Na Mwandishi Wetu
KITENDO cha Mahakama ya Rufaa kukubali
kusikiliza marejeo ya hukumu ya kifungo cha maisha jela katika kesi
iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viking 'Babu Seya' na mwanaye
Johnson Nguza 'Papii Kocha' kimetafsiriwa kuwa ni kama wamepata nafasi
ya mwisho ya kuweza kujinasua.
WARAKA WA PAPII KOCHA
Mahakama
hiyo ilikubali ombi hilo hivi karibuni na kueleza kuwa marejeo hayo
yanatarajiwa kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu ikiwa ni miezi kadhaa
baada ya Papii Kocha kutuma waraka wa kuomba msamaha kwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ndiye aliyekubali
kuufikisha kwa JK hivyo kuna madai kuwa huenda waraka huo ndiyo umezaa
matunda.(P.T)
WARAKA UMEZAA MATUNDA?
"Unajua
ule waraka ulikuwa na maneno ya kuumiza sana. Inawezekana kabisa kuwa
ulimfikia JK akaagiza suala hilo liangaliwe upya. Haina maana kuwa JK
anaingilia sheria. Nadhani wanasheria wana vipengele vingi ambavyo
vinaruhusu marejeo ya rufaa hiyo. Kilichopo hapa ni namna ya kuzitafsiri
sheria kisha kuona kama rufaa hiyo inaweza kusikilizwa.
"Ninachojua ni kwamba Babu Seya na
Papii Kocha wamepata nafasi ya mwisho ya kuweza kujinasua kwa sababu
hata wakili wao (Mabere Marando) yupo vizuri katika kuwatetea wateja
wake.
MUNGU ANAWEZA
"Mimi naamini Mungu anaweza yote hivyo tuwaombee rufaa yao iende vizuri," alisema mmoja wa ndugu wa familia ya Nguza.
Awali
mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi iliyowahusisha na
ubakaji wa watoto kumi wa Shule ya Msingi, Mashujaa iliyopo Sinza, Dar,
Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao Marando waliomba marejeo ya hukumu
hiyo.
JOPO LA MAJAJI
Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati.
Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati.
Katika hukumu hiyo iliyotolewa
Februari 2010, mahakama hiyo iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa
Babu Seya na Papii Kocha huku ikiwaachia huru watoto wawili wa Babu
Seya, Nguza Mbangu na Francis Nguza.
WATIWA HATIANI
Juni
25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar,
iliwatia hatiani Babu Seya na wanaye hao kwa kupatikana na hatia ya
kubaka na kulawiti.
Januari 27,
mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo
alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na
aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy
Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa
nayo Juni 25, mwaka 2004.
Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda
makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na
makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huohuo kati ya
Aprili na Oktoba 2003.
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment