Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe
Mama Salma Kikwete wakiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush
na Mkewe Laura Bush wakiwa jukwaa la viongozi na watu mashuhuri baada
ya Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa
Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela leo Desemba 10,
2013 katika uwanja wa FNB jijini Johannesburg.
PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Desemba 10,
2013, ameungana na viongozi wa mataifa mbali mbali duniani na maelfu ya
wananchi wa Afrika Kusini Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa
kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R
Mandela.
Maelfu kwa maelfu ya wananchi
wamehimili mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa nguvu kwenye Uwanja wa
Michezo wa FNB mjini Johannesburg kumwaga Mzee Mandela ambaye alikuwa
ishara kuu ya upinzani wa siasa za ubaguzi wa rangi za makaburu wa
Afrika Mashariki.(P.T)
Mheshimiwa Mandela ambaye alifariki
duniani Ijumaa iliyopita, Desemba 5, 2013, alikuwa Kamanda wa Jeshi la
Ukombozi la Chama cha African National Congress la Umkhoto we Sizwe
akafungwa jela kwa uhaini kwa miaka 27 na utawala wa Makaburu.
Baada ya kutoka jela mwaka Februari
1990, Mzee Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini ya
mwaka 1994. Lakini Mheshimiwa Mandela alitumikia kipindi kimoja tu cha
miaka mitano na kukataa kutumikia kipindi cha pili.
Kiasi cha viongozi 91 kutoka sehemu
duniani wamehudhuria Kumbukumbu hiyo iliyokuwa na kila aina ya
mchanganyiko wa hisia – wengine wakiwa na majonzi na wengine wakicheza
na kuimba kwa muda wote wa shughuli hiyo iliyochukua kiasi cha jumla ya
saa tano.
Mbali na Rais Kikwete ambaye
amefuatana na Mama Salma Kikwete, marais wengine mashuhuri duniani
waliohudhuria Kumbukumbu hiyo ni Mheshimiwa Barack Obama wa Marekani,
Mheshimiwa Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Uingereza,
Mheshimiwa David Cameroun na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki
Moon.
Kumbukumbu hiyo pia ilihudhuriwa na
viongozi wa zamani wa Marekani wakiwemo marais watatu wa zamani wa
Marekani – Mheshimiwa Jimmy Carter, Mheshimiwa Bill Clinton na
Mheshimiwa George W Bush na mawaziri wakuu wawili wa zamani wa
Uingereza, Mheshimiwa Tony Blair na Mheshimiwa Gordon Brown.
Rais Kikwete kesho, Jumatano, Desemba
11, 2013, ataungana na viongozi wenzake katia katika kutoa heshima za
mwisho na kuuaga rasmi mwili wa Marehemu Mandela ambao utawekwa kwenye
Majengo ya Urais wa Afrika Kusini ya Union Buildings mjini Pretoria.
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment