Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amemtetea
Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Shariff Hamad, kwamba hajakiuka
taratibu za kuendesha serikali ya umoja wa kitaifa kwa kutoa kauli
ambazo zinapingana na msimamo wa serikali hiyo.
Akizungumza na vyombo vya habari Ikulu mjini hapa jana, Dk. Shein alisema, Maalim Seif hakuwahi kutoa kauli ambazo zinahusu msimamo wa serikali kuhusiana na mambo mbalimbali na kwamba kama ametoa kauli ni maoni yake binafsi ama ya chama chake. Dk. Shein alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa swali kwamba inakuwaje Maalim Seif anatoa kauli tofauti na msimamo wa serikali hususani mfumo wa Muungano kwa kusema kwamba uwe wa mkataba.
Dk. Shein alisema kuwa kila mwananchi ana haki kikatiba kufanya jambo analolitaka ukiwamo uhuru wa kutoa maoni.
“Kama Makamu wa Kwanza wa Rais anayo maoni yake kuhusu muundo wa Muungano, ni maoni yake au ya chama chake. Lakini siyo msimamo wa serikali, isitoshe msemaji wa serikali ni mimi labda atoe msimamo wa serikali kwa maelekezo yangu.”
Aliongeza: “Waziri yeyote wa Serikali ya ya Mapinduzi Zanzibar hawezi kuisemea serikali juu ya katiba. Mimi sijamsikia (Maalim Seif) anazungumza hivyo kwa niana ya serikali.”
Hata hivyo, Dk. Shein alisema kuwa mawaziri wote wanaounda serikali hiyo wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kwamba hawajawahi kuvutana.
“Tunajadili maslahi ya watu wetu, ukija katika vikao vya Baraza la Mawaziri huwezi kujua nani anatoka chama gani. La msingi ni kuvumiiana na kila mmoja kufuata katiba,” alisema. Rais Shein alisema kuwa amefanikiwa kuiongoza serikaliya umoja wa kitaifa kwa mafanikio ingawa alisema kuna wanachama wa CCM ambao wakati inaundwa walimuuliza kama ataweza kuiongoza.
Alipoulizwa kuhusu kutofautiana kwa kauli kati Waziri wa katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakari na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, kuhusu mchakati wa Katiba Mpya baada ya Bakari kusema kuwa Zanzibar haikushirikishwa na Balozi Iddi kusema ilishirikishwa, Dk. Shein hakuwa tayari kujibu akisema kuwa suala hilo limemalizika.
Dk. Shein aliwashukuru Maalim Seid na Balozi Iddi kwa jitihada na kazi zao kubwa walizofanya katika kipindi cha miaka mitatu kumsaidia kuiongoza Zanzibar. “Umahiri wao na uadilifu wao umesaidia sana katika kuwatumikia wananchi,” alisema.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment