Waziri
wa Nchi Ofisi ya MAKAMU wa Rais anayeshughulikia Muungano Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan amechaguliwa kuwa MAKAMU wa Mwenyekiti wa Bunge la
Katiba.
Mheshimiwa Samia anaingia katika kitabu cha historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la kwanza la kuandaa KATIBA Mpya ya Tanzania baada ya kupata kura 390 sawa NA asilimia 74.6 ya kura zote 523 zilizopigwa NA wajumbe wa bunge hilo NA kumshinda mpinzani wake Mh. Amina Abdallah Amour wa Chama cha CUF aliyepata kura 126 sawa NA asilimia 24.1 ya kura zote. Kura 7 ziliharibika.
Mh. Samia Suluhu Hassan ni msomi mwenye Stashahada ya Uzamili (Masters Degree) ya Maendeleo ya Jamii katika Uchumi. Amekuwa Waziri katika WIZARA mbali mbali 3 katika kipindi cha miaka 14 Kama mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano .
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameliambia bunge la KATIBA wakati akijibu maswali ya wajumbe kuwa Amekuwa Waziri katika Ofisi ya MAKAMU wa Rais anayeshughulikia Muungano kwa miaka 4 ambapo ameweza kushughulikia kero zote 13 za Muungano isipokuwa moja inayohusu uchumi.

SOURCE: A. HAMIS
No comments:
Post a Comment