Leo tunaposubiri majina ya watanzania watakao tuwakilisha katika bunge la Katiba mpya 2014 hebu tujikumbushe tumefikaje hapa kwa ufupi?
BUSARA ALIYOIONYESHA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE YA
KUANZA KUKUTANA NA VYAMA VYA UPINZANI KUJADILI MCHAKATO WA KATIBA MPYA
TUMEzIPOKEA KWA FURAHA KUBWA;
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 29, 2011, alitia saini
Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011. Hatua hiyo ya
Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha
Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita cha Bunge.
Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010.”

Kama taifa inatupasa
kukumbuka kuwa mabadiliko ya katiba ni
madai ya msingi na matakwa ya lazima kama nchi yetu kama inataka kujenga na
kudumisha
amani ya kweli na kuleta maendeleo kwa watu wake; wazo la serikali na
vyama vya
siasa na asasi zingine zinazojishughulisha kudai na kuhamasisha mabadiliko haya ya msingi
kuendelea kutambuka kuwa Safari hii ya utungaji wa katiba ni ya Muhimu
sana.
Kutokana na umuhimu huu mkubwa kwa faida ya Taifa,hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kuwa wananchi wanapata nafasi ya kujua zaidi kuhusu mapungufu ya katiba ya sasa na nini kitarajiwe katika katiba mpya. Wananchi wapate nafasi ya kwanza katika kutoa mawazo ya nini wanataka wakati tume ya kukusanya maoni itakapowatembelea. Lakini kama watapuuzwa tutajenga ufa mwingine katika katiba mpya.
Je vyama vya siasa na asasi zake kwa sasa hivi zimeandaa mikakati gani ya kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia maoni?
Tatizo nilionalo mimi kama vyama vya siasa vitaendelea kulumbana vyenyewe vifahamu kuwa havina nafasi ya kumsaidia mwananchi wa katika kujinasua katika hali duni kwani katiba na utungaji wake vitabaki kuendelea kumilikiwa na wanasiasa na wasomi na wanjanja wachache.

Tukiangalia wenzetu kama
Marekani pamoja na uwezo wao na maendeleo yao bado Katiba ni chombo cha
wananchi na sio chombo cha chama Fulani, na katiba yao imejengwa katika
msingi mkubwa sana wa uhuru ambao umewekwa katika katiba yao. Ikiongozwa na maneno haya " We The People"
Jukumu
la wanasiasa
kuwaelimisha wananchi kuhusu marekebesho ya
kutungwa kwa katiba mpya ni la muhimu sana kwani wananchi wengi hawajui
katiba ya zamani ina
matatizo gani, hivyo wasipoelimishwa hata mabadiliko yanayokusudiwa
hayatakuwa
na msisimko wowote kwao na katiba mpya haitakuwa na maana yeyote kwao.
Kwa serikali vyama vya upinzani na Asasi zinazojihusiha na maswala ya katiba,
tunaviomba sana katika mchakato huu mzima wa uandikaji wa katiba mpya vitumie nafasi hii vizuri kwa kujadiliana juu
ya Katiba mpya, kwa kudumisha utamaduni wa kuvumilia pamoja na tofauti zao za vyama na mtazamo. itafurahisha sana kama wahusika wote watakuwa na mtazamo chanya na kutanguliza taswira nzuri ya Taifa kwa
masilaha ya wananchi wote bila kubagua.
Nakumbuka Profesa Shivji katika moja ya mikutano ya
changamoto ya katiba mpya ya Tanzania aliwahi sema kuwa “mchakato wa upatikanaji wa kabisa mpya ni
fursa muhimu ya kurejesha mwafaka kwa majadiliano kuliko ilivyo sasa ambako
kuna kila dalili za kuelekea katika magomvi na mapambano”
Kwa maneno mengine
Professor Shivji anatukumbusha kuwa
Katiba inatakiwa iwe ni mali ya wananchi, ndio
wananchi lazima wawe wenye uamuzi wa aina ya serikali wanayotaka
kuwa nayo na na namna itakavyo waongoza, wananchi ndio msingi wa madaraka yote nchini. Kwa
maneno mengine Katiba inatakiwa itoke kwa wananchi. Siyo katika kuipigia kura
tu bali katika uandikaji wake. Katiba ambayo haitoki kwa wananchi na haiweki
ushiriki wa juu kabisa wa wananchi kutoka mwanzo haiwezi kudai kuwa ni katiba
ya wananchi hao.
Kwa mtazamo wangu na wengine wengi ambao sio
wanansiasa au wasomi tunatamani kuwa Katiba
Mpya iwe ni kumbu kumbu endelevu na kwamba, kasoro zilizojitokeza kiasi cha
kutibua morari na hali ya watanzania, iwe ni changamoto ya kuwa makini zaidi
katika mchakato mzima wa uandikaji wa Katiba Mpya, mzaha wowote unaweza
kulitumbukiza Taifa katika maafa makubwa lazima usipewe nafasi kwani tunatamani
katiba yetu iwe kama ile ya Merakani ambayo imesimama imara na inatekelezeka.
Kama Mwalimu Nyerere
alivyowahi sema katika moja ya mikutano yake kuwa Katiba ni sheria mama, iguse msingi wa mambo
makuu yatakayoongoza sheria, sera na mifumo ya kitaifa. Hii ni dhamana nyeti
inayopaswa kuwashirikisha wataalam kutoka katika medani mbali mbali za maisha
ya wananchi nchini Tanzania.
Wanasiasa waepuke vishawishi na kudhani kwamba, wao ndio wanaopaswa kusimamia na kuongoza mchakato huu, wajitahidi kushiriki kama watanzania wengine kwa kuchangia mawazo yao na sio kuhozi katiba mpya kama mali ya chama chao.

Katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba tuzingatie,
- Katiba Mpya inapaswa kuwa ni mali ya watanzania wote kwa kuwa mchakato mzima unawashirikisha watanzania wengi zaidi kwa njia ya moja kwa moja au uwakilishi wao. Chombo kitakachopewa dhamana ya kusimamia kuandika Katiba Mpya, kwanza kabisa kikubalike na watanzania wengie, hii itakuwa ni hatua kubwa hata kuweza kuridhia kile kitakachoandikwa. Miongozo itolewe katika lugha inayoeleweka na fasaha ili kuwa na tafsiri sahihi na rahisi kwa watanzania wa kawaida kabisa
· Washauri wa mheshimiwa Rais tunawaomba
wamshauri Rais wetu kwa kujali zaidi masilahi ya Taifa na sio vinginevyo
wakizingatia kuwa serikali yetu kwa hivi sasa inaingia katika kipindi muhimu
sana cha kulipitisha Taifa letu katika wakati huu kwa maendeleo ya wananchi
wote na sio kikundi kidogo cha watu;
· Katiba yetu ikamilishwe kutungwa kwa
majadiliano na makubaliano ya umoja wa kitaifa na sio kwa vitisho vya Migomo na
maandamano na shinikizo la vyama kwa masilahi binafsi.
· ili kupata Katiba makini inayozingatia
mafao ya wengi kuna haja kwanza kabisa kuwa na utulivu wa kimawazo, busara na
hekima vitumike zaidi, kwa kuzingatia umoja wa kitaifa na upendo kati ya watu.
Masilahi ya taifa yapewe kipaumbele cha kwanza na kamwe ubinafsi usiruhusiwe
kutawala zoezi nyeti kama hili.
·
Ebu tuache malumbano wakati huu ni mzuri kwa vyama vya
siasa tanaznia pamoja asasi zanazojishughulisha
na mambo ya sheria kutumia muda huu kuwafundisha
wananchi katiba ya zamani na waone hayo mapungufu
yake halafu wapate kutoa maoni yanayolingana
na mahitaji yao na sio kufuata mkumbu wa mahitaji ya wanasiasa kama
inavyoendeleahivi sasa;
HITIMISHO;
Kwa msingi huu vyama vyote
yaani CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, TLP na
Vyama vingine vya siasa vikumbuke kuwa “Katiba ya nchi si mali ya chama au mtu
binafsi na wala si mali ya kiongozi fulani, ni mali ya watu wote raia wa
Tanzania na wala katiba isipatikane kwa shinikizo la kukundi chochote cha watu”
kama Dk Salim Ahamed
Salim aliwahi sema kuwa “Chama tawala na chama kikuu cha upinzani
vijue tunaangalia mustakhabali wa taifa letu, lazima uelewano uwepo malumbano
si mazuri japokuwa ni sehemu ya siasa, lakini akaonya kwamba yasiruhusiwe
yakasababisha nchi ikafika pabaya.
Ninachoomba chama tawala na Chadema wafikirie mwafaka na kuangalia mustakhabali wa taifa, kama hakuna maafikiano si jambo zuri kwa taifaKwa hali ya kisiasa hivi sasa ni lazima mjadala uwe wa nia njema lengo ni kuendeleza makubaliano na si kuhitilafiana. Tujenge na kuimarisha undugu na mishikamano wetu na kuonyesha uzalendo na uongozi madhubuti wa taifa letu,”

kwa
hiyo tunavyoelekea
kupata katiba mpyaa ifikapo mwaka 2015 kama serikali ilivyohaidi,
Tanzania kama
nchi ambayo imeingia katika mfumo wa vyama vingi miaka ya 90, inahitaji
mabadiliko au katiba mpya yenye misingi YA UPANA NA UWAZI WA DEMOKRASIA
na
misingi mipya ya kuongoza vyama vingi na mawazo mapya ya Jamii kwa
msingi huu
kama sisi kama Taifa tutafanikiwa kupata katiba mpya basi tukakuwa
tumejijengea katiba iwapo vile vile tutaweza kujumuisha kwenye
uandikaji wa katiba mpya kwa maoni ya wananchi hapo tutakuwa
tumejijengea Utawala wa Demokrasia ya umma.
Tunaendelea kumpongeza
mheshimiwa Rais kwa busara yake ya kuanza kukutana na vyama vya upinzani
CHADEMA, katika kufikia muafaka na kushauriana katika kuboresha uandikaji wa
katiba mpya; tunamwomba mheshimiwa Rais aendelee kukutana na wale wote wenye
nia njema, katika kuboresha katiba yetu mpya;
No comments:
Post a Comment