Gaudence
Mwaikimba na Mcha Khamisi wakipongezana baada ya Azam kupata bao la tatu katika
mechi kati yake na Coastal Union leo. Azam ilishinda mabao 4-1. (Picha kwa
hisani ya Bin Zubeiry).
KOCHA John Stewart Hall leo amerejea Azam kwa zali baada ya kuiongoza timu hiyo kuibugiza Coastal Union mabao 4-1 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Stewart amerejeshwa Azam baada ya kutimuliwa kwa Kocha Boris Bunjak, kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo katika mechi za ligi kuu ya Tanzania Bara.
Ushindi huo uliiwezesha Azam kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 21, nyuma ya Simba na Yanga, zinazoongoza kwa kuwa na pointi 23 kila moja, lakini zikitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Mechi hiyo ilitawaliwa zaidi na Azam, ambayo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 3-0, yaliyofungwa na Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche na Mcha Khamisi.
Bao la nne la Azam lilitokana na makosa ya beki Othman Tamimu wa Coastal Union kujifunga wakati akijaribu kuondosha hatari kwenye lango lake.
Bao la kufutia machozi la Coastal Union lilifungwa na kiungo wa kimataifa wa Kenya, Jerry Santo.

source: Liwazo Zito Blog
No comments:
Post a Comment