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheir amewateua Wajumbe wa Bodi ya Utumishi ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa Sheria namba 11 ya Mwaka 2003 iliyoanzishwa Ofisi ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika kifungu cha 8(1) kinachoanzisha Bodi ya Utumishi ya Ukaguzi.
Walioteuliwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikalini Othman Bakar Othman
Fatma Mohammed Said ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa Mjumbe wa Bodi
Wajumbe wengine wa Bodi ni Fatma Saleh Amour kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,
Abdalla Mohamed Mbwana na Tafana Kassim Mzee
Uteuzi huo umeanza Oktoba 27,2012
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 02/11/2012
No comments:
Post a Comment