KENYA imeingia mchecheto na makali ya
Kilimanjaro Stars na sasa imebainika kwamba Kocha Adel Amrouche ndiye
aliyesisitiza mechi ikachezwe Machakos badala ya Mombasa.
Kenya itacheza na Stars kesho Jumanne kwenye mechi ya nusu fainali ya Chalenji kwenye Uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.
Awali nusu fainali hiyo ilikuwa
ichezwe hapa Mombasa, lakini kutokana na hali ya joto ambayo inaibeba
Tanzania na kukaa vibaya kwa wachezaji wa Kenya wanaoishi Nairobi kwenye
baridi ndio maana mechi hiyo imeahirishwa.
Baada ya mechi dhidi ya Rwanda ambapo
Kenya ilishinda bao 1-0, Adel alikiri kwamba; "Hali ya hewa ya Mombasa
si nzuri kwetu ni joto kiasi na wachezaji wangu hawajazoea."
Habari za ndani zinadai baada ya
Uwanja wa Kisumu kushindikana kumalizika kwa wakati waandaji walipanga
mechi za nusu fainali zichezwe Mombasa na fainali ikachezwe Nyayo mjini
Nairobi lakini kwa hali waliyoiona katika mechi za juzi Jumamosi wenyeji
wakaamua kupeleka mechi ya Stars Machakos. Mechi nyingine ya nusu
fainali itachezwa mjini Mombasa.(P.T)
Habari za ndani zinadai kwamba Adel
amewaambia viongozi wake kwamba endapo Kenya ikicheza na Stars mjini
Mombasa itakuwa kwenye wakati mgumu kutokana na Tanzania kuzoea hali ya
joto na vilevile ina sapoti kubwa Mombasa kwavile ni jirani na Tanga.
Kenya iko kwenye presha ya kufuzu
fainali kwani siku ya fainali nchi hiyo itakuwa ikisherehekea Jubilee ya
miaka 50 ya uhuru wake.
Wakati huohuo, Zambia iliitoa Burundi
kwa penalti 4-3 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika jana Jumapili
hivyo kutinga nusu fainali.
Chanzo:http://www.mwanaspoti.co.tz
No comments:
Post a Comment