Prof.
Shivji katika kongamano lilofanyika tarehe 15/1/2011 Dar es Salaam alisema
kuwa: “ Katika nchi yoyote msingi wa uendeshaji wa nchi unategemea Katiba.
Katiba ni sheria kuu au sheria mama katika nchi yoyote. Sheria nyingine zote
zinategemea au zinatungwa kwa mujibu wa katiba, wakati mwingine katiba
hutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kijamii kati ya watawala na wananchi
(watawaliwa). Ni makubalianao ya wananchi husika juu ya ni jinsi gani taratibu
za kanuni za uendeshaji wa mambo mbali mbali katika nchi yao unapaswa
kuwa. Ni muafaka wa Kitaifa juu ya misingi mikuu ya kuendesha nchi.”
Swali
ambalo mimi najiuliza leo hii tutaipataje hii katiba bora? Katiba bora
itapatikana tu tutakuwa na bunge bora na imara ambalo litafanya shughuli zake
kwa masilahi ya wananchi wake na sio kwa kulenga kikundi Fulani au itikadi za
vyama au sehemu wanazotoka.
Tunafahamu
kuwa Bunge ni muhimili mkubwa sana wa demokrasia katika nchi yeyote ile
ambayo inajali maendeleo na demokrasia ya wananchi wake; Katiba ya Nchi ambayo
ni sheria mama katika shughuli za serikali hupitishwa na bunge maalumu ambalo
huitwa bunge la katiba; ni bunge ambalo linakuwa maalumu kwa ajili ya kazi
hiyo.
Wajumbe
wa bunge hili ni wawakilishi wa wananchi; bunge hili ambalo linakutana kwa muda
mfupi linakuwa na ajenda maalumu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa nchi inapata
katiba iliyo bora kwa taifa kwa miaka mingi ijayo.
Jambo la
kwanza katika bunge hili ambalo limeshitua wananchi wengi ni kwa wajumbe wa
bunge hili maalumu kuanza kazi kwa kuangalia masilahi yao binafsi ya kudai
Posho; kwa kweli tuache utani posho ya sh 300,000 kwa siku kweli haitoshi kwa
wakilishi wa wananchi ambao wanajua wananchi wao wanaishi katika mazingira
magumu sana? Kama wanazuoni wengi walivyoainidha kuwa agenda nyingine ni nje na
lengo na madhumuni ya mkutano huo.Suala la posho sio ajenda lakini inashngaza
kwa nini imetengenezewa kamati na kuangalia na eti wampelekee mheshimiwa
Rais mapendekezo ya mjadala huo wa ongezeko la posho.
Je mbunge
ambaye ni makini na anauchungu na nchi yake na amekubali kwenda Dodoma kwa
ajili ya kutoa mchango wake katika kuhakikisha kuwa taifa letu linapata katiba
iliyo bora anaweza kweli kukubaliana na wazo hili la ongezeko la posho? Kwa
kweli hii ni kuwapotezea watanzania raslimali zao.
Kwa nini
wawakilishi hao wasifikirie kuiomba serikali kuwaongezea mishahara watumishi
wake ili waweze kuishi maisha yaliyo bora zaidi?
Mwanzo
huu sio mwanzo mwema kwani wajumbe hao wanatupa wasiwasi sisi wananchi kweli
wanataka kutupatia katiba bora au wako pale kwa masilahi binafsi?
Nioavyo
mimi nafikiri kuwa waheshimiwa wabunge wa bunge maalumu ambao wamependekezwa na
wananchi na hatimaye kuchaguliwa na Mheshimiwa Raisi wazingatie kuwa
wanapojadili mstakabari wa sheria kuu ambayo itaongoza nchi ni vyema wajadili
na kuona umuhimu pia kuzingatia ukweli kwamba mabadiliko yoyote humpeleka
mtu upande mmoja kati ya pande mbili zinazokinzana. Kumtoa katika hali mbaya na
kumpeleka katika hali nzuri zaidi, au kutoka hali nzuri na kumpeleka katika
hali mbaya zaidi. Katika hali ya kawaida na kwa binadamu makini, hofu ya
kupoteza, yaani kutoka hali nzuri kwenda hali mbaya huwa kubwa kuliko hamu ya
kupata, yaani kutoka hali mbaya kwenda nzuri. Hili tumeanza kuliona kwani
wameanza kujadiliana kuhusu wao “posho” na pia wanaangalia zaidi itikadi ya
vyama vyao vinataka nini?
