WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, March 7, 2014

Mrema: Makundi yatavuruga Katiba

 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Augustine Mrema.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Augustine Mrema, ametahadharisha kwamba siasa za makundi yaliyojipanga kwenda bungeni kutaka mambo yao yapitishwe katika Katiba mpya yanaweza kuvuruga mchakato huo na katiba mpya kushindwa kupatikana.
Alisema jana kuwa moja ya makundi hayo ni la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambalo alisema lingetaka Katiba mpya iwasaidie kuendelea kubaki madarakani na wkamba kundi hilo linataka kila kifungu kiwe bora kwao.

“Kundi lingine ni la wapinzani ambao tungetaka kanuni za kupitisha Katiba zinatusaidia kuingia madarakani. Wajumbe wanakosa msimamo,” alisema.

Alisema baadhi ya wajumbe ni vigeu geu akisema kuwa wako wanotaka waape kwa utaratibu wa makundi, lakini linapokuja suala la upigaji wa kura wanataka kura ya siri.

“Hao hao hawataki kura ya wazi, kwa nini wanataka kura ya siri na siyo ya wazi ili Watanzania wasiwaone,” alisema na kuongeza kuwa wanazungumzia katiba kwa malengo yao.

Alisema bila wajumbe haoo kutanguliza mbele maslahi ya Taifa, upo uwezekano wa wajumbe hao kuondoka Dodoma bila kupitisha Katiba.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment