Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
(Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi (kulia) akizungumza na wabunge wa
Chadema baada ya kikao cha kunge kualishwa jana mchana. Picha na Edwin
Mjwahuzi
Na
Boniface Meena, Mwananchi
Dodoma.Wabunge watano wa Chadema jana walitimuliwa
bungeni na kuamriwa kukaa nje ya Bunge kwa siku tano kutokana na vurugu
zilizotokea jana usiku.
Wabunge hao ni Lissu, Hezekiah Wenje
(Nyamagana), Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) Godbless
Lema (Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).
Chanzo za kufukuzwa kwao ni kuwazuia
askari wa Bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu
Spika, Job Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya Mbunge wa Iramba Mashariki,
Mwigulu Nchemba.
Kutokana na tafrani hiyo, Nchemba
hakuweza kuhitimisha hotuba yake hivyo Ndugai alilazimika kukatisha mkutano wa
Bunge.Hata hivyo wakati akiahirisha mkutano huo, tayari wabunge hao walikuwa
wameshatolewa nje baada ya askari kuongezwa.
Mapema Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM),
Peter Serukamba alitoa tusi zito la nguoni wakati wa hotuba ya Msemaji Mkuu wa
Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, licha ya
Spika wa Bunge, Anne Makinda kupiga mkwara wa kuwashughulikia wabunge
watakaorusha matusi.
Mbali na tukio hilo Lema naye alichafua
hali ya hewa baada ya kuwatuhumu viongozi wa CCM akiwamo Rais Jakaya Kikwete
kwa udini, madai ambayo Bunge limempa siku saba kuyathibitisha.
Lema aliituhumu CCM na Serikali yake
chini ya Rais Kikwete kwa kushindwa kutatua mgogoro wa kidini na badala yake
kuwa kama analikwepa tatizo. Alionya kuwa Taifa linapasuka kwa migogoro
kutokana na viongozi wa Serikali kushindwa kulishughulikia.
Kauli iliwanyanyua vitini Waziri wa
Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Uratibu na Sera), William Lukuvi na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Lukuvi na Jaji Werema walisimama wakidai kuwa Lema alikuwa amemdhihaki Rais Kikwete kwa kauli zake za kumhusisha na masuala ya udini.
Lukuvi na Jaji Werema walisimama wakidai kuwa Lema alikuwa amemdhihaki Rais Kikwete kwa kauli zake za kumhusisha na masuala ya udini.
Hata hivyo, Mnadhimu Mkuu wa Upinzani,
Lissu alisimama kumtetea Lema akidai hakuwa amemdhihaki Rais bali alikuwa
amemkosoa kitu ambacho kanuni za Bunge zinaruhusu.
Lema aliruhusiwa kuendelea na hoja yake
na ndipo akamtolea mfano Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu),
Steven Wassira wakati alipokwenda Mwanza kutatua mgogoro baina ya Wakristo na
Waislamu kuhusu suala la kuchinja.
“Wassira akifahamu yeye ndiye, Waziri
alikwenda Mwanza na kuwaacha viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu watatue
wenyewe suala la kuchinja. Sasa alitaka diwani atatue mgogoro ule?”
Baada ya kumaliza kuchangia, Naibu
Spika alitangaza kuwa Lema anatakiwa kuwasilisha katika muda wa siku saba
uthibitisho kuwa Rais anahusika na tatizo la udini.
Serukamba
Serukamba alipewa nafasi ya kutoa taarifa wakati wabunge walipokuwa wakilumbana juu ya uhalali wa Msemaji wa Upinzani, Profesa Kulikoyela Kahigi kuzungumzia bungeni masuala yaliyoko mahakamani na shughuli za Idara ya Usalama wa Taifa.
Serukamba alipewa nafasi ya kutoa taarifa wakati wabunge walipokuwa wakilumbana juu ya uhalali wa Msemaji wa Upinzani, Profesa Kulikoyela Kahigi kuzungumzia bungeni masuala yaliyoko mahakamani na shughuli za Idara ya Usalama wa Taifa.
Wakati
akijiandaa kusoma vifungu vya kukatiza hotuba ya Profesa Kahigi, alitukana tusi
zito la nguoni kwa lugha ya kimombo ambalo kwa sababu za kimaadili hatukuweza
kuliandika, kisha akaendelea kuzungumza huku baadhi ya wabunge wakipigwa
butwaa.
Hata
hivyo, Naibu Spika, Job Ndugai aliyekuwa akiongoza shughuli za Bunge wakati
huo, hakutoa karipio lolote huku akimruhusu Serukamba kuendelea kwa muda kabla
ya kumkatiza na kumruhusu Mbunge wa Simanjiaro (CCM), Christopher Ole Sendeka
kuzungumza.
Ubishi ulivyoanza
Muda mfupi kabla ya Profesa Kahigi kuanza kusoma hotuba yake, Serukamba alisimama na kuomba mwongozo wa Spika kupitia Kanuni ya 68(1) akitaka isisomwe kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa nne kwa kuwa unaingilia uhuru wa Mahakama... “Ni juzi tu Akoonay (Mustapha, Mbunge wa Mbulu - Chadema), alitukumbusha kwamba mambo hayo ni ‘prejudice’ kwa Mahakama kwa hiyo ukiruhusu hilo Naibu Spika itakuwa ni ajabu.”
