Na Daniel Mbega
DEMOKRASIA ya sasa imepanuka kuliko
ilivyokuwa miaka ya nyuma, hasa kipindi cha ukoloni. Leo hii
tunashuhudia hata vijana wa shule wanaifahamu vyema siasa, huku uongozi
ukishikwa na vijana wadogo, wengine wakiwa hawajafikisha hata miaka 30.
Mwaka huu tunapomuenzi Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo
chake, tumeona bora tuzungumze, na tulete hotuba yake, akielezea namna
alivyoanza
siasa miaka ile ya 1950, mara baada ya kurejea kutoka mamsomoni Scotland.
Yeye anasema kwamba alianza akiwa
'mdogo' akiwa na miaka 30 hivi mwaka 1952 aliporejea, lakini kwa sasa
ukitaja miaka hiyo huwezi amini kama hukuwakuta waheshimiwa Wabunge wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hata wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar wakiwa wametopea kweli kwenye siasa.
Kwa miaka ile umri huo alikuwa bado mdogo, na hata yeye mwenyewe anakiri kwamba alikuwa kijana mdogo.
Hata hivyo, Mwalimu aliamini kwamba
wazee ndio nguzo ya maendeleo ya nchi, kwani yeye mwenyewe asingeweza
kufanikiwa kama si kulelewa na wazee waliompa miongozo ya kutosha hadi
akafikia mahali alipofikia.
Mwalimu aliyasema haya mbele ya Baraza
la Wazee wa Dar es Salaam wakati alipokuwa akiagana nao kabla ya
kung'atuka mwaka 1985. Hebu tuungane...
"MIMI nimeanza siasa na wazee wa Dar
es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli.
Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma.
Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi. (MNYAMA)
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment