Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi
(kushoto) akiwapita walinzi wa Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Afrika uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi
Jumamosi.
Dar es Salaam. Beki wa Al- Ahly, Said
Ahmed Shedid amesema mechi ya marudiano itakuwa ngumu kwao kutokana na
kasi ya washambuliaji wa Yanga pamoja na uwezekano wa mechi hiyo
kuchezwa nje ya Cairo na El Gouna.
Yanga na Ahly zitashuka uwanjani Jumapili hii kuumana katika pambano la marudiano la Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya kwanza.
Beki huyo Shedidin alisema pamoja na
kubadilishwa uwanja huo bado wanategemea kupata ushindani mkali kutoka
kwa washambuliaji wa Yanga wenye kasi kubwa katika kushambulia.
Alisema mechi hiyo itakuwa ngumu kwao
kama itachezwa nje ya Cairo na El Gouna, ambako hali yake ya hewa
inafanana na ile ya Tanzania.
Kutokana na vurugu zilizojitokeza
kwenye fainali ya Kombe la Super Cup kati ya Al-Ahly na CS Sfaxien na
kusababisha polisi 22 kuumia, mechi hizo zitachezwa bila mashabiki.
Serikali ya Misri imesema mechi zote za Cairo zitachezwa bila ya mashabiki au kucheza kwenye Uwanja wa Jeshi wa jijini Cairo.
Naye nahodha Mohammad Yousuf,
akiuzungumzia mchezo huo wa Jumapili alisema mabingwa hao wa Tanzania
wameoneka kuwa wazuri zaidi katika kushambuliajia kwa kasi na kujilinda.
"Nidhamu na kasi yao wanapokuwa na mpira ni jambo inabidi kulifanyia kazi ya ziada kabla ya mechi yetu ya marudiano."
Yousuf alifafanua kuwa mechi hiyo
haitakuwa rahisi kwao kutokana na uchezaji wa wapinzani wao. Lakini
kurejea kwa nyota wao kama Abdullah Saeed na Sherif Abdul-Fadil ni faida
kwao.
Tayari CAF imeshamtangaza mwamuzi wa
Badara Diatta kuchezesha mchezo huo akisaidiwa na Jay Haji Abdul Aziz,
na Bangor Forbade, na mwamuzi wanne Kebbi Dauda, na msimamizi wa mchezo
huo atakuwa Massa Diarra kutoka Mauritania.
Wakati huohuo; Serikali imeitoa hofu
Yanga kwa kusema kwamba tayari imechukua hadhari ili kuhakikisha inakuwa
salama muda wote itakapokuwa Misri kwa ajili ya pambano dhidi ya Al
Ahly.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Benard Membe akizungumza jijini Dar es Salaam alisema,
wizara yake imefanya mawasiliano na Balozi wa Tanzania nchini Misri kwa
ajili ya kuhakikisha usalama wa msafara wa Yanga.
"Nichukue fursa hii kusema kwamba
serikali ipo nyuma ya Yanga kwa kuhakikisha inakuwa salama muda wote
itakapokuwa Misri kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Al Ahly.
"Tayari wizara yangu imewasiliana na
balozi wetu Misri. Watapewa ulinzi mkali na wa hali ya juu kuanzia
mazoezini hadi hotelini,"alisema Membe.
Aliongeza:"Lengo ni kuhakikisha timu
yetu haifanyiwi vioja au vituko vya aina yoyote itakapokuwa kule,
tunataka icheze mechi ikiwa huru."
Tayari uongozi wa Yanga umethibitisha
kwamba msafara wa timu hiyo utaondoka nchini kesho kwa ndege ya kuekelea
Misri tayari kwa ajili ya mchezo wao.
Chanzo, mwananchi
No comments:
Post a Comment