Muda mfupi kabla ya Profesa Kahigi kuanza kusoma hotuba yake, Serukamba alisimama na kuomba mwongozo wa Spika kupitia Kanuni ya 68(1) akitaka isisomwe kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa nne kwa kuwa unaingilia uhuru wa Mahakama... “Ni juzi tu Akoonay (Mustapha, Mbunge wa Mbulu - Chadema), alitukumbusha kwamba mambo hayo ni ‘prejudice’ kwa Mahakama kwa hiyo ukiruhusu hilo Naibu Spika itakuwa ni ajabu.”
Kabla
Naibu Spika hajatoa mwongozo wake, alimtaka Profesa Kahigi kuzungumza kama
anakubaliana na Serukamba, lakini Profesa Kahigi alisema anaomba kuendelea
kusoma hotuba yake kama ilivyo.
Baadaye
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika aliomba kumpa taarifa Serukamba kwamba
katika kurasa alizozitaja hakuna jambo lolote lililopo mahakamani hivyo
aangalie vizuri.
“Mheshimiwa
Naibu Spika napenda kumpa taarifa mtoa taarifa kwamba hakuna lolote lililopo
mahakamani, ukurasa wa kwanza unazungumzia Idara ya Usalama wa Taifa, haipo
mahakamani, ukurasa wa pili umemtaja Dk Stephen Ulimboka, halipo mahakamani
hivyo hakuna lolote lililopo mahakamani,” alisema.
Baada
ya hapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William
Lukuvi alisimama na kueleza kuwa aliyoyasema Serukamba ni kwamba hotuba hiyo
inafanya kesi iliyopo mahakamani kuwa ya kisiasa akisema... “Kifungu cha 16 cha
Sheria ya Usalama wa Taifa hakiruhusu watumishi wa Usalama wa Taifa kutajwa
humu ndani wala kuchapishwa popote.”
Naibu
Spika alisimama na kusema jambo hilo limeshajitokeza ndani ya Bunge na Akoonay
alishawakumbusha kuwa ni kuingilia Mahakama.
“Jambo
hili lilishaleta kasheshe humu ndani na ruling (uamuzi) ya hili ilishatolewa na
Spika, ‘ruling’ yangu ni kwamba kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa nne, mambo
ya Dk Ulimboka, Usalama wa Taifa na Lwakatare.........,” aliishia hapo Ndugai
na kuwaruhusu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki na Ole Sendeka
kuzungumza.
Mdee
alisema ukurasa wa kwanza mpaka wa tatu wa hotuba hiyo hakuna sehemu jina la
Lwakatare lilipotajwa na kwamba ukurasa wa nne uliotaja jina la Lwakatare
hauzungumzii mwenendo wa kesi... “Hoja anazoleta Lukuvi atusomee hiyo Sheria ya
Usalama na atuelezee na alinganishe na kilichopo hapa.”
Mdee
aliungwa mkono na Lissu aliyesema kuwa sheria anayozungumzia Lukuvi ipo lakini
haikatazi kutajwa majina ya wanausalama ndani ya Bunge... “Ninayo hiyo sheria
hapa ya mwaka 1996, haya maneno kwamba Sheria ya Usalama inakataza masuala ya
Usalama wa Taifa kutajwa ni uchochezi. Hicho kinachoelezwa kukataza
‘disclosure’ (kuwataja) ni huko nje na si humu ndani.”
Lissu
alisema sheria hiyo inakataza kuchapishwa majina hayo nje ya Bunge na si
vinginevyo.
Kairuki
alipingana na Lissu akieleza kuwa amepotosha kwa kuwa sheria hiyo ya Usalama wa
Taifa hairuhusu kuwataja watumishi wake bila kuomba ruhusa kwa waziri.
“Lissu
anapotosha kwa kuwa hairuhusiwi mtu yeyote kuchapisha jina la mtumishi wa
Usalama wa Taifa bila kuomba ruhusa kwa waziri,” alisema Kairuki.Ndipo Naibu
Spika alipompa tena nafasi Serukamba na alipoanza tu kuchangia kuliibuka maneno
ya chinichini ambayo yalionekana kumkera ndipo alipotoa neno hilo zito.
Baadaye
Ndugai alisema kwa kuwa hilo suala ni la kikanuni, anaiagiza Kamati ya Kanuni
ikutane ili tujadili suala hilo.
Katika
hotuba hiyo ambayo awali, waandishi walipata nakala yake, Profesa Kahigi
alikuwa ameandika mambo mbalimbali yanayohusu kutekwa na kuteswa kwa Kiongozi
wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka na masuala mengine
yanayohusiana na kesi ya ugaidi inayomkabili Mkurugenzi wa Usalama wa Chadema,
Wilfred Lwakatare.
Source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment