Ndugu zangu,
Chadema ' Civil War' imepamba moto.
Media imeripoti kuwa leo Chadema Makao Makuu watajibu mapigo. Bado moshi
wa makombora ya Zitto haujatua. Ni juzi Zitto alitoka kwenye handaki na
kajibu mapigo. Na kama ilivyotarajiwa, Chadema nao wametoka kwenye
handaki. Nao wamejipanga kufanya mashambulizi leo. Naam, siasa ni
burudani pia. Kuna wengi watasubiri kwa hamu.(P.T)
Bila shaka, Chadema watakwenda
kuyaonyesha mashimo kwenye utetezi wa Zitto juzi. Watazama sana kwenye
Katiba yao na kuonyesha walivyo makini katika kuifuata.
Ni nini kinachoendelea ?
Tafsiri yangu kiini ni mgogoro wa
uongozi ndani ya Chadema. Ni mgogoro wenye kuiweka Chadema kwenye hatari
ya kugawanyika. Na kama nilivyobainisha juzi, unahusu uongozi na
mamlaka na hususan kuelekea 2015 na mbele zaidi.
Kuna mahali wahusika, kama watataka
kupata - win-win situation, itawabidi wakae meza moja na kukubaliana.
Lakini, inavyoonekana sasa, hakuna mwenye haja ya matokeo ya suluhu. Ni
lazima mmoja apigwe. Na kama nilivyobainisha juzi, kuwa atakayeshindwa,
basi, itakuwa ni mwanzo wa mwisho wake wa kuwepo katika hali aliyo nayo
sasa.
Na nilisema, kuwa ' Vita' hii
itapiganwa kwanza kwenye media. Na baada ya hapo itahamia kwenye
mikutano ya hadhara. Ndio, na tuisubiri ' Kamukunji' .
Maggid Mjengwa.
Iringa.
Iringa.
No comments:
Post a Comment