WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, November 12, 2012

Mbowe:Karibu Chadema Sumaye


Hanang
MWENYEKITI  wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemtaka Waziri Mkuu, mstaafu Fredricke Sumaye, kujiondoa CCM na kujiunga na Chadema, bila masharti ya kuteuliwa na chama hicho kugombea urais mwaka 2015.

Akizungumza katika mkutano mkubwa katika mji wa Katesh ambako ni nyumbani kwa Sumaye na Nagu, Mbowe alisema anashangazwa na Sumaye kuendelea kulalamikia rushwa iliyosababishia kushindwa kupata ujumbe wa Halmashauri Kuu ya (NEC) kupitia Wilaya ya Hanang.

Katika mkutano, mamia ya wafuasi wa Sumaye, wakiwemo wazee maarufu wa CCM katika Kata ya Endasaki, wajiunga na Chadema.


Wafuasi hao ni wale waliokuwa wakipinga Dk Nagu kupambana na Sumaye katika kuwania ujumbe wa NEC.

Katika hotuba yake, Mbowe alisema Sumaye  ndiye alimlea Dk Nagu bila kujua anafuga mzimu ndani ya nyumba yake.

“Baada ya matokeo ya NEC Hanang , nilimpigia simu Sumaye nikamweleza tayari ameshindwa na anachopaswa kufanya ni kuvua gamba na kuvaa gwanda na sio kuendeleza malalamiko ya kushindwa,” alisema Mbowe.

Hata hivyo, baadaye akizungumza na Mwananchi, alisema wanamkaribisha Sumaye Chadema, bila masharti yoyote na kama anataka kugombea urais, wanachama wa Chadema, watazichambua sifa zake.

Alisema kwa sasa chama hicho,hakijadili masuala ya urais na kwamba inachokifanyua ni kujiimarisha.

 

Hata hivyo, aliwataka wanachama na baadhi ya viongozi wa Chadema, wenye nia ya kugombea urais, wasubiri vikao na kwamba wakati huu si muafaka kutangaza nia.

Hivi karibuni,Naibu Katibu Mkuu Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma, Kaskazini, Kabwe Zitto, alitangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kupitia Chadema.


Akizungumzia kukithiri kwa rushwa katika uchaguzi wa CCM, Mbowe alisema CCM imepoteza mwelekeo wa kupambana na rushwa.

“Leo (jana) Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete anawaomba wanaCCM wanaogombea  nafasi mbalimbali,  kuacha rushwa tena kwa kauli ya upole wakati yeye kama Rais, wizara inayohusika na rushwa ipo chini yake, sambambamba na Takukuru," alisema.

Alisema viongozi wote wa CCM, wanaoendelea na vikao vyao mjini Dodoma wamepatikana kwa misingi ya rushwa jambo ambalo ni hatari hasa ikizingatiwa kuwa miongoni mwao kuna mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na  wengine wa juu.

 Alisema hata hivyo kushindwa kwa Sumaye ni kielelezo cha kutosha kuwa bila fedha huwezi kushika uongozi ndani ya CCM .

“Kama Sumaye, alikuwa Waziri Mkuu, mbunge wa jimbo hili kwa miaka 10 na ameshika nafasi nyingi serikalini ameshindwa kupata uongozi ndani ya CCM, mwananchi maskini utashinda nafasi gani,”alihoji Mbowe.

Alisema hata katika chaguzi zinazoendelea sasa, Watanzania wasitegemee jambo jipya hasa ikizingatiwa kuwa hata viongozi walioko madarakani, wamepatikana kwa njia ya rushwa.

Katika mkutano huo, Mbowe alizungumzia pia hali ngumu ya maisha na kwamba inatokana na Serikali kuwa na mlolongo wa  kodi kubwa katika bidhaa mbali mbali muhimu kama sukari, mafuta, unga  na vifaa vya ujenzi.

“Serikali inajisifia kwa kukusanya kodi kubwa na sasa imefikia Sh450 bilioni kwa mwezi  lakini hapo hapo inawanyonya wananchi wake,”alisema Mbowe.

Mbowe aliwaomba wakazi wa wilaya hiyo na maeneo mengine nchini, kuendelea kukiunga mkono chama hicho, ili kiweze kushika dola katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.

Mwananchi

No comments:

Post a Comment