Nyamazeni; Tambwe akishangilia bao lake la pili leo
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
SIMBA SC imefufua matumaini ya ubingwa, baada ya leo kuifunga JKT Oljoro ya Arusha mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Simba SC itemize pointi 30 baada ya kucheza mechi 15, ikiwa nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City pointi 31, Yanga SC pointi 32 na Azam FC pointi 33 kileleni.
Hadi mapumziko tayari Wekundu wa Msimbazi walikuwa mbele kwa mabao 3-0, matatu akifunga Mrundi Amisi Tambwe na moja kiungo mzalendo, Jonas Mkude.

Mabao
yote hayo yalitokana na pasi na kiungo machachari wa pembeni wa timu
hiyo, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ ambaye kwa hakika alikuwa mwiba
kwa safu ya ulinzi ya timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa.
Jonas Mkude alifunga kwa shuti kali la
umbali wa mita 20 baada ya kuletewa kwenye himaya yake moja kwa moja
mpira wa kona uliopigwa na Messi.
Wachezaji wa Oljoro walijazana kwenye lango lao kumlinda kipa wao Mohamed Ali, lakini Messi akautoa nje kabisa mpira alipokuwa Mkude, ambaye aliunganisha moja kwa moja kwa shuti kali.
Wachezaji wa Oljoro walijazana kwenye lango lao kumlinda kipa wao Mohamed Ali, lakini Messi akautoa nje kabisa mpira alipokuwa Mkude, ambaye aliunganisha moja kwa moja kwa shuti kali.
La kwanza; Jonas Mkude kulia akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza Tambwe akipongezwa na Awadh Juma kulia na Donald Mosoti kushoto Haroun Chanongo akimuacha chini beki wa JKT Oljoro
Tambwe alifunga bao lake la kwanza leo
na la pili kwa Simba SC dakika ya 22 akiunganisha krosi nzuri ya Messi
wakati la tatu, alifunga dakika ya 28 baada ya kupata pasi ya
kutanguliziwa kutoka kwa winga huyo machachari anayetumia vyema mguu
wake wa kushoto.
Kipindi cha pili, Simba SC walirudi na moto wao na kufanikiwa kupata bao la nne dakika ya 52 mfungaji Tambwe tena, safari hii akiunganisha krosi ya Awadh Juma.
Baada ya mabao hayo manne, kocha Mcroatia akawapumzisha wachezaji wake nyota Messi, Amri Kiemba na Tambwe na kuingiza wachezaji wa kwenda kuulinda ushindi huo.

Kikosi
cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, William Lucian ‘Gallas’, Issa
Rashid ‘Baba Ubaya’, Donald Mosoti, Joseph Owino, Jonas Mkude, Haroun
Chanongo, Awadh Juma, Amri Kiemba/Uhuru Suleiman dk64, Amisi
Tambwe/Abdulhalim Humud na Ramadhani Singano ‘Messi’/Said Ndemla dk55.
JKT
Oljoro; Mohamed Ali, Paul Malipesa, Ali, Omar, Nurdin Mohamed, Sabri
Makame, Babu Ally, Jacob Masawe, Amir Omar, Shijja Mkina na Majaliwa
Mbaga/Shaibu Nayopa dk38.
chanzo: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment