Rais wa Uganda, Yower Museven.
Raia wa Uganda kutoka dini mbali mbali
hii leo wamekusanyika katika uwanja wa Kololo mjini Kampala kwa maombi
maalum na kutoa shukurani kwa Rais Yoweri Museveni kwa kutia saini
mswaada wa sheria unaozuia mapenzi ya jinsia moja.
Rais Museveni aliidhinisha sheria ya adhabu kali kwa Mashoga nchini Uganda mwezi Februari, kwa hatua hiyo viongozi wa dini mbalimbali wakristo na waislamu wamehimiza waumini wao kujitokeza kwa wingi katika ibaada hiyo maalum.
Hii ni mara ya kwanza viongozi wa dini
mbali mbali nchini Uganda kujitokeza kwa pamoja na kuandaa Ibaada
maalum ya kumshukuru Rais Museveni na kuliombea taifa kuepuka vitendo
vya ushoga.
Rais Museveni aliidhinisha sheria hiyo ambayo raia wengi wa Uganda wameipigia debe sana.
Ibada hiyo maalum inafanyika uwanja wa
uhuru wa Kololo mjini Kampala, baada ya karibu mwezi mmoja na nusu
tangu rais Yoweri Museveni kuiidhinisha
Tangu Rais Museveni kuidhinisha sheria
hiyo kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mataifa ya Magharibi
yakimtaka kubadili msimo wake, huku baadhi ya mataifa yakipunguza msaada
kwa Uganda lakini raia wengi wa Uganda walimsifu Rais Museveni kwa hatua yake.
Chanzo, bbcswahili
No comments:
Post a Comment