Hiki ni Kituo kikuu cha Umeme cha
Mtoni Unguja.ambacho tayari Mradi wake uliofadhiliwa na MCC Marekani
umezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,kwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la
‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo, pia Balozi wa Marekani
Nchini Tanzania ALfonso Lenhardt, alihudhuria katika uzinduzi
huo,utakaochukua Ukubwa wa Kilowati 100.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akikata utepe na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes
Ceo, kama ishara ya uzinduzi mradi wa Umeme wa Njia ya Pili ,kutoka
Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la
Misaada la MCC la Marekani,hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo kikuu
cha Umeme Mtoni Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuzindua mradi
wa Njia ya Pili ya Umeme,kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa
umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,hafla hiyo
ilifanyika jana katika kituo kikuu cha Umeme Mtoni Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu
wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo,(katikati)
na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania ALfonso Lenhardt,wakipata maelezo
ya kiutendaji kazi katika kituo kikuu cha umeme kutoka Ubungo Dar es
Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la
Marekani,kwa Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali,(kushoto)
baada ya ufunguzi rasmi jana.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.-Zanzibar
No comments:
Post a Comment