Polisi mkoani Kigoma, imemshauri,
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod
Slaa kusitisha ziara zake mkoani Kigoma kwa sababu za kiusalama.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Zedekia Makunja alisema jana: "Ni ushauri tu tunatoa kwa Dk Slaa kwamba anaweza kuahirisha kutokana na hali ilivyo hapa." Hata hivyo, Kamanda Makunja alisema pamoja na yote hayo bado Polisi mkoani, Kigoma imejipanga imara kukabiliana na vurugu zozote zinazoweza kutokea katika ziara hiyo.(HD)
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Zedekia Makunja alisema jana: "Ni ushauri tu tunatoa kwa Dk Slaa kwamba anaweza kuahirisha kutokana na hali ilivyo hapa." Hata hivyo, Kamanda Makunja alisema pamoja na yote hayo bado Polisi mkoani, Kigoma imejipanga imara kukabiliana na vurugu zozote zinazoweza kutokea katika ziara hiyo.(HD)
Lakini Dk Slaa alipoulizwa kuhusu
ushauri huo alisema hawezi kufuta ziara hiyo na kusema hahofii chochote.
Alisema na alishafahamu siku nyingi kuwa hayo yanayotokea. Juzi, vijana
mbalimbali waliandamana kwa pikipiki na wengine wakitembea kwa mguu
huku wakiwa na mabango kupinga ziara ya Dk Slaa Kigoma. Anatarajiwa
kuwasili Kigoma Kaskazini keshokutwa.
Hatua hiyo ya kupinga ziara hiyo,
imetokana na Kamati Kuu ya Chadema kumvua madaraka aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma
Kaskazini.
Wakizungumza baada ya maandamano yao
yaliyoanzia Kijiji cha Mwandiga kilichopo Kigoma Kaskazini hadi Uwanja
wa Mwanga Center, Kigoma, vijana hao walisema kundi hilo halimuungi
mkono Dk Slaa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema
katika Kijiji cha Mwandiga, Mtoro Mvunye alisema: "Tumetoa wito kwa Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Issa Machibya na Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kigoma (RPC) Fraser Kashai kusitisha ziara hiyo mara moja."
Akizungumza baada ya kupokea
maandamano hayo juzi, Mvunye alisema hawataki kumwona Dk Slaa akifika
katika Kijiji cha Mwandiga, Ujiji na Mwanga.
"Kwanza nampongeza Mkuu wa Mkoa na RPC
kwa kusimamia vizuri maendeleo ya Kigoma, lakini nataka niwaeleze
kwamba endapo hawatachukua hatua ya kumzuia Dk Slaa kuja hapa Kigoma,
hawa watu wanatudharau sana sisi wa Kaskazini," alisema Mvunye.
Alitoa wito kwa wanachama wa Chadema
kutowapigia kura kuwachagua viongozi wote wa mikoa na majimbo
walioonyesha kutomuunga mkono Zitto katika sakata hilo ambalo
limesababisha mgawanyiko kwa baadhi ya mikoa.
Mjini Singida, Baraza la Uongozi
mkoani Singida, limemtaka aliyekuwa Mwenyekiti Chadema Mkoa huo, Wilfred
Kitundu kuomba radhi ndani ya siku 14 kutokana na kutoa taarifa ya
uongo, uzushi na upotoshaji mkubwa wakati akitangaza kujiuzulu nafasi
yake hiyo. Taarifa ya Baraza la Uongozi ilisema asipotekeleza agizo
hilo, atavuliwa uanachama. Akisoma taarifa hiyo, Kaimu Mwenyekiti,
Shaaban Limu alisema tuhuma zilizotolewa na Kitundu kuwa uamuzi
uliotolewa na Kamati Kuu ya kuwavua uongozi kina Zitto na wenzake ni za
kipuuzi ni zake binafsi na si za Chadema.
Vurugu zavunja mkutano wa Dk Slaa
Vurugu kubwa zilizuka jana na
kusababisha mkutano wa Dk Wilbrod Slaa uliokuwa ukifanyika kwenye Uwanja
wa Kigalamo, Kasulu kuvunjika.Mkutano huo ulivunjika baada ya polisi
kufyatua mabomu ya kutoa machozi kwa kundi la vijana waliokuwa wakifanya
vurugu kwa kuwarushia mawe wanachama na wapenzi wa chama hicho
waliokuwa wakimsikiliza Dk Slaa.
Vurugu hizo zilianza baada ya Dk Slaa kumaliza kuhutubia na kuruhusu watu kuuliza maswali.
Polisi walichukua hatua hiyo baada ya
kuona hali inazidi kuwa mbaya. Walifyatua mabomu kutawanya kundi hilo na
kumteremsha Dk Slaa harakaharaka jukwaani na kuingizwa kwenye gari na
kuondoka chini ya ulinzi vijana wa chama hicho, Red Brigade.
Imeandikwa na Frederick Katulanda, Thomas Kayanda na Gasper Andrew.
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment