Na Happiness Katabazi
MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
nchi na mhadhiri mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo(UB),
Dk.Sengondo Adrian Mvungi, saa saba usiku wa kuamkia leo amevamiwa na
watu wasiyojulikana na kumacharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake
ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni
majambazi walikuwa wakimshinikiza awapatie fedha na Dk.Mvungi
alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.
Mtoto mkubwa wa Dk.Mvungi, Dk.Natujwa
Mvungi ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar
es Salaam, saa nane usiku alimthibitishia mwandishi wa habari hizi kuwa
ni kweli baba yake ambaye aliwai kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi ya
Chama cha NCCR-Mageuzi, lakini kura kwa upande wake hazikutosha na
hatimaye aliyekuwa mgombea mwenzie kwa tiketi ya CCM, Dk.Jakaya Mrisho
Kikwete, ndiye aliyeshinda na kutangazwa kuwa ndiye rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania hadi sasa.(P.T)
Dk.Natujwa anasema baada ya watu hao
kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza
katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, na kupatiwa matibabu ya huduma
ya kwanza na kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ambapo alisema
kwanza alipokelewa katika eneo la Emergence na kisha saa kumi na moja
asubuhi aliingizwa kwenye wodi ya Taasisi ya Mifupa Moi kwaajili ya
kuanza kupewa matibabu.
Binafsi habari hizi nimenishtua na
zimeniumiza sana na kujikuta nalia usiku wa manane na ninaiomba serikali
iwasake watu hao na iwafikishe katika vyombo vya sheria. Mara ya mwisho
kuonana na Dk.Mvungi 'Rais Mdhulumiwa' ilikuwa Jumanne iliyopita ambapo
nilienda ofisini kwake saa 12 asubuhi ofisi za Tume ya Mabadiliko ya
Katiba ,ambapo nilikuwa na mdogo wangu Michael Machale ambapo
tulizungumza mambo mengi sana kwa zaidi ya saa tatu.
Sina cha kueleza zaidi ila napenda
kusema kuwa Dk.Mvungi ambaye amekuwa akipenda kuniita jina la utani '
First Lady' kwa sababu kuwa endapo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005
angeshinda nafasi ya urais , mimi ndiye ningekuwa mkewe na mimi hupenda
kumtania kwa kumuita jina la utani 'Rais Mdhurumiwa' kwa maana kuwa
mpinzani wake Rais Kikwete alimuibia kura za kiti cha urais katika
uchaguzi mkuu mwaka 2005, na hivyo kusababisha mimi nisiwe First Lady ni
mtu wangu wa karibu sana na nimiongoni mwa wazee wangu ambao wamekuwa
wakinishauri mambo mengi hasa suala zima la kwenda kusomea kozi ya
sheria na amekuwa akinichukulia kuwa ni mmoja wa watoto wake katika
familia yake.
Itakumbukwa kuwa mimi nilikuwa ni
mwandishi wa habari wa kike peke yangu kati ya waandishi wa habari wanne
wa kiume ambao tulizunguka nchi nzima na Dk.Mvungi katika kampeni za
yeye kusaka urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 2005.
Pole mke wa Dk.Mvungi, Anna, watoto
wake ambao nawaita wanangu Dk.Natujwa, Nakundwa,Mwenyekiti wa NCCR
Mageuzi James Mbatia,NCCR MAgeuzi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa
Costa Mahalu,UB na watu wengine wote ambao ni watu wa karibu wa
Dk.Mvungi.
Nakuombea Dk.Mvungi 'Rais Mdhurumiwa'upone haraka ili urejee tena katika kazi za ujenzi wa Taifa.
source: Mjengwa blog
No comments:
Post a Comment