WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, November 9, 2013

azima mizuka wabunge CCM

 
Rais Jakaya Kikwete, akilihutubia Bunge mjini Dodoma jana. Kulia ni Spika wa Bunge, Anne Makinda. (Picha na Selemani Mpochi)

Hasira ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo ilikuwa ikichemka kiasi cha kuanza kuzusha hofu kuwa wangesusa kujadili marekebisho ya Sheria ya Marekebisho ya Sheia ya Mbadiliko ya Katiba, imeyeyuka baada ya mkutano kati yao na Rais Jakaya Kikwete uliodumu kwa zaidi ya sa tatu juzi mjini Dosoma.
Habari ndani ya wabunge wa CCM zilikuwa zinasema kuwa hasira hiyo ilikuwa imejengwa kwa kuwa Rais Kikwete kwa mara ya pili aliamua kukutana na viongozi wa upinzani Ikulu na kujadili sharia ambayo tayari ilikuwa imekwisha kupitishwa na Bunge, lakini wapinzani wakaisusia, kasha kuirejesha bungeni kwa marekebisho.

Marekebisho ya muswada huo unaotarajiwa kujadiliwa leo bungeni, unalenga kurekebisha sheria ya Marekebisho ya Sheria Mabadiliko ya Katiba Mpya ambayo awali ulipitishwa Septemba 6, mwaka huu na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mmoja wa TLP, huku wabunge wote wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na wale wa Chama cha NCCR-Mageuzi wakisusia na kutoka nje ya Bunge.

 Jana Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alilithibitishia NIPASHE kuwa muswada huo utawasilishwa na kujadiliwa bungeni leo. Aidha, ratiba ya shughuli za Bunge iliyotolewa jana ilionyesha kuwa muswada huo utawasilishwa leo.

Wakati wa kujadili muswada huo, wabunge wa CCM walionyesha walivyochukizwa na ususiaji wa kambi ya upinzani kiasi cha baadhi ya mawaziri, akiwamo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano ya Jamii), Stephen Wasira, kuwakejeli kuwa safari hii hawataitwa Ikulu kunywa juisi na Rais Kikwete.

Baada ya Rais kuwaita viongozi hao Ikulu siku chache baada ya kuaasa kuacha maandamano kupinga sheria hiyo ambayo yalikuwa yametangazwa kufanyika Oktoba 10, mwaka huu, kwa kuwa waliokuwa wanalalamikia yanajadilika, wabunge wa CCM walionyesha kukerwa na hali hii ambayo ilijirudia kama ilivyokuwa wakati wa kupitishwa kwa muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba ya mwaka 2012.

Rais Kikwete akijua hisia za wabunge wa chama chake, juzi usiku alikutana nao usiku kwa muda wa saa 3:10 zikiwa ni juhudi za kujaribu kuzima hasira za wabunge hao dhidi ya hatua yake ya kukutana na wapinzani Ikulu kujadili muswada ambao tayari ulipitishwa nao huku wapinzani wakihususia.

Habari za ndani ya kikao hicho kilichoanza saa 2.00 usiku hadi saa 5:10 usiku, zinasema kuwa Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaeleza yaliyojiri katika mazungumzo kati yake na viongozi wa vyama vya upinzani Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 15, mwaka huu ambao ulikuwa mahususi kusikiliza malalamiko yao juu ya muswada huo ambao ilipitishwa na Bunge lakini upinzani ukiususia.

Muswada huo ambao ulipitishwa bungeni Septemba 6 mwaka huu na Rais kuuridhia Oktoba 10, mwaka huu kwa kuusaini, ulijadiliwa bungeni wakati wa mkutano wa 12 na wabunge wa upinzani waliususia wakilalamika kuwa wadau wa Zanzibar hawakushirikishwa na pia ulikuwa umehodhiwa na CCM.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vilieleza NIPASHE kuwa wabunge walionyesha kutoridhishwa na hatua ya Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kuwaita wapinzani Ikulu kujadiliana nao suala la muswada huo wakati tayari ulikuwa umepitishwa bungeni na wabunge wote wa CCM na mmoja wa Tanzania Labour Party (TLP).

Habari za uhakika zinasema kuwa waliokuwa mstari wa mbele kurusha makombora walikuwa ni Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, Said Nkumba (Sikonge), Kangi Lugola (Mwibala), Naibu Spika, Job Ndugai, Deo Filikunjombe (Ludewa), Pindi Chana (Viti Maalum) na Kangi Lugola (Mwibara).

Vyanzo vyetu vinasema kuwa wabunge hao walisimamia kwenye hoja kuwa Rais anapokutana na wapinzani wakati wamesusia hoja zinazojadiliwa bungeni anawapa nguvu kisiasa na hivyo chama tawala, wabunge na viongozi wake kukosa mvuto wa kisiasa mbele ya jamii.

