Na
Waandishi Wetu, Mwananchi
Dar/Dodoma. Mvutano kuhusiana na mchakato wa kupata Katiba Mpya unaozigonganisha Serikali na Chadema ulizidi kupamba moto bungeni jana wakati wa mjadala wa kuhitimisha hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Dar/Dodoma. Mvutano kuhusiana na mchakato wa kupata Katiba Mpya unaozigonganisha Serikali na Chadema ulizidi kupamba moto bungeni jana wakati wa mjadala wa kuhitimisha hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana
alitumia muda wake karibu wote wa saa moja kujibu maoni na kumshambulia
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliyoyatoa kuhusu
hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hoja za Mbowe zilizoonekana kumsumbua
Pinda ni malalamiko dhidi ya Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba, Tume ya Taifa ya
Uchaguzi na kauli yake kwamba serikalini hakuna weledi wa kuwezesha kupanga
mipango ya maendeleo.
Hata hivyo, baada ya kuhitimisha hotuba
hiyo, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alisimama kuomba mwongozo wa Spika chini ya
kanuni ya 68 (7) akidai kuwa Pinda alikuwa ametoa kauli ya uongo kuwa Chadema
haikuwasilisha mapendekezo yake juu ya muundo wa Mabaraza ya Katiba, badala
yake walilalamika tu kwenye mkutano wa hadhara.
Akizungumzia, Pinda alieleza kumshangaa
Mbowe kwa kudai kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba haina weledi wakati kuna
maprofesa na kati ya hao ni Profesa Mwesiga Baregu wa Chadema.
“Hivi kweli hawa wazee na maprofesa ni
mambumbumbu kweli au ni kauli ambayo hakuipangilia. Haiwezekani kwa mjumuiko wa
wazee wote waliomo mle ndani."
“Tuwatendee haki Watanzania na
tusiwakatishe tamaa wazee wetu ambao wamezunguka nchi nzima na kufanya kazi
kubwa, kama haya ndiyo Mbowe ametumwa basi nadhani aliteleza.”
Pinda alisema kama kuna tatizo kwenye
mchakato ni kutokana na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iliyopitishwa na Bunge.
Wakati anazungumzia suala hilo
ilisikika sauti kuwa wakati sheria hiyo inapitishwa Chadema walitoka bungeni, na
Pinda alirudia, “Nasikia kuwa mlitoka bungeni.”
Pinda alisema kutakuwa na Bunge la
Katiba na wabunge wote ni wajumbe, pia kwa Zanzibar kuna Baraza la Wawakilishi,
hivyo Mbowe kuanza kutoa maoni hayo inaonyesha wana hofu.
“Kama Chadema wana hofu basi ni jambo
lingine, nilipoisoma `speech’ (hotuba) ya Mbowe mawazo yake yanaonyesha anawaza
uchaguzi wa 2015 na si kitu kingine,” alisema Pinda na kupigiwa makofi na
wabunge wa CCM.
Alisema Mbowe alimtisha zaidi pale
aliposema kuwa wataitisha maandamano nchi nzima kupinga suala hilo,
“Wananchi
msiambiwe mwandamane, kama mnapinga basi mpinge wenyewe, kwani akili za
kuambiwa inabidi uchanganye na zako,” alisema Pinda na kuongeza:
“Tume
haiwezi kufanya kazi kisiri na tume haitoi taarifa kwa Rais kama ilivyodaiwa na
Mbowe, bali inatoa taarifa kwa umma wote. Alichosema Rais Jakaya Kikwete ni
ratiba ya tume ambayo imo kwenye sheria na ilikuwa imeshatolewa na Mwenyekiti
wa Tume Jaji Joseph Warioba kwenye vyombo vya habari.”
Kuhusu
suala la Mabaraza ya Katiba kukaa ki-CCM, alisema kama ni hivyo basi Bunge
ndiyo lililofanya makosa kwa kuwa ndiyo lililopitisha kuwa wajumbe watapitishwa
na Mkutano wa Maendeleo wa Kata (WADC).
“Bado
tuna mwanya mkubwa sana huko mbele wa kurekebisha mambo haya na kufika mahala
pazuri,” alisema Pinda.
Alisema
kinachowatia hofu Chadema ni kuwa mikutano ya WADC ina wenyeviti wengi wa CCM,
jambo alilosema ni zuri kwa kuwa ndiyo wameaminiwa na wananchi.
Pinda
alisema kuwa hata hiyo Tume ya Katiba ilipotaka wadau watoe mapendekezo ya
mfumo wa mabaraza hayo Chadema haikuwasilisha lakini baada ya muundo uliopo
kupangwa ndipo chama hicho kilitoa maoni kwenye mkutano wa hadhara.
Kauli
hiyo ndiyo ilimfanya Mnyika aombe mwongozo wa Spika akisema Pinda alitoa kauli
ya uongo kwa kuwa chama hicho kiliwasilisha mapendekezo yake lakini
hayakuzingatiwa.Kabla ya kuanza kutoa mashambulizi kwa Mbowe, Pinda alianza
kutuma ujumbe kwa wabunge wawili wa CCM waliotangaza wazi kuwa wasingeunga
mkono bajeti yake.
