Siku chache tu baada ya taifa
kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu nchini, Edward
Moringe Sokoine aliyekuwa mwenyekiti wa Uvccm mkoani Arusha, James Ole
Milya ameibuka na kutamka kwamba jamii ya kimasai imetupwa na kubaki
kama yatima ndani ya nchi yao.
Ole Milya, alitoa kauli hiyo juzi
wakati akizuru kaburi la hayati Sokoine ambapo akiongea na waandishi wa
habari alitamka kwamba serikali haimuenzi kiongozi huyo kwa vitendo na
badala yake imekuwa ikipora haki za wafugaji kwa kumega ardhi yao kila
kukicha.
Alisema kuwa tangu kufariki kwa
Sokoine ambaye alikuwa msatari wa mbele kupigania haki za makabila yote
nchini lakini kwa hali ya sasa jamii ya kimasai imetupwa na vijana wake
wamebaki wazururaji na walinzi katika nchi yao.
“Jamii ya kimasai inamkumbuka Sokoine
kwa masikitiko makubwa sana kwani wamebaki wazururaji na walinzi katika
nchi yao”. Alisema kwa huzuni
Hata hivyo,Ole Milya ambaye kwa sasa
yuko Chadema alisema kuwa marehemu Sokoine alikuwa ni kiongozi wa mfano
kwa kuwa alitoa ushirikiano katika maeneo mbalimbali nchini, lakini cha
ajabu serikali imeshindwa kufuata nyendo zake.
Alisema kuwa serikali imeyasahau yote
mazuri aliyokuwa akiyafanya wakati wa uhai wake huku akisisitiza kuwa
kwa hali ya sasa keki na taifa inaliwa na watu wachache badala ya
wananchi wote.
Ole Milya alisisitiza kuwa yeye
anatoka katika jamii ya wafugaji wa kimasai na isingekuwa jitihada za
wafadhili wachache ambao ni wazungu kumpeleka shule leo angekuwa mlinzi
katika nyumba za baadhi ya watanzania.
Hata hivyo,alisema kuwa tangu kufariki
kwa Sokoine ardhi ya jamii ya kimasai imekuwa ikimegwa siku hadi siku
na serikali tofauti na maeneo mengine hapa nchini.
Alisema kuwa wachache kama yeye
wataendelea kumuenzi Sokoine kwa kusema ukweli ndani ya nchi yao bila
kujali vitisho vya kuuwawa au kuteswa.
“Nahaidi kuishi kama Sokoine hata kama
nikitolewa vitisho vya kuuwawa niko tayari kusema ukweli bila kujali
kupingwa wala kupigwa”alisema Ole Milya,
Chanzo: Fullshangweblog.com
No comments:
Post a Comment