Hasira
za Wamarekeni kwa Serikali na Wawakilishi wao zimeishia kwenye mitandao
ya kijamii kama vile Twitter, Facebook na Instagram huku kila mmoja
akilaumu upande anaoona ndiyo uliosababisha shughuli muhimu za
Kiserikali kufungwa kutokana na mzozo wa bajeti baina ya Republicans
wanaoshikilia Baraza la Wawakilishi, na Democrats wanaoshikiliza Seneti
ya Marekani.
Maoni ya wengi yamekazia kuwafahamisha viongozi hao kuwa "hawajakomaa", ni "wajinga" na "wapuuzi" wanaopaswa

"kupevuka" ("immature", "stupid", "idiots", "grow up").
Baadhi ya wahafidhina wachache wanaojiita wawakilishi wa majimbo-mekundu (red-State) wao waliunga mkono hatua ya wawakilishi wa Republican ya kuzuia mpango wa afya wa Rais Barack Obama, hata ikiwa matokeo yake ni kusababisha baadhi ya miradi mikubwa na maarufu ya Serikali kuzorota pamoja na waajiriwa wa Serikali zaidi ya laki nane kukosa mshahara kwa kipindi kisichofahamika.
Lakini wengi wa waliotoa maoni kwenye mtandao wa Twitter walisema hawaelewi ni kwa nini viongozi wao hawakuweza kufikia muafaka ili kuinusuru Serikali.
Mmoja wao aliwaambia Wawakilishi hao kuwa hawastahili kulipwa mshahara, tena inapaswa watimuliwe kazini, "DearCongress, You should noe be getting paind. In fact, you all should be firee!" aliandika Bruce Swedal (46) mkazi wa Denver, dalali wa nyumba na viwanja ambaye anasema ana wasiwasi kuhusu mustakabali wa mauzo ya nyumba endapo mikopo inayoidhinishwa na Serikali itakauka kwa kukosa fedha za kukopesha, jambo ambalo litaathiri ajira na kipato chake.
Kufungwa kwa baadhi ya ofisi na huduma zinazotolewa na Serikali ya Marekani kumesababisha hata baadhi ya tovuti zinazohusika na huduma muhimu kama vile sensa na takwimu, kilimo na maktaba ya masuala ya kihistoria kufungwa, hata ikiwa tovuti hulipiwa ada ya usajili wa jina kwa kipindi cha mwaka mzima na 'hosting' kwa kipindi cha kati ya miezi sita na kuendelea, kwa kile kilichoelezwa kwenye tovuti hizo kuwa ni kukosekana kwa mtu atakayeweza kutoa huduma pale itakapohitajika kwa wauliza maswali au wataka ufafanuzi.

No comments:
Post a Comment