Waheshimiwa
wabunge wa bunge maalumu wajue kuwa kazi sio ngumu sana kwani wana sehemu
ya kulinganisha nini watanzania wanataka kwa miaka mingine 300 inayokuja;
wanayo katiba ya sasa kama wamekuwa na muda wa kuielewa na kusikiliza maoni ya
wananchi basi wasipoteze mazuri yaliyopo katika katiba ya sasa, ni vizuri
mabadiliko hayo yafanyike kwa umakini mkubwa. Naendelea kukumbusha kuwa katiba
ni Nguzo kubwa ya demokrasia katika
Jambo
nyingine ambalo limejitokeza na kuchelewesha kuanza kwa bunge hilo ni utaratibu
gani utumike katika kupitisha vipengele katiba mpya je watumie kura za siri au
kura za wazi. Demokrasia ya kweli iko inatakiwa iwe wazi wajumbe wasiwe na hofu
ya kuonekana wasaliti na wanafiki mbele ya wananchi wao na vyama vyao.
Utaratibu wowote ambao utapitishwa na wengi ndio uwe msingi wa demokrasia;
kwani demokrasia ni sauti ya wengi ; japo John Locke aliwahi kuhoji je wachache
je hawana nafasi katika demokrasia hata kama mchango wao ambao wanatoa ni mzuri
ukilinganisha na mchango walio wengi ambao pengine huishia kufuata mkumbo?
“For one,
a defining characteristic of democracy must be the people's right to change the
majority through elections. This right is the people's "supreme
authority." The minority, therefore, must have the right to seek to become
the majority and possess all the rights necessary to compete fairly in
elections—speech, assembly, association, petition—since otherwise the majority
would make itself permanent and become a dictatorship. For the majority,
ensuring the minority's rights becomes a matter of self-interest, since it must
utilize the same rights when it is in minority to seek to become a majority
again”. John Locke.
Tunawaomba
wajumbe wa bunge la katiba kuvumiliana kwani kila mwakilishi anauwezo tofauti
katika kujieleza. Tukumbuke kuwa Uwezo wa kusema na kujenga hoja hutofautiana
kati ya mtu na mtu, na kwa wakati huo huo anasema kwa ya kundi
lililo mchagua. Lakini tumeshajionea wenyewe kuwa wawakilishi wetu wameamua
kulitumia Bunge kukidhi matakwa yao na wala sio ya wananchi wao.
Haya yote
yametupelekea tuanze kuona kuwa kuna kitu kinakosekana kwa waheshimiwa
wawakilishi wetu ndani ya bunge la katiba ni dhana ya uongozi bora. Hapa
wabunge wetu wanaweza wakawa na mapungufu yanayotokana na ufahamu,
ubunifu, maadili, mfano bora kwa wengine; mwajibikaji; mwenye uwezo wa kutoa
ushauri.
Je
wabunge wetu ambao tunategemea watuletee katiba mpya wanajifahamu
mwenyewe. Pili je wananfahamu itikadi, uwezo, mwelekeo na malengo ya wale
anawaongoza. Na tatu wanajua mazingira ya uongozi wao.
Kwa kweli
hatutamani kabisa bunge letu liwe la kifisadi na kinafiki katika jambo hili
muhimu kwa taifa; kwani kwa kufanya hivyo nchi itapoteza mwelekeo kwa kukosa
Katiba iliyo bora. Uongozi wa kifisadi unawavutia sana watu wenye tamaa ya mali
kuingia katika siasa ili wakaibe hivyo badala ya siasa inakuwa “matumizi ya
nguvu ya udikiteta”; tukikaribisha ufisadi wakati wa matayarisho ya katiba hii
mpya itatupelekea nchi kukosa katiba iliyobora kwa maisha bora ya Taifa na
hivyo katiba hiyo mpya itatengeneza ombwe la uongozi na kuwa kikwazo kikuu cha
maendeleo.
Maneno
“siasa na uongozi” yana maana sawa kwa maudhui ya makala hii. Nimekumbuka
alichokisema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipohutubia kilele cha maadhimisho
ya miaka kumi ya CCM na miaka 20 ya Azimio la Arusha mwaka 1987.
Akizungumzia
dhana ya uongozi, Mwalimu Nyerere lisema, “uongozi ni kuonyesha njia.” Kwa
maana hiyo, viongozi shurti wafahamu vema matokeo ya uongozi wao. Wasome imani
za wanaowaongoza na nyakati zilizopo ili kutambua matumaini ya umma kimaisha.
Yapasa viongozi watambue kuwa siasa njema hutatua matatizo na shida za wananchi
zikiwemo zinazokwamisha maendeleo ya uchumi wa nchi na wa familia mojamoja.
Siasa mbaya huangusha huduma za jamii. Kwa kuwa siasa ni uongozi, basi viongozi
lazima waongoze kiadilifu, kizalendo na kwa kuzingatia hali halisi ya mambo.
Wanapaswa pia kuwa wenye huruma na imani kwa wananchi.
Basi
mwanasiasa yeyote katika nchi masikini kama Tanzania, anapochaguliwa kuongoza
popote, ajuwe anabeba jukumu la kubadilisha hali za watu kuwa nzuri. Atumie
stadi za uongozi mwema kuonyesha njia. Tabia ya viongozi kuongoza kwa kufikiria
zaidi maslahi binafsi mwiko. Viongozi wa nchi hizi masikini waangalie maisha ya
Manabii ambao waliongoza karne za mwanzo za ulimwengu. Haya ni maneno muhimu
sana hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba mpya.
Bunge la
katiba mpya tutatamani kutowaona wajumbe wenye sura mbili, yaani waoga wa
kupigania kitu bora kwa ajili ya taifa bila kujali Itikadi, dini au sehemu
anayotoka na wale wanaotafuta masilahi binafsi ya kujinufaisha wao
wenyewe. Wajumbe wa Bunge maalum itakuwa vyema kama watabadilika.
Bunge
hili tunaomba lisiwe kama bunge la Bajeti ambalo likuwa limetawaliwa na
misengwe na kulifanya lipoteze hadhi; bunge ambalo tulikuwa tunaona raha kuangalia
sio hoja bali kuzomeana, kulaumiana, kunyosheana vidole; mpaka msanii mmoja
akalitungia wimbo Bunge kama kariakoo,
Mambo
kama haya hayatalivusha Taifa letu katika maisha bora
tunayoyafikiria kwa faida ya Taifa letu, nafikiri itastusaidia sana kama wajumbe
watakuwa wakishindana kwa hoja zitakazofanikiwa kulipatia Taifa Katiba ambayo
tunahihitaji katika karne ya leo.
Bunge
imara linajengwa katika msingi wa uwazi kwa kukosoana na kuheshimiana kihoja;
ushindani na uchambuzi wa hoja ni sehemu muhimu sana katika kusaidia Taifa
kusonga mbele; wabunge wote hawawezi kamwe kuwa na mtazamo wa pamoja; Mwenyezi
Mungu ametujalia vipaji tofauti katika kufikiri na katika kutatua matatizo;
Waheshimiwa wabunge wetu ni lazima wajifunze kujenga bunge lenye ushindani
wa hoja kama sehemu ya kutatua matatizo mbalimbali. Tutaweza kushinda tu
kama tutafanikiwa kujenge jamii inayotafakari na si jamii ya kulalamika kila
wakati na kuishia kutukanana bila aibu.
Tunafahamu
kuwa Bunge ndicho chombo cha kutunga sheria na muhimili mkuu sana wa uchumi
kutokana na michango yao bungeni hasa wakati huu wa bunge la Bajeti. Bunge
linatakiwa liwe na uwezo wa kuchangia na kuandaa mazingira yanayofaa kwa
maendeleo yetu. Lakini Kama Bunge halina uwezo wa kuyaangalia
matatizo ya nchi hii na kuyatafutia ufumbuzi, basi, kuna tatizo kubwa katika
jamii yetu, kuna tatizo kubwa ambalo kama tukibweteka, litatutafuna sisi na
vizazi vijavyo.
Nafikiri
linalowezekana leo lifanyike leo kwani hakuna kesho katika maendeleo ya
binadamu kwani sisi tunaishi leo na sio kesho; kesho inabaki katika hazina ya
Muumba wetu tu;
Itafurahisha
pale tunapowaona waheshimiwa wabunge wa Bunge hili maalum, bila kujali chama
wakikubaliana hoja za msingi ambazo zinasaidia kujenga uzalendo wa kutetea
maslahi ya ya watanzania katika kutuletea Katiba mpya ambayo
haitafungamana na chama chochote cha siasa wala dini. Bunge letu Maalum
likiweza kufanya kazi yake katika msingi huu kuondoa taswira ya BUNGE LENYE
SURA MBILI NA MBAYA ZAIDI LINALOANGALIA MASALAHI BINAFSI YAKUWANUFAISHA WAO NA
KUTOKUMJALI MTANZANIA WA KAWAIDA AMBAYE NDIYE WANAYEMWAKILISHA WATAKUWA
WAMEWASALITI WANANCHI NA TAIFA LA TANZANIA.
MUNGU
IBARIKI TANZANIA TUWEZE KUPATA KATIBA ILIYO BORA KABISA
No comments:
Post a Comment