“Nawashukuru
sana kwa michango yenu Lugola (Kangi Lugola) na Filikunjombe (Deo) kwa kukataa
kuunga mkono hoja, tutafanyia kazi maoni yenu, lakini nimeshindwa kumwelewa
Filikunjombe aliposema tuchukue hoja za wapinzani tuzifanyie kazi,” alisema
Pinda.
Kadhalika
Waziri Mkuu alisema hoja ya Chadema ya kutaka Waziri wa Elimu na Mafunzo, Dk
Shukuru Kawambwa kuwajibika halina tatizo ila ni baada ya tume aliyoiunda kujua
tatizo la wanafunzi kufeli mitihani.
“Endapo
ikibainika kuna uzembe ambao ulijitokeza suala la Kawambwa kuwajibika hilo
halina shida hivyo tusubiri tume itakuja na taarifa gani,” aliongeza Pinda.
Maoni ya Mbowe
Wakati
Waziri Mkuu akisema hayo, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman
Mbowe alisema mchakato huo wa kuwapata wajumbe wa Mabaraza ya Katiba hauko sawa
na watajitoa kama walivyokwisha kusema.
“Utaratibu
wa mabaraza ya katiba haukuzingatiwa,tunataka kulifumbia macho hili tunataka
kujenga ufa wa wananchi na huu mpango ukiendelea hivi tutawaachia ninyi
muendelee.
“Kama
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba isipoletwa Bungeni tukiomba rejeo ya mambo
mawili ya sheria hiyo hatutakuwa na uhalali wa kuendelea kushiriki mchakato huu
kwani kinyume cha utawala bora na mabaraza haya hatuyakubali na tutajitoa
mwishoni mwa mwezi huu”.
Alisema
kupatikana kwa Katiba Mpya na iliyoshirikisha wananchi itasaidia kutibu
majeraha ya wananchi waliyokwisha yapata kutokana na ubovu wa Katiba iliyopo.
Mawaziri 10 tu wachapakazi
Mbunge
wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM) amesema Tanzania inashindwa kupiga hatua
kimaendeleo kwa kuwa asilimia kubwa ya mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne
hawafanyi kazi.
Akizungumza
wakati akichangia Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni mjini Dodoma
jana, Filikunjombe alisema kati ya mawaziri 55 wa Serikali ya Awamu ya Nne,
wanaofanya kazi zao kikamilifu hawazidi 10.
Filikunjombe
alitishia kuwa hahofii chochote na ana uwezo wa kuwataja mawaziri wachapakazi
na wale ambao hawafanyi kazi kwa kuzingatia viapo na maadili ya uongozi.
Alitoa
mfano huo kwa maelezo kuwa hoja mbalimbali zinazotolewa na wabunge na wananchi
kuhusu wizara husika, nyingi zimekuwa hazifanyiwi kazi na badala yake ahadi na
uundwaji wa tume ambazo ripoti zake zinakaliwa.
“Viongozi
wa Serikali wanafanya mambo wanavyojua wao, mawaziri wakati wanaapishwa
wakiahidi kuwa watailinda Katiba ya nchi, badala yake wanalindana wao wenyewe
na badala ya Katiba,” alisema Filikunjombe.Imeandikwa na Reginald Miruko,
Boniface Meena, Ibrahim Yamola na Fidelis Butahe.
“Kiwango
cha elimu kinazidi kushuka na tume zilishaundwa miaka iliyopita kuchunguza
suala hilo na kuja na majibu mazuri, lakini badala ya kufanyia kazi mapendekezo
hayo sisi tunaunda tume nyingine,” alilalamika Filikunjombe.
Alisema
kuwa mawaziri hao kila wanapoelezwa mambo mbalimbali wengi husema kuwa mchakato
unaendelea, tutafuatilia kwa kina suala hilo, kwamba majibu hayo hayajibu hoja
za msingi zinazowasilishwa.
Mbali
na kutounga mkono hoja za Waziri Mkuu wakati akiwasilisha bajeti yake, alisema
Serikali imekuwa ikiunda tume kwa kigezo cha kuzima hoja.
“Tume
zikishaundwa ujue kuwa mambo ndiyo yamekwisha, tufike mahali sisi kama viongozi
tubadilike jamani, tunaelezwa kuwa elimu ya msingi ni bure, sasa mbona wazazi
wanatoa fedha nyingi kuchangia michango.”
Alisisitiza
kuwa huo ndiyo udhaifu mkubwa kwa baadhi ya viongozi, na kuongeza kuwa hata
hoja zinazotolewa na vyama vya upinzani kuhusu utendaji mbovu wa viongozi wa
Serikali nyingine zina ukweli ndani yake.
“Tusipinge
kila hoja ya wapinzani bali tuzifanyie kazi, nasema hivi kwa sababu hata kobe
ukimkuta juu ya mti ujue kapandishwa,” alionya Filikunjombe.
Aliwataka
watendaji wa Serikali kutimiza malengo na wajibu na kwamba hiyo ndiyo njia
nzuri ya kuwanyamazisha wapinzani.
Source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment