Mbunge wa Mbeya mjini- Joseph mbilinyi aka Sugu akiunguruma kwenye mkutano mkubwa wa hadhara wa chadema kwenye viwanja vya Uwanja wa
Mwembetogwa iringa jana
Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika
akihutubia mamia yawatu waliofurika katika mkutano wa hadhara
uliofanyika jana katika vinwaj vya Mwembetogwa mjini Iringa
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa
Kushoto akipitia katiba kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliyofanyika
iringa jana kulia kwake ni mbunge wa jimbo la ubungo Mh John Mnyika
Sehemu ya mamia ya wafuasi wa chadema wakisiliza hotuba mbalimbali kutoka kwa viongozi mbalimbali wa chama hicho viwanja vya Uwanja wa
Mwembetogwa iringa jana. Picha Zote na Chadema na Said Ng’amilo
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji
Peter Msigwa amemlipua kigogo mmoja wa juu wa CCM (jina tunalihifadhi
kwa kuwa hakupatikana kujibu tuhuma hizo), kuwa ndiye kinara wa biashara
haramu ya pembe za ndovu na utoroshaji wa wanyama nchi za nje.
Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa
Mwembetogwa, Iringa jana, Mchungaji Msigwa alisema anashangaa Serikali
ya CCM kushindwa kumchukulia hatua.
Mchungaji Msigwa alidai kuwa tembo wapatao 75 wamekuwa wanauawa kila siku kutokana na tatizo hilo kufumbiwa macho na Serikali.
Alidai kuwa pamoja na Waziri wa zamani wa
Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige kujiuzulu mwaka jana kutokana na
kashfa ya kutorosha twiga, Serikali ilitakiwa kuwafuatilia wahusika
wote.
“Kinara wa biashara haramu ya uuzaji wa pembe za ndovu anajulikana, sasa inakuwaje Serikali inashindwa kumkamata?” alisema Msigwa na kuahidi kulipua mabomu zaidi atakaporudi bungeni kwa maelezo kuwa anao ushahidi wa suala hilo.
“Kinara wa biashara haramu ya uuzaji wa pembe za ndovu anajulikana, sasa inakuwaje Serikali inashindwa kumkamata?” alisema Msigwa na kuahidi kulipua mabomu zaidi atakaporudi bungeni kwa maelezo kuwa anao ushahidi wa suala hilo.
Huo ulikuwa mkutano wa mwendelezo wa wabunge wa Chadema waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kuwapasha wananchi sababu ya kuchukuliwa hatua hiyo.
Wabunge hao walisimamishwa na Naibu Spika, Job Ndugai kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje ya ukumbi, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu. Wabunge waliosimamishwa pamoja na Lissu ni Godbless Lema (Arusha Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini), Ezekiah Wenje (Mwanza Mjini) na Msigwa.
Hata hivyo, Lema na Lissu hawakuwapo katika mkutano huo wa jana ambao pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Mnyika kutoa hoja binafsi
Katika mkutano huo, Mnyika aligawa fomu kwa wananchi kuomba aungwe mkono wakati atakapotoa hoja binafsi bungeni juu ya mfumuko wa bei na umaskini nchini.
Mbunge huyo alisema wananchi wanakabiliwa na maisha magumu kutokana na hali mbaya ya uchumi.
“Napata uchungu ninavyoona Watanzania wakiishi maisha magumu kwa hiyo naandaa hoja binafsi ya kuwasilisha bungeni ili umma uelewe umuhimu wa suala hili,” alisema Mnyika na kuongeza kwamba atagawa fomu hizo kila atakapohutubia mikutano ya hadhara.
Dk Slaa na Usalama wa Taifa
Katika mkutano huo, Dk Slaa alidai kuwa maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wamegawanyika kutokana na makundi ya wanaotaka kuwania Urais mwaka 2015 kupitia CCM.
Dk Slaa alisema mgawanyiko huo ndiyo chanzo cha siri nyingi za idara hiyo kuvuja.
Aliwatuhumu baadhi ya wanachama wa CCM akidai kuwa wamekuwa wakiwavuta baadhi ya maofisa katika idara yao ili kuwasaidia kwenye harakati zao.
source: mwananchi
No comments:
Post a Comment