GREAT MAN OF ALL TIMES;
Dunia
nzima imeshitushwa na kifo cha shujaa wa Africa Raisi wa kwanza Mweusi na
mpiganiaji haki wa Afrika kusini na dunia kwa ujumla hayati Nelson Mandela;
Swali la kujiuliza kwa nini kifo chake kimevuta hisia za
mataifa yote duniani?
Kwa
ufupi Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa
tarehe 18 Julai,mwaka 1918. Ni Rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia
Nchini Afrika Kusini. Alikuwa Mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa
za ubaguzi katika Afrika ya Kusini.
Mandela alianzisha
kampeini ya kuhujumu serikali. Hatimaye alikamatwa na kushtakiwa kwa kosa la
kuwa na njama ya kuipindua serikali. Kutokana na kosa hilo Mandela alitumikia kifungo cha
maisha kwa miaka 27, alifungwa katika kisiwa cha Robben; jela
lenye ulinzi mkali mjini Cape, Table Bay
Mwaka 1990, .W. de Klerk,
alitangaza kuondoa marufuku dhidi ya chama tawala ANC hatua ambayo iliwezesha Mandela,
hatimaye alichiliwa huru.
Kufuatia kuachiwa huru
mwaka 1994 chama na ANC kilipata fursa ya kushiriki uchaguzi wa kwanza wa
kidemokrasia, na ambao uliwahusisha wazungu na waafrika,na hatimaye chama cha
ANC kilishinda uchaguzi huo na Nelson Mandela kuapishwa kuwa Raisi wa kwanza
Mweusi kuongoza Afrika ya kusini.
FIKRA TIMILIFU:
Tunafahamu
kuwa Mandela alilikuwa kiongozi mpinanaji ambaye hakupenda siasa za ubaguzi wa
rangi ambazo zilikuwa zikiendeshwa na makaburi waliotawala Africa kusini pamoja
na washirika wake; kwa maneno mengine Mandela alikuwa kiongozi mwenye si tu hekima bali pia aliweza kuongozi kwa kuzingatia uadilifu.
Tunachojifunza
sasa ni kuwa viongozi wengi ambao walikuwa waadilifu kama Mandela ndio wamekufa,
na wengine wanaendelea kufa; hata waliobaki, tuliokuwa tunawategemea, wameanza
kutukatisha tamaa.
UONGOZI WENYE TIJA
Mandela aliongoza
Taifa lake kwa kipindi kimoja tu; na aliacha madaraka kwa furaha na upendo mkubwa na kuwapisha wengine nao waongoze;
baada ya kukaa gerezani kwa miaka 27 hakuwa na uchu wa madaraka baada ya
kuwaunganisha wanasouth Afrika pamoja na kuondoa zana ya ubaguzi kati ya
makaburu na wananchi wazalendo wa Afrika kusini; ni kiongozi wa ajabu ambaye
alipigania usawa na umoja bila kujali rangi na dini;
2004
Thabo Mbeki alichukua mamlaka kutoka kwa Mandela
kama kiongozi wa chama tawala ANC na hata kushinda uchaguzi wa mwaka
1999.Mandela alimuoa Graca Machel, mjane wa aliyekuwa rais wa Msumbiji, akiwa
na miaka 80. Aligunduliwa kuwa na saratani ya Tezi Kibofu na hivyo kuanza
matibabu.Mnamo mwaka 2004, alitangaza kujiuzulu, akisema kuwa anataka maisha ya
kimya nyumbani kwake na familia yake. Kwa mzaha aliwaambia wandishi wa habari
wasimpigie simu.
Mandela baada ya kutoka gerezani na wakti huu
akiwa raisi wa Afrika ya kusini aliweza kuendesha mijadala, mikubwa ya kisomi yenye kutafakari ya njia
sahihi ya kuleta umoja wa wana afrika
kusini na hivyo kuyaonyesha mataifa makubwa kuwa hata Africa tunajua nini maana
ya demokrasia na kuvumiliana na si tabia ya kulipiza kisasi.
Mandela ndiye
aliyekuwa na nguvu za kiutawala tangu lakini alitoa fursa kwa wengine pia nao
waweze kuonyesha uwezo wao na vipaji vyao katika kuongoza, hakuwa mbinafsi
alikuwa ni kisima cha hekima ambacho alitamani wengine ambao wanataka kuchota
maarifa wafaidike.
Historia inatuambia kwamba
viongozi wengi waliofanikiwa ni wale ambao walikuwa na wafuasi wa kweli,
wafuasi ambao walikuwa tayari hata kupoteza maisha yao ili kulinda na kutetea
itikadi na harakati zilizoanzishwa na viongozi wao. Na hapa sizungumzii
madikteta waliolazimisha itikadi zao kwa wafuasi wao kwa mkono wa chuma na
kumwaga damu.
Mandela atakumbukwa sana
kwa kuweka maslahi ya taifa lake mbele. Pamoja na Hatati Mwalimu Nyerere,
Nkwame Nkuruma Moses Macheli ni viongozi ambao kwa pamoja walisimamia na
kutetea sana haki za wana Afrika. Hakutetea hata siku
moja siasa za ubeberu, walizipinga kwa nguvu zote na kwa gharama yeyote
ile.
“Kama kuna kitu cha muhimu alichokifanya
Mandela basi ni kuhimiza wanaafrika
kusini wawe kitu kimoja na kuutokomeza ugaguzi.
Hebu tujikumbushe matukio makuu ambayo Marehemu Nelson Mandela amepitia:
Februari
11, 1990
BAADA
ya miaka 27 jela, Nelson Mandela, hatimaye aachiwa na serikali ya makaburu wa
Afrika ya Kusini iliyokuwa ikiongozwa na Rais Fredrick Willem de Klerk.
Tukio
hilo ni miongoni mwa matukio makubwa katika historia ya Afrika Kusini maana
lilimaanisha kwamba makaburu wameanza kutambua kwamba hawawezi kushindana na
nguvu ya umma.
Julai
5, 1991
Chama
cha African National Congress (ANC) chamchagua kuwa Rais wa Afrika Kusini.
Mandela alipewa nafasi hiyo akichukua nafasi ya swahiba wake wa kisiasa, Oliver
Tambo, aliyefariki dunia.
Wadhifa
huo ndio uliomwezesha kuchaguliwa na chama chake kuwania urais wa Afrika Kusini
baadaye.
Aprili,
1992
Atangaza
kuachana na aliyekuwa mkewe, Nomzamo Winnie Madkizela Mandela, baada ya
uhusiano wao wa zaidi ya miaka 30 uliotawaliwa na misukosuko mingi.
Inadaiwa
Mandela alimuacha Winnie kutokana na mwanamama huyo kudaiwa kuwa na mahusiano
ya kimapenzi na vijana wadogo mbalimbali ndani ya ANC aliokuwa akifanya nao
kazi.
Oktoba
15, 1993
Atunukiwa
tuzo ya Nobel kwa pamoja na De Klerk kutokana na mchango mkubwa katika kuleta
upatanishi na maelewano nchini Afrika Kusini.
Mei
10, 1994
Achaguliwa
kwa kura nyingi kuwa Rais wa Kwanza Mweusi katika Uchaguzi wa Kwanza wa
Kidemokrasia nchini Afrika Mashariki. Urais wake unaashiria kumalizika rasmi
kwa zama za ubaguzi wa rangi nchini humo.
Julai
18, 1998
Akiwa
ziarani nchini Canada, ofisi yake yatangaza kwamba anamuoa Graca Machel, mke wa
rais wa zamani wa Msumbiji, Samora Machel.
Ndoa
hiyo inaelezwa kumaliza upweke aliokuwa nao Mandela kutokana na uamuzi wake wa
kumuacha Winnie miaka saba nyuma.
Mwaka
1999
Baada
ya miaka mitano ya urais, Mandela alitangaza kutowania nafasi hiyo katika
uchaguzi unaofuata na badala yake akamuachia makamu wake, Thabo Mvyelwa Mbeki,
kuwania nafasi hiyo.
Mandela
aliachia ngazi wakati bado akipendwa na wananchi wake. Hatua yake ya kuachia
ngazi ilikwenda kinyume na viongozi wengi wa Afrika ambao hupendelea
kung’ang’ania madaraka.
Mwaka
2000
Achaguliwa
kuwa msuluhishi wa mgogoro wa Burundi akichukua nafasi ya Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere, aliyefariki dunia mwaka mmoja nyuma.
Kazi
hiyo aliifanya hadi alipoanza kudhoofu kiafya na akamwachia aliyekuwa Makamu wa
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ambaye sasa ndiye rais wa nchi hiyo.
Mwaka
2001
Baada
ya vipimo vya kitabibu, Mandela alibainika kuwa na ugonjwa wa kansa ya tezi ya
kiume ya uzazi (prostate cancer).
Taifa
la Afrika Kusini lilipatwa na mshtuko mkubwa kutokana na na habari hizo za
kushtusha kumhusu kiongozi wao mpendwa.
Mwaka
2003
Kutokana
na hatua ya Marekani na washirika wake kuivamia Irak kwenye vita ya pili ya
Ghuba ikidai ina silaha za maangamizi, Mandela azungumza hadharani na kukemea
sera za nje za taifa hilo kubwa duniani.
Mwaka
2004
Mandela
atangaza kurejea kijijini kwake Qunu na kusema hatakuwa akionekana tena
hadharani mara kwa mara. Aomba aachwe apumzike na wajukuu zake.
Aprili
19, 2009
Mandela
atoa hotuba ya mwisho ya kisiasa baada ya kuongea kupitia hotuba iliyorekodiwa
kwenye mkutano wa hadhara wa ANC wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini.
Kulikuwa
na utata kuhusu iwapo Mandela amependezewa na hatua ya ANC kumchagua Jacob Zuma
kuwa mgombea wake wa urais badala ya Mbeki.
