CHARLES
Montesque ni mwanafalsafa mkongwe aliyezaliwa mwaka 1689 nchini
Ufaransa. Ndiye aliyejenga hoja ya kuwa na dola yenye mihimili mitatu
huru.
Kwa mujibu wa Montesque, Dola haina budi kutenganisha mamlaka ya
taasisi hizi tatu. Ni muhimu kwa mihimili hii mitatu kuwa huru. Ifanye
kazi kwa kujitegemea. Kuwepo pia na mazingira ya mikono yote mitatu
kudhibitiana.
Mihimilimitatu ya dola ni; Utungaji sheria (Bunge) Utawala (Serikali)
na Hukumu (Mahakama). Kuna wenye hoja ya kwamba mikono hii mitatu iwe
na ushirikiano wa karibu.
Montesque anapingana na hoja hiyo, anaamini kutenganisha mamlaka ya
mihimili hii mitatu ya dola kunaipa uhuru kamili wa kufanya kazi zake
bila kuingiliana. Hilo ni muhimu ili kuwepo na utawala bora uliojengeka
katika misingi ya haki.
Katika nchi zetu hizi tunahitaji rais (serikali) yenye nguvu za
kikatiba, bunge lenye nguvu za kikatiba na mahakama huru yenye nguvu za
kikatiba. Mahakama zenye majaji wasioteuliwa na rais. Kwamba mikono
hii mitatu iwe huru na yenye majukumu ya kudhibitiana kwa maslahi ya
nchi. Tuandae katiba yenye kulipa bunge uwezo zaidi wa kufanya maamuzi
ya kikatiba. Bunge ndilo mwakilishi wa wananchi.
Tuwe na Mahakama Kuu Huru ya Katiba. Mahakama yenye jukumu la
kutafsiri sheria na maamuzi yote yaliyofikiwa na Bunge. Mahakama ya
Katiba iwe ni chombo cha juu kitakachoshughulikia mashauri ya ukiukaji
wa sheria na maamuzi ya Bunge. Iwe na uwezo wa kisheria wa kupitisha
hukumu kwa kuzingatia sheria za nchi bila kuathiriwa na Serikali au
Bunge.
Kwa mujibu wa Montesque, kama bunge halitakuwa na nguvu, kuna hatari
ya bunge hilo kuchukua nafasi ya serikali na kwa maana hiyo utaratibu
mzima wa mgawanyo wa madaraka ya dola kwa mihimili hii mitatu utakufa.
Montesque anabainisha pia; kuwa endapo mawaziri ambao ni watekelezaji
wa maamuzi ya bunge watatoka miongoni mwa wabunge, basi, hakutakuwa
tena na uhuru, kwani serikali yenye mamlaka ya utekelezaji itakuwa
imechanganyika na bunge.
Rais apewe madaraka ya kuchagua mawaziri, lakini, watoke nje ya
bunge. Hata kama rais atamteua waziri ambaye pia ni mbunge, basi,
mbunge alazimike kuachia kiti chake cha ubunge na atafutwe mwakilishi
mwingine wa wananchi. Haiwezekani kutumikia mabwana wawili kwa wakati
mmoja.
Na kuna hoja hii ya kuwapo ama kutokuwapo kwa wagombea binafsikatika
chaguzi zetu. Tunapaswa kujiuliza;je, ni wakati sasa wa kuwa na
wagombea binafsi? Swali hilo linatutaka kuumiza zaidi vichwa vyetu.
Maana, maamuzi yatokanayo na vifungu vya sheria ya vitabuni ni jambo
moja, lakini hali halisi katika jamii tunayoishi ni jambo jingine
kabisa.
Kwa kuziangalia jamii nyingine na kulinganisha na hapa kwetu, mimi
nadhani,kuwa nchi yetu haijawa tayari kuruhusu wagombea binafsi katika
utaratibu usiotokana na vyama vya siasa.
Nasema hivi kwa kuzingatia kuwa nchi yetubado ni changakidemokrasia.
Demokrasia hukua kulingana na hali halisi ya nchi.Ni vema na ni
busara kwawagombea binafsi wakatokana na vyama na waruhusiwe tu katika
nafasi ya udiwani, ubunge na useneta, na si katika nafasi ya urais.
Kwa kuweka msisitizo; kusiwe na mgombea binafsi katika nafasi ya
urais. Mgombea urais kikatiba atokane na chama cha siasa. Apitishwe na
idadi ya wanachama itakayokubalika, mathalan, awe ni Mtanzania
aliyepigiwa kura na kupitishwa na wanachama wa chama chake wasiopungua
1,000.
Tusiruhusu mazingira ya Mtanzania aamke tu Kamachumu au Masaki na
amwambie mkewe au mumewe kuwa; “ Naenda kuchukua fomu ya kugombea
urais!”.Katika mazingira ya nchi zetu hizi, huko ni kukaribisha
uwendawazimu, na mwishowe ikulu zetu zitakaliwa na wendawazimu au watu
wasio hata na uwezo wa kuongoza klabu ya soka lakiniwana pesa,
umaarufu na mbinu za kufika ikulu.
Hivyo basi, Katiba ijayo ingewekautaratibu wa kuruhusumgombea
binafsi anayetokana na chama cha siasa katika ngazi ya udiwani, ubunge
na useneta, si urais.
Katika utaribu huu wanaonawania ubunge katika jimbo X watapigiwa
kura na wanachama wenzao katika idadi ya wanachama itakayokubalika.
Atakayeongoza katika kura atakuwa ni mgombea ubunge kuwakilisha chama
chake.Huyo atapewa pia msaada wa kukampeni na chama chake ikiwamo fedha
za kampeni.
Mgombea ubunge huyo atatambuliwa rasmi na chama chake. Lakini
wagombea wengine walioshindwa katika kura wana hiari ya kusimama
wenyewe kama wagombea binafsi. Wajinadi wenyewe na kwa gharama zao na
bila kupigiwa debe na chama chao. Wakibahatikakuchaguliwa na wananchi
na kuingia bungeni, basi, wataingia bungeni kama wagombea binafsi
lakini wakiwakilisha itikadi na sera za vyama vyao.
Utaratibu wa wagombea binafsi wanaotokana na vyamautasaidia pia
kuimarisha vyama vya siasa. Tumeamua kuingia katika mfumo wa vyama
vingi na si mfumo wa wagombea wengi binafsi. Chama ni wanachama na
vikao vya chama. Ni itikadi na sera.
Kuruhusu mgombeabinafsi asiyetokana na chama ni kuhujumuna kupoteza
maana nzima ya uwapo wa siasa za vyama vingi. Na swali ni je, hatuoni
kuwa umefika wakati wa kuondokana na uchaguzi wa rais na badala yake
rais atokane na chama kilichopata kura nyingi? Hili nalo linajadilika.
source: Raia Mwema :Maggid
No comments:
Post a Comment