Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia sherehe hizo.
Rais
Jakaya Kikwete, akiingia uwanja wa Uhuru akiwa ndani ya gai la wazi
wakati alipowasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuwaongoza wananchi katika
shambra shambra za sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange. Katika
kuadhimisha sherehe hizo, Rais Kikwete, ametoa msamaha kwa wafungwa
wapatao 4180 kwa nchi nzima, huku msamaha huo ukiwa hauwahusu, Wafungwa
wanaotumikia kifungo cha maisha, Kifungo cha ubakaji, wezi wa magari,
Rushwa, Matumizi mabaya ya Madaraka na Kunyongwa.
Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete
akikagua gwaride la heshima wakati wa sherehe za miaka 49 ya Muungano
kwenye Uweanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana
Rais
mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume (kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu
mstaafu, Edward Lowassa
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idii (kulia) akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Othmani Makungu
Rais wa
Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif
Shalif Hamad wa pili kutoka (kulia), Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi
Seif Ali Idd na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Othmani Ramadhani Makungu wakiwa katika
maadhimisho hayo.
Rais Jakaya, akisalimiana na baadhi ya viongozi baada ya kuwasili
uwanjani hapo.pichani akisalimia na makamu wa Rais Dr Gharib Bilal
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bila,
Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Mama
Karume na baadhi ya viongozi wakisimama kumpokea Rais Kikwete wakati
akiwasili uwanjani hapo.
Viongozi wa
kiatifa wakimba wimbo wa Taifa. Kutoka kushoto, Rais mstaafu, Ali Hassani
Mwinyi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, mke wa Rais
Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali
Mohamed Shein, Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali
Davis Mwamunyange, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Mama Fatma Karume.
Askari wa Jeshi la Magereza wakipita mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima.
Jeshi la Wanamaji (Nevy)
Kiapo
cha Utii kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais
Jakaya Kikwete jana.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais na Issa
Michuzi-IKULU
No comments:
Post a Comment