Habari hizo zinasema kuwa kwa maelezo tofauti, wabunge hao walimshauri Rais Kikwete kwamba anapokutana na viongozi wa upinzani Ikulu wabunge wa CCM nao wawe wanaalikwa ili ajenda husika inayokuwa inajadiliwa yanatolewa maamuzi yenye msimamo mmoja.

Walimweleza Rais kuwa wapinzani ni wajanja sana kwani anapokutana nao Ikulu wakitoka nje wanakuja kueleza tofauti na alivyojadiliana nao na jamii inakuwa inaamini walichokisema ni sahihi na matokeo yake CCM na wabunge wake wanaonekana si lolote.

 “Wabunge walichachamaa wakamwambia Rais unapokuwa unawachukua wapinzani pekee yao kuwapeleka Ikulu wakishamaliza kunywa chai anaponyamaza kimya wao wanabaki kuongea na kuonekana wao wameshinda,” kilisema chanzo chetu kikimnukuu Sendeka.

Wabunge hao pia walihoji Rais kama anaamua kukutana na viongozi wa upinzani wanakuwa viongozi na siyo hata watu wengine wasio viongozi nao wanakwenda Ikulu na kutolea mfano wa mbunge wa Ubungo John Mnyika kuwa hakustahili kwenda Ikulu.

Walimuomba rais abadilishe utaratibu ili akiamua kukutana na wapinzani na viongozi wa CCM au wabunge nao wawepo vingenevyo CCM itajichimbi kaburi kwa wananchi ambao watakuwa wanawaamini zaidi wapinzani kuliko chama tawala.

 “Mangula (Katibu Mkuu wa CC Tanzania Bara) na baadhi ya wengine, pamoja na kushiriki kikao hicho, hawakuwa wabunge na hawakuwa bungeni. Yote  yaliyojiri bungeni ama walisikia kwenye vyombo vya habari au kwa kuambiwa na watu wao,” alisema mmoja wa wabunge hao.

Wabunge hao walisema wanalalamikia hilo, kwa kuwa yawezekana wabunge wa upinzani waliokwenda Ikulu walipotosha ukweli juu ya yaliyojiri bungeni kuhusu muswada huo na hakukuwa na mbunge anayetoka CCM wa kuwasahihisha.

Mmoja wa wabunge hao alinukuliwa akisema: “Hatua ya Rais Kikwete kukutana na sisi kabla ya muswada huo kurudishwa bungeni inaonyesha machale yalimcheza. Kwamba, ameona kama asingetuita na kuzungumza na sisi mapema angerushiwa ‘madongo’ katika kujadili huo muswada bungeni.”

Taarifa zinaeleza kuwa Rais Kikwete alikubali ushauri uliotolewa na wabunge hao na kuahidi kuyafanyia kazi.

Kwa mujibu wa habari hizo, Rais Kikwete, aliwaondoa wasiwasi wabunge hao kuwa uamuzi wake wa kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani Ikulu, jijini Dar es Salaam, haukuwa na nia mbaya.

Aliwaeleza kwamba  lengo la kukutana na viongozi wa vyama hivyo lilikuwa ni kuondoa mkanganyiko uliokuwa umejitokeza kipindi kile kuhusu Muswada wa Sheria ya hiyo na kuweka sawa hali ya utulivu uliokuwa ukielekea kutokweka nchini.

Taarifa za awali ambazo NIPASHE ilizipata ni kwamba hatua ya Rais Kikwete kuamua kukutana na wabunge wa CCM ni kutokana na wabunge huo kutaka kufanya mgomo wa kutoshiriki kwenye mjadala wa muswada huo uliorejeshwa bungeni kutokana na rais kukutana na wapinzani ikulu.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema hatua iliyofikiwa na Rais Kikwete kukutana na wabunge hao amesaidia kukinusuru chama kwani suala hilo lingeiweka CCM katika wakati mgumu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015.

Rais Kikwete alikutana na wapinzania Oktoba15, mwaka huu kujadili suala la Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kukubaliana nao mambo mawili.

Walikubaliana kuwa vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka Serikalini ili itafutwe namna ya kuyashirikisha mapendekezo hayo katika marekebisho ya Sheria hiyo.

Pili, kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano kwa pamoja vitakavyosukuma mbele mchakato huo kwa maslahi mapana ya nchi yao na mustakabali wa taifa.

Aidha, Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kilipewa jukumu la kuratibu jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini.

Viongozi wa vyama vyama vya siasa waliokutana na Rais Kikwete ni Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF; Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.

Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, na Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo aliwakilishwa na Isaac Cheyo; na Nancy Mrikaria ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema. Mrema na Cheyo walidaiwa kuwa nje ya nchi wakti huo.

Wengine ambao walifika Ikulu siku hiyo wakifuatana na wenyeviti wao ni Mbunge wa CUF, Habib  Mnyaa; Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro; wabunge wa Chadema Tundu Lissu na John Mnyika; na Martin Mng'ongo wa NCCR-Mageuzi.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment