“Wasipotandikwa mambo hayaendi, nilipokuwa mwalimu mkuu nilikuwa nawatandika kweli ndiyo maana shule yangu ilikuwa ikiongoza Mkoa wa Mbeya hivihivi hawaendi...”
( Mwananchi, Aprili 9, 2013)
- Je kauli hii ya mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo ndio inashinikiza kurudishwa kwa adhabu ya viboko mashuleni?
Je
kweli kuwa nidhamu miongoni mwa watoto wetu suluhisho lake ni viboko kama kauli
hii hapa chini inavyojieleza? “Mimi naunga mkono matumizi ya viboko kwa kuwa nidhamu
kwa wanafunzi imeshuka sana, ilimradi tu walimu wasitumie hii fursa kwa lengo
la kuwakomoa wanafunzi kwa kuwapiga bakora hata kwa makosa ya kipuuzi..”
Je kweli jamii ya vijana wetu na
matendo yote mabaya ni kweli umechangiwa na kuondolewa adhabu ya viboko?
“Utovu wa nidhamu, unaotokana na kutochapwa
bakora, sio tu kwamba unachangia matokeo mabaya tu lakini pia unawafanya
wanafunzi wajisikie huru zaidi na kuiona shule kama mahali pa kwenda kustarehe
na kupoteza muda! Matokeo yake wanafunzi hujiingiza katika matendo ya ajabu
kama ngono na uvutaji bangi, hivyo kujikuta wakipotea zaidi kimaadili pamoja na
kupata mimba za utotoni (teenage pregnancies) ambazo huwafanya wafukuzwe shule.”
Mkurugenzi
wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo Bisimba alisema
adhabu ya viboko haina maana katika kipindi hiki akisema wanafunzi wanapaswa
kupewa adhabu ambazo zinawafundisha kama zile za kufanya usafi na kazi
mbalimbali.
“Viboko havifundishi zaidi ya kumpatia mwanafunzi maumivu na kusababisha aichukie shule. Waelimishwe kwa kuelekezwa lakini wakiendelea kukiuka, wapewe adhabu za kufanya kazi mbalimbali.”
“Viboko havifundishi zaidi ya kumpatia mwanafunzi maumivu na kusababisha aichukie shule. Waelimishwe kwa kuelekezwa lakini wakiendelea kukiuka, wapewe adhabu za kufanya kazi mbalimbali.”
Rais
wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba alisema walimu hawapati
faida yoyote kuwachapa au kutowachapa viboko wanafunzi.
“Hawa viongozi kila kukicha wanazungumza mambo yasiyo na maana, badala ya kuzungumzia masilahi ya walimu wanazungumza kuhusu viboko, hatuelewi wakiamka kesho watasema nini,”
“Hawa viongozi kila kukicha wanazungumza mambo yasiyo na maana, badala ya kuzungumzia masilahi ya walimu wanazungumza kuhusu viboko, hatuelewi wakiamka kesho watasema nini,”
Maoni
ya ndugu Majjid Mjengwa kuhusiana na mjadala huu :
- “Tunarudi nyuma miaka 50 badala ya kwenda mbele. Kuna wengi kama mimi tusioamini, kuwa, kumchapa mwanafunzi bakora ni kumsaidia kujenga nidhamu na kujituma.”
- “Kinyume chake, kama ni nidhamu, utamjengea nidhamu ya woga na kufanya yale ambayo anadhani unataka ayafanye na si kuwa ayafanye kwa faida yake na jamii hapo baadae.”
- “Viboko vinamfanya mwanafunzi asijiamini na hata akose uwezo wa kudadisi. Bado nakumbuka, kuwa nikiwa Darasa la Tano ilinitokea nikachapwa bakora darasani kwa kosa la ‘ kumdadisi sana mwalimu’. Mimi nilitaka kupata ufahamu zaidi lakini mwalimu aliniona nimekosa nidhamu.”
- “Wanafunzi kukosa nidhamu na kutokufanya vizuri kwenye masomo inachangiwa na mambo mengi. Tuanze kuyaangalia hayo kwanza kabla hatujawahamasisha walimu wakate bakora za miti ya mipera kuwachapa watoto wetu.”
