WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, October 16, 2013

Neno La Leo: Ujasiri Na Unyenyekevu..


1377003_10201480627510353_2094433159_n_7b389.jpg
Ndugu zangu,
Rais wa nchi hasikii ya kuambiwa, bali ya kushauriwa. Hivyo, anayoambiwa ni anayoshauriwa. Akiyasikiliza anakuwa amesikiliza aliyoshauriwa.
Kuna simulizi ya Bwana mwenye hekima aliyekwenda kwenye mkutano wa Khalifa Haroun Arrashid.
Bwana huyo mwenye hekima alikuwa ni mshauri wa Khalifa na mwenye mazoea ya kuhudhuria mikutano ya Khalifa Haroun Arrashid.
Siku moja akiwa kwenye mkutano, Bwana mwenye hekima na ambaye aliaminiwa na Khalifa Haroun Arrashid alimwona Khalifa Arrashid akiwa kwenye mabishano makubwa na wapinzani wake.
Bwana yule akamwambia Khalifa Haroun Arrashid;
" Hivi, ungefanyaje kama ungalikuwa jangwani na ukawa na kiu kali ya maji, akatokea mtu mwenye maji na akakwambia; kuwa yu tayari kukupa maji kwa sharti la wewe kumpa nusu ya mali zako?
Khalifa Haroun Arrashid akajibu;
" Ningekubali"
Bwana yule mshauri wa Khalifa akaongeza;
" Na ungefanyaje kama ungelikuwa mwenye kuhitaji, na kwamba ungepaswa utoe maji yako ili unusurike, lakini hukuweza, na akatokea mtu akakwambia; nipe nusu ya mali yako ili nikusaidie.
Khalifa Haroun Arrashid akajibu;
" Ningefanya hivyo".
Naam, inahusu mambo mawili; ujasiri na unyenyekevu. Kwa mwanadamu, na hususan kiongozi, lililo na faida kubwa ni kuwa nayo yote mawili.
Jakaya Kikwete, kwa kuwa tayari mara zote kukutana na kukaa meza moja na wapinzani wake wa kisiasa, ameonyesha kuwa na sifa hizo mbili; Ujasiri na unyenyekevu.
Eid Mubarak.
Maggid.
Iringa.(P.T)

No comments:

Post a Comment