WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, December 19, 2013

Ndege Ethiopia yakwama kutua KIA, yatua Arusha

Ndege aina ya Boeing 767 ya Ethiopian Airlines, ikiwa na abiria 213, ililazimika kutua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Arusha kutokana na ndege moja kuharibika katika njia ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana. Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 300, iliekelekezwa ikatue kwa dharura jijini Nairobi lakini ilishindwa kufanya hivyo kutokana na kuishiwa mafuta.
Umati wa wakazi wa Jiji la Arusha jana ulifurika katika Uwanja wa ndege wa Arusha, kushangaa ndege aina ya Boeing 767 mali ya Shirika la Ndege la Ethiopia, iliyotua uwanjani hapo kwa dharura, badala ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ikiwa na abiria 213.
Kwa mujibu wa mmoja wa walinzi wa Uwanja wa Ndege wa Arusha, ambaye jina lake hakutaka kutajwa, ndege hiyo ilikuwa ikitokea Addis Ababa kuelekea KIA, ikiwa  abiria hao na afanyakazi 15.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo, alisema, rubani wa ndege hiyo aliombwa kuzunguka kwa muda angani, ili kupisha ndege iliyokuwa imepata hitilafu KIA kuondolewa.

Alisema waongoza ndege wa KIA walimpa maelekezo rubani wa ndege hiyo na kumuomba aende kutua Nairobi, Kenya au Dar es Salaam, lakini aliwaeleza kuwa hakuwa na mafuta ya kutosha.
Mulongo alisema alipopewa maelekezo ya kushuka, walimuuliza kama anauona uwanja na kuwaambia kuwa anauona na tayari alikuwa ameanza kushuka akidai ni Nairobi kumbe ni Uwanja wa Arusha.
Alisema pamoja na kutua kwa dharura, hakuna abiria aliyepata majeraha zaidi ya hofu kutokana na kupoteza mwelekea na kwenda kwenye nyasi uwanjani hapo.
Meneja wa Uwanja mdogo wa Arusha, Ester Dede, alithibitisha ndege hiyo na kwamba ni mali ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Baadhi ya wakazi  waliiona ndege hiyo katika maeneo ya Ngarenaro na Majengo walidhani ilikuwa inaenda kuanguka kutokana na kuyumbayumba ikiwa angani.

Hata hivyo, rubani alifanikiwa kuishusha salama na alienda  hadi mwisho wa uwanja, lakini ilishindwa kugeuka kutokana na uwanjwa kuwa mdogo.

Kutokana na uwanja kuwa mdogo ndege hiyo ilijikuta ikizunguka hadi kwenye nyasi nje ya uwanja wa lami na kusababisha tairi za mbele  kukitia kwenye udogo huku tairi za nyuma zikititia pia kwenye nyasi.

Tukio hilo lililotokea jana saa 7:00 mchana lilisababisha pia ndenge ndogo zinazotumia uwanja  mdogo wa Arusha kuzuiwa kuruka hadi saa 9:42 alasiri huku ndege hiyo ikiwa pembeni mwa uwanja kwenye majani.

Wakati ndege hiyo iliposimama ikiwa nje ya uwanja kwenye majani huku tairi zake zikiwa zimetitia kwenye udongo kutokana na mvua kunyesha, abiria 213 walizuiwa kushuka na wahuduma wa ndege hiyo kwa kutumia magari ya Zima Moto ya Manispaa ya Arusha.

Pamoja na juhudi za maofisa wa Usalama, Uhamiaji na Polisi  kutaka kuwashusha abiria hao, wahuduma waliendelea kusimama mlangoni wakizuia abiria hadi hapo gari lenye ngazi kutoka KIA lifike.

Hadi saa 11 jioni abiria wa ndege hiyo walikuwa hawajashuka huku wengine wakionekana kupandwa na shinikizo la damu na kulazimika kupepewa na ndugu zao.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment