Dar es Salaam. Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetakiwa kuweka kando tofauti za
kisiasa na kuunganisha nguvu zao, hasa katika kipindi hiki ambacho taifa
lipo katika mchakato wa uundaji wa Katiba Mpya.
Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa
akifungua mkutano wa baraza kuu la chama hicho.
Alisema kuwa chama hicho chenye wabunge wengi
kinapaswa kutafakari na kuweka kando itikadi za vyama na kuangalia
mustakabali wa nchi katika kipindi muhimu.
“Ningependa kuwashauri Chadema kama chama chenye
wawakiishi wengi bungeni kinapaswa kuweka kando tofauti za kisiasa na
kuunganisha nguvu katika kwa kuangalia masilahi na mustakabali wa
taifa,” alisema
“Licha ya changamoto tulizonazo hakuna sababu ya kukata tamaa mapema kiasi hiki, tunapaswa kuondoa tofauti zetu za kisiasa a.”
Kauli hiyo ya Lipumba inakuja kutokana na vuguvugu
la mgogoro ulioibuka hivi karibuni ndani ya Chadema ambao ulisababisha
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe kuvuliwa nafasi
zake zote za uongozi.
source: mwananchi
source: mwananchi
No comments:
Post a Comment