Tukiangalia kwa undani
kabisa swala la kushuka kwa nidhamu ya watoto wetu na kuendelea kufanya vibaya
katika matoke ya mitihani ya kitaifa, kama nilivyowahi andika huko nyuma serikali
kupitia kwa waziri mwenye dhamana na wizara yao nafikiri wameacha kutatua
tatizo na kukimbilia kutoa hitimisho la tatizo bila hata kuligundua tatizo ni
nini;
Mimi inanipa ugumu uwezo
wa kiutendaji wa viongozi hawa ambao wamepewa dhamana na serikali ili waweze kutuletea
falfasa muhimu ya kuboresha elimu ya vijana wetu ambao ni muhimili imara wa
Taifa letu; tukiwa wakweli tutaona kuwa Wizara imekosa mwelekeo ya kuleta
mabadiliko katika elimu nchini. Naungana
na mwandishi aliyewahi sema kuwa “ Napenda
kupingana na wewe maana suala la kutoa adhabu kama suluhisho la utovu wa
nidhamu au kutozingatia masomo limepitwa na wakati. Jamii yoyote amabayo walezi
wake wamebobea katika kuelekeza watoto kupima athari za matendo yao kabla ya
kutenda an kufundisha maadili ya akili kuliko maadili ya kuachana na ngono:
mfano kufundisha matumizi bora ya muda, matumizi ya pesa, umuhimu wa kufanya
mambo kwa tija, umuhimu wa kusikiliza sauti za nafsi zao na wenzao pamoja na
Mungu itaweza kufanikiwa sana bila viboko.”
Makosa mengi wanayofanya watoto yanatokana na makosa ya walimu au walezi wao nukweli ambao haufichiki kwani sisi wazazi vilevile tunamchango mkubwa sana katika elimuorya watoto wetu.Lakini Kwa hali tuliyofikia viboko siyo suluhisho. Wazazi wana msaada mkubwa katika kusaidia ufaulu wa watoto wetu.
Makosa mengi wanayofanya watoto yanatokana na makosa ya walimu au walezi wao nukweli ambao haufichiki kwani sisi wazazi vilevile tunamchango mkubwa sana katika elimuorya watoto wetu.Lakini Kwa hali tuliyofikia viboko siyo suluhisho. Wazazi wana msaada mkubwa katika kusaidia ufaulu wa watoto wetu.
Nafikiri Tatizo la Naibu Waziri bado anamawazo ya miaka ya 1950 kuishi kwa mazoea dhana ambayo kwa kweli imepitwa na wakati; “Je, ni kweli umefanya hata utafiti kidogo kuona kuwa kushuka kwa nidhamu, ufaulu wa wanafunzi unasababishwa na kutochapwa viboko?
Kama Askofu
Muhogolo aliowahi sema “kwa namna moja au nyingine, kwamba adhabu ya viboko ni
adui wa taaluma ya elimu. Kama walimu wataendelea na hali ya kuwachapa viboko
wanafunzi, ni wazi watakuwa ni maadui wa wanafunzi. Tunafahamu kwamba mwalimu
ndiye wa kwanza kumfungulia milango ya ufahamu mwanafunzi, hivyo ni vema
akamwekea mazingira mazuri ya kumfundisha na kumuonya pindi anapofanya kosa na
si kumchapa viboko, kwani viboko si fundisho bali ni kumfanya mwanafunzi awe
jeuri”.
Je ufaulu mdogo wa wanafunzi nafikiri
kiini chake kumesababishwa kwa kiasi kikua na:
- mishahara midogo,
- makazi duni na mazingira magumu ya kazi
- mchango mdogo wa wazazi katika maisha ya shule ya vijana wetu
- mitaala ambayo imekosa mwelekeo na vifaa vya kiada
( vitabu, madarasa mazuri, maabara
mazuri, maktaba etc)
kama Naibu Waziri anafiki viboko ni suluhisho la matatizo je yale yanayoendelea
leo bungeni ambako wabunge wanaochangia hoja baada ya kutoa hoja wanatoa
matamshi yaliyojaa matusi nafikiri tungeanzia huko kutoa adhabu ya viboko;
kwani wao pia hawalisaidia taifa pamoja na kutumia pesa nyingi za walala hoi.
kama mwandishi mmoja alivyowahi sema:
kama mwandishi mmoja alivyowahi sema:
“Kama viboko ni
suluhisho, basi tuwachape wote sio watoto/wanafunzi tu. Tuwachape Mawaziri
wanaoshindwa kutimiza majukumu yao, tuwachape Wabunge wanaosinzia Bungeni,
tuwachape mafisadi, tuwachape wafanyakazi wanaochelewa kazini, tuwachape
maaskari wanaokula rushwa, tuwachape akina mama wanaoshindwa kunyonyesha watoto
wao, tuwachape wanaume/wanawake wanaotoka nje ya ndoa.tumchape kila mtu.”
Serikali kuendelea kufumbia matatizo
ya msingi ambayo yanaikabili wizara ya Elimu na kukimbilia kushinikiza adhabu
ya viboko irudi mashuleni nafikiri itakuwa inapingana na nia yake njema
ya kuanzisha kwa shule hapa nchini;
Je kurudishwa kwa adhabu ya viboko
ndio vision ya kuelekea elimu na malezi Bora? Kwa nini uanzishe shule nyingi za
sekondari wakati huna uwezo wa kuwasaidia vijana wetu kutimiza ndoto zao za
elimu ya juu wakati huna uwezo wa kuziendesha
kwa ufanisi hazina walimu wala vifaa?
Wizara inajua kuwa mwanafunzi
anayepata daraja la tatu au la pili katika shule za aina hii anao uwezo mkubwa
wa kujifunza kuliko wanafunzi wengi wanaosoma katika shule za ambazo
zinafaulisha vizuri ambazo ni bora kwa kila kitu?
Baada ya kukimbilia kwenye adhabu ya viboko je wizara
imeshaangalia uhusiano wa wanafunzi kufanya vibaya na wanafunzi kuchukia shule
kutokana na sababu za kitaaluma na kimazingira, shule zetu nyingi zina kosa
vifaa muhimu ya kufundishia na kujifunza shule kama inakosa vitabu vya kiaada
vifaa vya mahabara je unategeme kuwa kutakuwa na ubora wa elimu hapo? Mimi
nasema hapana na tusitegemee miujiza kutoka katika shule zetu za serikali
ambazo watoto wetu wengi ndiko wanakosoma. Viboko Mheshimiwa Naibu Waziri sio
suluhisho ni kuongeza tatizo juu ya Tatizo.
Pale
tutakapo amua kuacha maneno na kuanza kutekeleza maneno yetu kwa vitendo ndipo
tutegemee kuona: watoto wetu wakifikia malengo yao ya elimu kupitia elimu bora
na kufanikiwa kuondoa umasikini kwa kiwango kikubwa sana.
Lazima tukubali kuwa kuwa na walimu bora ambao wanavifaa
vinavyotakiwa kwa ajili ya elimu bora huleta tofauti kubwa sana kwa wanafunzi
wetu na sifa kubwa kwa taifa letu; taifa lisipokuwa tayari kubadilika
tutaendelea kunyosheana vidole kuhusu matokeo ya wanafunzi wetu kila mwaka kama
jedwali la hapo chini linavyoonyesha, kwa ujumla ni aibu kubwa kuona watoto
wetu wanafeli kwa kiasi kikubwa namna hii, na kubaliana na wengi ambao
wamediriki kusema kuwa hili ni janga la kitaifa ni vyema kama tulitafutia
ufumbuzi wa haraka; washauri wa serika li yetu mnashauri nini?
Hii
ni vita ya mafahari wawili na wanaoumia kwa kiasi kukubwa ni wananchi ambao
hawana kosa pamoja na mchango mkubwa mkubwa wa kodi zao wameishaia kupoteza
maisha na kwa mvutano unaoendelea;
“Tatizo la wakati wetu tabaka la masilahi
bora linaongezeka na kusababisha migomo miongoni mwa jamii; kwa
viongozi wetu na wanansiasa wetu nafikiri ni wakati mwafaka wa kuitafakari hali
hii na kuijengea mikakati ya kuhakikisha kuwa migomo inatokomea kabisa ndani ya
jamii zetu; Hakuna lisikowezekana; Pamoja tukisima tutaendelea kwa faida ya
wote”
pamoja na kauli ya Mheshimiwa Raisi kuwa serikali haiwezi kuyatekeleza madai ya walimu; lakini bado serikali yetu inanafasi ya kukaa na walimu na kuangalia namna mbadala ambayo inaweza kuwamotisha walimu katika kazi yao hii ngumu. lakini kama serikali yetu itatumia kauli za vitisho na za kukatisha tamaa, hata walimu wakirudi kufundisha basi tutegemee matokeo mabaya katika mitiani inayokuja. Mungu liepushe Taifa na mporomoka wa elimu bora kwa vijana wa Taifa hili.
pamoja na kauli ya Mheshimiwa Raisi kuwa serikali haiwezi kuyatekeleza madai ya walimu; lakini bado serikali yetu inanafasi ya kukaa na walimu na kuangalia namna mbadala ambayo inaweza kuwamotisha walimu katika kazi yao hii ngumu. lakini kama serikali yetu itatumia kauli za vitisho na za kukatisha tamaa, hata walimu wakirudi kufundisha basi tutegemee matokeo mabaya katika mitiani inayokuja. Mungu liepushe Taifa na mporomoka wa elimu bora kwa vijana wa Taifa hili.
Napenda kumaliza kwa nukuu hii “Kwa nini
viboko viwe kwa ajili ya wanafunzi/na watoto pekee na sio wengine wanaofeli
kutimiza majukumu yao? Tumchapee kila mtu halafu tusiwe na miudombinu
mashuleni, vijana wetu watashinda kwa miujiza ya kiboko nakwambia”
Nafikiri wakati wakubadilisha fikra
za utendaji wetu umefika ili vijana wetu waweze kupata au kufikia malengo yao
ya maisha.
Tufikiri kwanza kabla ya kukurupuka
kutoa uamuzi
No comments:
Post a Comment