Kwenye
hotuba hiyo, Mandela aliweka hadharani msimamo wake wa kumuunga mkono Zuma na
ANC. “Nitakuwa na ANC hadi kufa kwangu,” alisema Mandela.
Januari
26, 2011
Alazwa
hospitali kutokana na kile kilichoelezwa kuwa matatizo katika mfumo wake wa
kupumua.
Matatizo
haya ndiyo yalikuwa kama yamefungulia njia ya yeye kuanza kuumwa mfululizo.
Februari
25, 2012
Alazwa
hospitali kutokana na kusumbuliwa na maumivu makali ya tumbo.
Desemba
8, 2012 hadi Januari 6, 2013
Anakimbizwa
hospitalini na kulazwa kwa takribani mwezi mmoja baada ya kukutwa na mawe
kwenye kongosho lake. Huu ndiyo muda mrefu zaidi kwa kiongozi huyo kukaa
hospitali tangu apatwe na matatizo ya kiafya.
Machi
28 hadi April 6, 2013
Mandela
alazwa tena hospitali kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kichomi
(Pneumonia).
Juni
8, 2013
Alazwa
hospitali kutokana na matatizo katika mapafu.
DECEMBER 5 2013-
Afariki Dunia
Mzee Nelson “Madiba” Mandela amefariki dunia kwa
mujibu wa CNN mzee Madiba amefariki dunia tarehe 05/12/2013 akiwa na umri wa
miaka 95.Kwa mujibu wa Rais wa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema mzee
Mandela amefariki Ijumaa usiku baada ya kuugua kwa muda mrefu.Anatarajiwa
kuzikwa tarehe 15/12/2013.
MWENYEZI MUNGU
AIPUMZISHE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI: SISI TULIMPENDA SANA SHUJAA WETU
LAKINI MWENYEZI MUNGU AMEMPENDA ZAIDI; AMEN
NELSON MANDELA INSPIRATIONAL QUATATIONS
"I was made, by
the law, a criminal, not because of what I had done, but because of what I
stood for, because of what I thought, because of my conscience.” Mandela, 1962.
“Social equality is
the only basis of human happiness.”
Mandela, 1970
"Great anger and
violence can never build a nation. We are striving to proceed in a manner and
towards a result, which will ensure that all our people, both black and white,
emerge as victors” - Mandela 1990.
“When a man has done
what he considers to be his duty to his people and his country, he can rest in
peace” - Mandela, 1994.
"Reconciliation
means working together to correct the legacy of past injustice.” - Mandela 1995.
"If you want to
make peace with your enemy, you have to work with your enemy. Then he becomes
your partner." - Mandela 1995.
"I like friends
who have independent minds because they tend to make you see problems from all
angles." - Mandela
"I hate race
discrimination most intensely and in all its manifestations. I have fought it
all during my life; I fight it now, and will do so until the end of my
days." - Mandela
“A leader. . .is like
a shepherd. He stays behind the flock, letting the most nimble go out ahead,
whereupon the others follow, not realizing that all along they are being
directed from behind.” —Long Walk to Freedom: The Autobiography of Nelson
Mandela
“No one is born hating
another person because of the color of his skin, or his background, or his
religion. People must learn to hate, and if they can learn to hate, they can be
taught to love, for love comes more naturally to the human heart than its
opposite.” —Long Walk to Freedom: The Autobiography of Nelson Mandela
“I have walked that
long road to freedom. I have tried not to falter; I have made missteps along
the way. But I have discovered the secret that after climbing a great hill, one
only finds that there are many more hills to climb. I have taken a moment” - Mandela
“The greatest glory in
living lies not in ever falling, but in rising every time we fall.” - Mandela
“Difficulties break some men but make others. No
axe is sharp enough to cut the soul of a sinner who keeps on trying, one armed
with the hope that he will rise even in the end.” —From a letter to Winnie
Mandela, 1975
Today we are entering
a new era for our country and its people. Today we celebrate not the victory of
a party, but a victory for all the people of South Africa… The task at hand on
will not be easy. But you have mandated us to change South Africa from a
country in which the majority lived with little hope, to one in which they can
live and work with dignity, with a sense of self-esteem and confidence in the
future. –mandela- Inaugural speech, May 9, 1994
No one truly knows a
nation until one has been inside its jails. A nation should not be judged by
how it treats its highest citizens but its lowest ones. –Mandela Long Walk to
Freedom
I have walked that
long road to freedom. I have tried not to falter; I have made missteps along
the way. But I have discovered the secret that after climbing a great hill, one
only finds that there are many more hills to climb. I have taken a moment here
to rest, to steal a view of the glorious vista that surrounds me, to look back
on the distance I have come. But I can rest only for a moment, for with freedom
comes responsibilities, and I dare not linger, for my long walk is not yet
ended. –Mandela Long Walk to Freedom
RIP NELSNON MANDELA THE GREAT MAN OF ALL TIMES
No comments:
Post a Comment