HATIMAYE ubishi wa timu za Azam Fc wana lambalamba na wekundu wa
msimbazi Simba umemalizika leo hii uwanja wa taifa baada ya kuchoshana
nguvu kwa kufungana sare ya 2-2.
Matokeo hayo, yanaiongezea Azam pointi moja na kufikisha 47
kibindoni ikibaki nafasi ya pili, nyuma ya Vinara Yanga wenye pointi
52, wakati Simba wanasalia nafasi ya nne kwa pointi zake 36, nyuma ya
Kagera Sugar yenye pointi 37 nafasi ya tatu.
Hadi kipindi cha kwanza cha kipute hicho kulichochezeshwa na mwamuzi
Orden Mbaga kinamaliziaka, Mnayama alikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Nyota na Chipukizi wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ alifunga mabao
yote mawili kwa upande wa klabu yake akiunganisha pasi nzuri za winga
mwenye kasi Mrisho Khalfani Ngasa aliyeaambaa na gozi wingi ya kushoto.
Kipre Tchetche aliifungia Azam kwa penalti dakika ya 29, baada ya
Khamis Mcha ‘Vialli’ kuangushwa kwenye eneo la hatari na William Lucian
‘Gallas’.
Refa Orden Mbaga alimpandisha jukwaani kocha Muingereza wa Azam,
Stewart Hall dakika ya 31 kwa kutoa maneno machafu, akilalaimikia
uchezeshaji wa refa huyo.
Kipindi cha pili, Azam walirejea kwa nguvu na kutaka kujinusuru na
kipigo na walitimiza ndoto yao baada ya Humphrey Mieno kuunganisha
shuti la mpira wa adhabu lililopigwa na kiungo Khamis Mcha
‘Vialli`’katika dakika ya 72 na kuzamisha gozi nyavuni..
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo Afisa habari wa klabu ya Azam Fc
Jafar Idd Maganga amesema wamepokea matokeo kwa mikono miwili kwani ndio
soka hilo.
Idd alisema “Tulisema tangu awali kuwa simba ni wazuri na tulikuwa
tayari kupokea matokeo yoyote yale, tumetoa sare nao lakini tunajipanga
kwa mechi zijazo”.
Kwa uapnde wa simba kupitia kwa kocha msaidizi Jamhuri Kiwhelu Julio
alisema bado wanahitaji kupata muda wa kutosha kwani ndio kwanza timu
inaanza kushika kasi.
“Wana Simba tuwe na umoja, timu imecheza vizuri na tunamshukuru mungu
kwa kupata pointi moja na kwa pamoja tunatakiwa kusonga mbele”. Alisema
Julio.
kikosi cha Simba SC kilikuwa; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’,
Miraj Adam, Mussa Mudde, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Haroun
Chanongo/Edward Christopher, Abdallah Seseme, William Lucian/Mwinyi
Kazimoto, Ramadhani Singano na Mrisho Ngassa/Fliex Sunzu.
Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika,
Joackins Atudo, Kipre Balou, Luckson Kakolaki/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk,
Salum Abubakar, John Bocco/Abdi Kassim, Humphrey Mieno/Jabir Aziz na
Kipre Tchetche
(Chanzo: www.fullshangweblog.com)
No comments:
Post a Comment