WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, April 22, 2013

HILI NI BUNGE TULILOLICHAGUA



 
 Sehemu ya Bunge la Tanzania

Mheshimiwa Anna Makinda Spika wa Bunge

Mheshimiwa  Naibu Spika Job Ndugai

  • “Siwezi kuzungumza na mbwa, nazungumza na mwenye mbwa” au “Baraza la Mawaziri ni wapumbavu na kuna wabunge wenye mimba zisizotarajiwa.”

  • JE KATIBA MPYA ITATUSAIDIA SISI KAMA TAIFA KUTUPA NAFASI NZURI YA KUPANGA NI KUCHAGUA BUNGE IMARA KWA MASILAHI YA TAIFA LETU?

Ndani ya Ya Taifa letu leo hii mambo mengi  hayendi vile ambayo  wengi tumekuwa tukitegemea na kufikiria. Najaribu kujiuliza tatizo hasa liko wapi? Mbona nchi nyingine za kiafrika kama sisi zinaendelea kwa kasi kubwa tu nchi kama Rwanda kwa mfano wanasonga mbele pamoja na matatizo mazito ya vita ambavyo vimekabiliwa huko nyuma siri ni nini na je bunge lao linafanya kazi kama bunge letu?

  • Je tatizo letu liko wapi nikwa sababu ya Kuchagua kwetu  au  kupanga kwetu.

  •  Je unafikiri tumepanga vizuri au tumechagua vizuri au kimojawapo hatujakifanya vizuri?

  • Au ni kushindwa kwetu katika kutekeleza kile tulichochagua ndiko kunatupelekea kwenye matatizo yanayotusumbua leo na wabunge wetu bila aibu wanaona fahari kutumia lugha za matusi wakati wa vikao vyao?

Ni wakati umefika sasa kama taifa tunaanza kujitia uchaguzi wetu na lazima tukubali kuwa maendeleo yoyote yale yatatokanana kuchagua kwetu , kwani tukichagua vizuri tutajikuta tunaweza kupanga vizuri!

Je mfano tatizo la wabunge wetu na bunge letu pamoja na kutumia pesa nyingi za walala hoi na kwa makusudi kabisa wanaacha hoja za msingi za kumkomboa mtanzania na kutumia muda mwingi kuanza kujadili mambo yao binafsi kwa faida ya wao wenyewe “ madaraka”; kwa nini wqasitumie muda mwingi pengine kutafuta suluhu ya tatizo la “Elimu” kwa kuangalia tatizo letu liko wapi? 

  • je mfumo tuliochagua ndio tatizo au tumeshindwa kupanga vizuri? 

  • Je mifumo yetu ya elimu inawasaidia wahaitumu nini kwa msingi upi? 

  • Je wahitimu wetu wananafasi ya  kuweze kujiajiri katika kazi mbali mbali.

tulitegemea jukumu moja kubwa wabunge wetu ni kujadili matatizo yetu kwa uwazi kabisa na kuikosoa serikali katika misingi mizuri ya kidemokrasia kwa kuangalia matatizo ambayo kama taifa yanatusumbua sasa wadau wengi wananishia kusema kuwa tulipotoka ni afadhali kuliko tunakokwenda,maisha leo yanaonekana magumu kwa wengi na mazuri kwa wachache; serikali yetu inaonekana kushindwa kuhimili mfumko mzito wa rushwa na ufisadi kuliko ilivyokuwako huko nyuma.

Je tatizo Tunachagua mambo mengi kwa kufanya mambo kwa mazoea. Mfano tumeuma kabisa kilimo ambacho ndicho chanzo ya maendeleo ya viwanda, na viwanda ambavyo vilikuwako vyote tumewauzia watu ambao hawana dhamira ya kuinua uchumi mdogo; kwa maneno mengine tungeweka kipaumbele katika kuimarisha uchumi mkubwa unaonyanyua uchumi mdogo.

mambo ya msingi hapo ni miundo mbiu na elimu kwa ujumla wake.

 

Ukiangalia fafasa ya Nyerere na ujamaa ilikuja kama sera mpya ya kuwaunganisha watu maisha bora ya pamoja. Sera ilikuwa ni kuwaunganisha watanzania, wazalishe pamoja na kufaidi matunda ya ujamaa pamoja. Nchi isiwe na wenye nacho na wasionacho.  

Taifa letu hivi sasa kumekuwa na kilio kikubwa  tumetoka kabisa katika utaratibu wa wengi kuchagua na tunakokwenda sasa ni katika sera ya kuchaguliwa na kupangiwa lakini utaratibu wa kupanga lazima kwanza uwanufaishe wachache  kwa masalahi binafsi, nini kitajitokeza hapa ni haki ya kuingilia  kuchagua na kuchaguliwa

Kwa hivi sasa Kupanga na Kuchagua kwa masilahi ya Taifa kumehusishwa sana na tatizo la rushwa ni adui wa haki, na kwa hakika hakuna mtu anayeipenda rushwa. Lakini rushwa katika nyakati za chaguzi zetu imekuwa ni kama jambo la kawaida. Katika taifa lolote linalohitaji kuwa na demokrasia ya kweli katiba ya nchi huundwa kwa kuzingatia matakwa na mahitaji ya msingi ya wananchi wake hasa kwa vile wananchi ndio msingi wa mamlaka yoyote ile. Hii ni kwasababu katiba ndio yenye kuweka mipaka ya kila moja ya asasi katika jamii.

 
Hoja ya msingi katika wazo hili nzima ni kuendelea kuwaomba waheshimiwa wabunge kuwa tumewachagua ili watusaidie 
“kulijenga taifa”. Yaani, wabunge watumie vikao vyao vya bunge katika kuwasilisha hoja kwa kuvumiliana na kuleta mijadala yenye tija ili tuweze kupima tulikotoka, tujue ni wapi tumefanya makosa, na kutoka hapo tusonge mbele upya kwa kuangalia jinsi gani tutafika huko kwa majadiliano ya hoja na sio unafiki wa kisiasa na kukimbilia kutafuta madaraka na kutumia hoja za matusi.

Tunahitaji kurudi kwenye misingi ya “kupanga ni kuchagua” iliyotolewa na Baba wa Taifa miaka 50 iliyopita. Vinginevyo tutaendelea kuburuzana tu.

Waheshimiwa wabunge waepuke tatizo kubwa ambalo kama taifa tunalo la mazoea vya kunyonga. Hakuna kitu kibaya kama kuzoea mambo rahisi rahisi na njia za mkato.

Kwa nini nimesema kupanga ni kuchagua? Ni kwa sababu kama unataka maendeleo, lazima uwe tayari kuingia kwenye ushindani wa hoja tuweze kumwondoa mtanzania ,masikini kutoka katika lindi la umasikini. Ni muhimu viongozi wa Bunge wakazingatia kwamba watazamaji na wasikilizaji wa vipindi vya Bunge hawapo kwa ajili ya kushuhudia umahiri wa kuchambua matusi na kuyanyumbulisha. Wana hamu na hamasa ya kutazama na kusikiliza jinsi ambavyo wabunge wao wanaibua hoja zinazohusu maendeleo ya maisha yao na nchi yao.

 

Nafikiri tunatakiwa kuwa makini tunapochagua ili tuweze kupanga vizuri kwa masilahi ya Taifa letu.

No comments:

Post a Comment