Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano Samia Suluhu Hassan
akipata Maelezo kwa Mhadhiri Mwandamizi wa Taasisi ya Sayansi ya Bahari
Dkt Narriman Jiddawi juu ya Utunzaji wa Samaki Aquarium wakati wa Ziara
ya waziri huko Zanzibar
Mhadhiri Mwandamizi wa Tasisi ya Sayansi ya Bahari ya Chua Kikuu cha
Dar es Salaam Dkt NarrimanJiddawi akimuonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan aina ya Kasa katika chumba
cha Kutunzia samaki[AQUARIUM}wakati wa Ziara ya Kutembelea Tasisi za
jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizopo Unguja .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan
akipata Maelezo juu ya Ujenzi wa Kituo cha tasisi ya Sayansi za Bahari
kilichopo Chukwani Unguja kwa Kaimu Mkurugenzi Dkt Christophet Muhando
wakati waziri alipofanya Ziara ya Kutembelea Tasisi za Jamhuri za
Muungano wa Tanzania zilizopo Unguja [PIcha na Ali Meja]
ZAIDI ya shilingi bilioni
14 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa chuo cha Taasisi ya Sayansi za Bahari kilichopo Buyu wilaya ya
Magharibi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Hayo yamesemwa leo huko
Forodhani mjini Zanzibar na Muhadhiri Dkt. Ntahondi Nyandwi wakati alipokuwa
akisoma ripoti ya chuo hicho na rasilimali zake mbele ya Waziri anae
shughulikia masuala ya Muungano Samia Suluhu Hassan aliyekuwa katika mfulilizo
wa ziara yake kuzitembelea Taasisi za muungano hapa Zanzibar.
Amesema fedha hizo zitahitajika
ili kukamilisha ujenzi wa jengo lote na miundombinu ikiwemo vifaa vya maabara, sehemu za
wanafunzi wa uzamili, zamivu, kumbi za mikutano, ofisi za programu za
kimataifa, ofisi za wageni wa kimataifa na mengineyo.
Dk. Nyandwi amesema
kupatikana kwa fedha hizo kutakamilisha
mahitaji hayo na mengine ambapo kwa sasa ujenzi huo umefikia hatua nzuri
na wameshatumia zaidi ya bilioni nne
kwa kujenga miundo mbinu mbalimbali ikiwemo ofisi za viongozi na madarasa.
“Kwa vile pesa za kumlipa
mkandarasi hazikupatikana kwa wakati na hakukuwa na uhakika kuzipata, ujenzi
ulisimama Agosti 2008 na mkandarasi aliondoka lakini kwa sasa ujenzi unaendeleo
taratibu”alisema Nyandwi . Aidha alifahamisha kuwa ujenzi huo unaendelea kidogo
kidogo kadri fedha zinavyo patikana
baada ya kumuomba mkanda rasi awapunguzie gharama na kuweza kumaliza mipango ya
awamu ya kwanza na ya pili.
Nae Waziri wa
Nchi Afisi ya Makamu wa Rais,
Muungano Samia Suluhu Hassan amesema kuwa atamuagiza Mkuu wake wa kazi
kuja Zanzíbar kujionea na yeye Jengo hilo hatua ilio fikiwa.
Aidha alisema kua ujenzi
huo utaendelea kidogokidogo mpaka utapomalizika. Maendeleo ya ujenzi wa Taasisi
ya sayansi Baharini ni moja ya Taasisi za Chuo
Kikuu cha Dar-es Salaam kampasi ya
Mwalimu Nyerere ambapo umuhimu wa Taasisi hiyo ulianza kujitokeza Mwaka 1978
chini ya sheria Na. 12 ya 1970 ya chuo kikuu cha Dar-slamu kwa tamko la
Serikali Na. 34 lililo pitishwa tarehe 16 march 1979.
Chuo hicho kumalizika kwake
kufanya kazi za kutafiti nyanja zote za Sayansi za Baharini, kutoa mafunzo ya
uzamivu, uzamili katika sayansi ya Bahari ,kutoa ushauri wa kitalamu ,kutoa
mafunzo ya Shahada ya kwaza kwa kulingsana
na mahitaji ya Taifa la Tanzania kama sehemu ya Taluma kwa vitendo.
IMETOLEWA NA IDARA YA
HABARI MAELEZO ZANZIBAR LEO 5/4/2013
No comments:
Post a Comment