Kwa matokeo haya ya Coastal U 1-1 Azam FC, Yanga
anakuwa bingwa kwakuwa Azam ina michezo miwili kama ikishinda itakuwa na 54,
pointi ambazo Azam haitaifikia Yanga ambayo inapointi 56 mpaka sasa.
Fuatilia ratiba na msimamo hapa.
Tovuti ya kandanda itawaletea takwimu za mechi zote za mshindi wa kwanza na wa
pili hapo baadae mwishoni mwa msimu.
Uchambuzi
|
Hatimaye
timu ya soka ya Dar Es Salaam Young African imechukua ubingwa wake wa 24 bila
kuingia uwanjani. Hiyo imetokana na wapinzani wake wakubwa kwenye Ubingwa kwa
mwaka huu timu ya Azam kutoa sare ya kufungana goli moja kwa moja katika mchezo
uliopigwa katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Kwa matokeo hayo Azam imefikisha point 49 na hivyo hata ikishinda mechi zake 2 zilizosalia itafikisha point 55 ambazo tayari zimekwisha pitwa na Yanga yenye point 57. Yanga pia imebakiza michezo miwili yote itapigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam
Kwa matokeo hayo Azam imefikisha point 49 na hivyo hata ikishinda mechi zake 2 zilizosalia itafikisha point 55 ambazo tayari zimekwisha pitwa na Yanga yenye point 57. Yanga pia imebakiza michezo miwili yote itapigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam
Kimsingi dalili za Yanga kuchukua Ubingwa zilijionyesha tangu awali na tunaweza
kusema imepata ubingwa iliyostahili.
Pamoja na kuanza ligi kwa kususasua kwa kutoa sare na Prison ya Mbeya na kufungwa mechi ya pili kwa mabao 3 kwa nunge, Yanga ilibadilika na kuanza kushinda mfululizo na mpaka pale mzunguko wa kwanza ulipokuwa unamalizika, tayari ilikuwa inaongoza kwa pointi 5 mbele ya Azam na kuipoteza kabisa Simba kwa pointi 6 zaidi na kufaulu kuziba pengo la pointi 8 ilizokuwa nazo samba dhidi ya Yanga.
Pamoja na kuanza ligi kwa kususasua kwa kutoa sare na Prison ya Mbeya na kufungwa mechi ya pili kwa mabao 3 kwa nunge, Yanga ilibadilika na kuanza kushinda mfululizo na mpaka pale mzunguko wa kwanza ulipokuwa unamalizika, tayari ilikuwa inaongoza kwa pointi 5 mbele ya Azam na kuipoteza kabisa Simba kwa pointi 6 zaidi na kufaulu kuziba pengo la pointi 8 ilizokuwa nazo samba dhidi ya Yanga.
MAPINDUZI
|
Mafanikio
ya Yanga yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uongozi ulioingia baada ya
kushinikiza kuondolewa kwa uongozi wa Lord Nchunga aliyeonekana kushindwa
kuongoza timu na kupelekea Yanga kumaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya 3
nyuma ya Simba waliokuwa mabingwa na Azam iliyoshika nafasi ya 2. Kumaliza
nafasi ya 3 ilikuwa matokeo mabaya zaidi kwa Yanga katika miaka ya hivi
karibuni lakini kibaya zaidi walifunga dirisha la msimu kwa kupatwa kipigo cha
aibu cha magoli 5 kutoka kwa hasimu wake Simba.
UONGOZI BORA
|
Kiukweli
uongozi wa Yanga umekuwa makini sana kuanzia katika mfumo, uendeshaji wa timu,
huduma kwa wachezaji na menejimmenti kwa ujumla. Chini ya uongozi wa Yusuph
Mehboob Manji, Yanga hawajatetereka na wamekuwa mfano wa kuigwa katika mambo
yake kuhusu klabu
USAJILI
|
Ili
timu ifanikiwe ni lazima uwekezaji uanzie kwa kusajili wachezaji wenye kiwango.
Katika hilo, Yanga hawakufanya ajizi, walisajili wachezaji wenye kiwango kama
akina Mbuyu Twite, Frank Domayo, Nizar Khalfan, Kelvin Yondani, Ally Mustapha (Barthez)
na Simon Msuva na kuwaongezea mikataba wachezaji wengine wenye viwango kama
akina Kiiza (Diego) na Niyonzima (Fabregas). Ukiangalia na ukajaribu kuwa
makini, utagundua kuwa Yanga ndiyo iliyosajili kwa umakini zaidi labda
ikikaribiana na Azam
MAANDALIZI YA TIMU
|
Hapa
pia YANGA walikuwa makini, walimsikiliza kocha kuangalia program zake na
kuzifuata. Itakumbukwa kwamba timu ilipata michezo kadhaa ya kujipima nguvu na
hata kuweka kambi nje ya nchi (Uturuki) kama ilivyopendekezwa na kocha
ARI YA WACHEZAJI
|
Ari
ya wachezaji wa Yanga kusaka ushindi ilikuwa juu. Hata kama timu ilicheza na
kushindwa kupata pointi yeyote katika mchezo mmoja, timu ilijipanga na kupata
pointi katika mchezo uliofuata. Kitu kikubwa zaidi, wachezaji walichukulia kila
mechi kama fainali kwao na walikuwa na uchu wa kupata pointi kwa mchezo
UMOJA NA MSHIKAMANO
|
Kulikuwa
na umoja na mshikamano baina ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Hii
iliwawezesha kuelekeza nguvu zao katika michezo inayowakabili badala ya kushughulikia
migogoro isiyokuwa na tija klabuni.
JE AZAM ALISTAHILI
KUSHIKA NAFASI YA PILI
|
Ndiyo
na hata ubingwa pia kwani sifa zote zilizotajwa hapo juu pia Azam alikuwa nazo.
Kimsingi kama kuna klabu ambayo ilikuwa inawanyima usingizi viongozi wa Yanga,
benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla basi ni klabu ya Azam. Walijipanga na
wanastahili heshima yao
Hongera Yanga kwa kurejesha Ubingwa wenu mliopokonywa na Simba msimu ulioisha na hongera Azam kwa kushika nafasi ya pili na kupata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa. Safari moja huanzisha nyingine. Wito wangu kwenu (Yanga na Azam) mjiandae vyema ili kuepuka aibu kama iliyowakuta wenzenu Simba
Kwa upande wa mahasimu wa Yanga timu Ya Simba msimu huu haukuwa mzuri sana kwenu. Kimsingi, migogoro na soka havikai pamoja. Nawaomba make chini na kujipanga upya mkisahahihisha yaliyojitokeza ili yasijitokeze tena na kwa kufanya hivyo mtarudisha ushindani uliaonza kupotea
Source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment