Uchumi mnao, lakini mmeukalia!" – Julius Nyerere.
Bunge la Bajeti linaendelea kule Dodoma. Kwa mengine tunayoyaona yakitokea ndani ya Bunge wakati mwingine unawaza na kujiuliza; hivi ni Bunge la Wanasiasa au Bunge la Wananchi?
Bunge la Bajeti linaendelea kule Dodoma. Kwa mengine tunayoyaona yakitokea ndani ya Bunge wakati mwingine unawaza na kujiuliza; hivi ni Bunge la Wanasiasa au Bunge la Wananchi?
Maana, waliomo ndani bungeni wametumwa
na wananchi. Inakuwaje basi, wanatumia muda mwingi pia kujadili mambo
yasiyo na masilahi kwa wananchi? Watanzania wengi wana hali mbaya za
kiuchumi. Wanataka kupiga hatua za maendeleo ya kiuchumi. Wanahitaji
sana kuona yanazungumzwa masuala ya msingi kwa maendeleo yao.
Pia kauli ya ' Uchumi mnao,
mmeukalia!' Inanikumbusha utotoni pia. Nilipata kusikia redioni kauli
hii ya Mwalimu . Tulipokuwa shuleni tulifundishwa na hata kuimba kwamba
ili tuendelea tunahitaji vitu vinne; Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi
bora.
Ni dhahiri kwamba, watu tunao, tena
wengi sana. Ardhi tunayo, tena kubwa sana. Hivyo viwili nilivyovitaja
ndiyo mtaji mkubwa tulio nao. Huo ndiyo utajiri wa maskini, lakini
hauonekani. Huenda kinachokosekana ni Siasa safi na Uongozi bora katika
kuuendeleza mtaji tulio nao. Kuna Mtanzania mwenzetu aliyebainisha kuwa
mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe. Labda nyongeza hapa ni kuwa;
mtaji wa nchi ni watu wake wenyewe.
Nchi kupitia vyanzo vyake vya mapato,
siasa safi na uongozi bora na zaidi utawala bora, vina wajibu wa kujenga
misingi ya jamii bora. Jamii bora ni ishara ya kuwepo kwa taifa bora.
Taifa bora ni taifa lenye nguvu. Hilo litafanikiwa kama dola itaweka
kipaumbele katika kuwaendeleza watu wake. Muhimu na la kwanza kabisa ni
kuwekeza katika elimu. Huko ni kuuendeleza mtaji muhimu kwa maendeleo ya
taifa.
Angalia hapa, wasichana hawa wenye
kupata mimba na kufukuzwa shule ndiyo sehemu ya makabwela tunaotaka
kuwawezesha. Hawa ndiyo wazazi wa kesho. Kuwapa nafasi ya pili katika
maisha yao angalau tu wamalizie elimu yao ya shule ya msingi ni moja ya
njia za kuwawezesha wanawake hawa ili nao waje kuwa walezi bora wa
watoto wao ambao pia ni taifa la kesho.
Hebu tujikite zaidi kwenye elimu. Ni
ukweli, kuwa Serikali kwa kupitia mpango wake wa MMEM (Mpango wa
Maendeleo ya Elimu ya Msingi) ilifanikiwa katika ujenzi wa madarasa
mapya katika sehemu mbalimbali. Lengo pia ni kuwashirikisha wananchi
katika masuala ya elimu.
Hata hivyo, kuna ugumu mkubwa katika
hili, kwani wengi wa wananchi ambao Serikali inataka kuwashirikisha, nao
pia wana kiwango kidogo kabisa cha elimu ikiwamo ujinga wa kutokujua
kusoma, kuandika na kuhesabu.
Ili mipango ya Serikali iwe na
mafakinio ya muda mrefu, kunahitajika pia kuwepo na mpango wa kuimarisha
Elimu ya Watu Wazima. Wazo hapa ni kuwepo kwa Mpango wa Kuendeleza
Elimu ya Watu wa Wazima (Mkewawa).
Visheni ya Serikali ya kuondoa
umaskini ifikapo mwaka 2025 haiwezi kufanikiwa endapo hakutakuwepo na
visheni ya kuondoa ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika sambamba na
kampeni ya kuondoa umaskini.
Kwa vile zaidi ya asilimia 80 ya watu
wa nchi hii wanaishi vijijini na kwamba kilimo ndiyo uti wa mgongo wa
uchumi wetu, kamwe hatuwezi kupiga hatua za haraka za maendeleo, endapo
idadi kubwa ya watu wetu na hususan waishio vijijini watazidi kuzama
kwenye bahari ya ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika.
Kuufuta ujinga wa kutokujua kusoma na
kuandika miongoni mwa watu wetu iwe ndiyo hatua ya kwanza katika kampeni
za kuondoa umaskini. Hapa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima(TEWW) kupitia
Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi ingeweza kushiriki kikamilifu katika
Mpango wa Kuendeleza Elimu ya Watu Wazima kwa kutoa mchango mkubwa
katika kuendesha kampeni za kufuta ujinga na kuwandeleza wananchi
kielimu katika hatua ya utu uzima
source: Mjengwa Blog
No comments:
Post a Comment