Na Mahmoud Zubeiry, Dar es
Salaam
YANGA SC imepanda
kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-0
dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Azam FC
ikitoka sare ya 3-3 na Mbeya City, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo
ya Jiji la Dar es Salaam.
Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, mabao ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva dakika 23, Mrisho
Ngassa dakika ya 23 na Jerry Tegete dakika ya 53.
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, hadi mapumziko, timu
hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Azam wakitangulia kupata bao kupitia
kwa Humphrey Mieno dakika ya 13 na Mbeya City wakasawazisha kupitia kwa Mwagane
Yeya 'Morgan' dakika ya 30.
Ngassa ameifungia
Yanga Taifa leo
Mabao yote
yalitokana na mipira ya pembeni, Mieno akifunga kwa kuunganisha kwa kichwa mpira
wa adhabu uliopigwa na Farid Mussa nje kidogo ya 18, kufuatia kipa David Burhan
kudakia nje ya eneo lake na Mwagane aiunganisha krosi ya Deus
Kaseke.(P.T)
Kipindi cha pili, Mbeya City walitangulia kupata bao dakika ya 52 Mwagane Yeya tena akiunganisha kwa kichwa krosi ya Steven Mazanda, lakini John Bocco 'Adebayor' akaisawazishia Azam dakika ya 60 akiunganisha krosi ya Kipre Tchetche.
Mwagane tena akaifungia Mbeya
City kwa shuti kali dakika ya 73 baada ya pasi ya Mazanda, lakini Khamis Mcha
'Vialli' aliyetokea benchi aliisawazishia Azam dakika ya 83, dakika tatu tu
tangu aingie kuchukua nafasi ya Farid Mussa.
Kwa matokeo hayo, Yanga inamaliza mzunguko wa kwanza
ikiwa na pointi 28 na kupaa kileleni, wakati Azam inashuka nafasi ya pili kwa
pointi zake 27 sawa na Mbeya City, lakini inabebwa kwa wastani mzuri wa mabao ya
kufunga na kufungwa.
Azam; Mwadini Ally,
Erasto Nyoni, Waziri Salum, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Salum
Abubakar, Kipre Tchetche, John Bocco/Joseph Kimwaga 72, Humphrey Mieno na Farid
Mussa/Khamis Mcha dk80.
Mbeya City; David Burhan, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Yussuf Abdallah, Anthony Matogolo, Mwagane Yeya, Steven Mazanda/Alex Sethi dk90, Paul Nonga/Francis Castor, Deus Kaseke na Richard Peter/Peter Mapunda dk46.
Mbeya City; David Burhan, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Yussuf Abdallah, Anthony Matogolo, Mwagane Yeya, Steven Mazanda/Alex Sethi dk90, Paul Nonga/Francis Castor, Deus Kaseke na Richard Peter/Peter Mapunda dk46.
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment