CHADEMA YAPIGWA CHINI,
KATIKA VITUO TISA VILIVYOPIGIWA KURA, CCM IMESHINDA VITUO NANE WAKATI
CHADEMA WAKIPATA KIMOJA TU KATIKA KATA YA NDULI KWENYE MANISPAA YA
IRINGA.
Baadhi ya wanachama wa chama cha
mapinduzi katika kata ya nduli kwenye manispaa ya Iringa wakiserebuka na
kuimba kwa furaha baada ya kupata taarifa ya ushindi wa chama cha
mapinduzi katika ngazi ya udiwani, uchaguzi huo ulifanyika jana, siku ya
jumaapili ya tarehe 9/2/2014 ambapo Bw. Bashiri Richard Mtove aliibuka
mshindi na kumpiku mpinzani wake kutoka chama cha demokrasia na
maendeleo Bw. Ayubu Abdalah Mwenda katika ngazi hiyo ya udiwani
Bw. Bashiri Richard Mtove akiwashukuru
wanachama wake wa CCM waliomuwezesha kuibuka na ushindi katika kampeni
hizo ziliofanyika katika kata ya nduli, jumla ya vituo vya kupigia kura
vilikuwa tisa lakini CCM ilishinda katika vituo nane na kupoteza kimoja
tu ambacho kilishikiliwa na CHADEMA; kituo cha Mibata ndicho
kilichoongozwa na CHADEMA kwa jumla ya kura 103 wakati CCM ikipata kura
48 lakini katika vituo vingine vyote CCM walishinda kwa kishindo kikubwa
na hata kuweza kunyakua nafasi hiyo dhidi ya wapinzani wao wakuu
CHADEMA.
baadhi ya wanachama wa CCM wakiwa
katika shangwe na vifijo baada ya kupata taarifa ya ushindi dhidi ya
CHADEMA, hili ni eneo la kituo cha mabasi ya kubeba abiria katika kata
ya Nduli.
mwanachama mmoja wa CCM akitoa pongezi
zake za dhati kwa Bw. Bashiri Richard Mtove aliyeibuka na ushindi wa
udiwani katika kata ya Nduli; wanachama wa chama cha mapinduzi walijawa
na furaha isiyo kifani na hata kupiga mayowe huku wakiwaimba wanachama
wa CHADEMA kwa kushindwa kuipata nafasi hiyo ya udiwani wa kata hiyo.
katibu wa CCM katika manispaa ya
Iringa Bw. Hassan Mtenga akitoa shukhrani zake kwa wanachama
waliojitolea kumpigia kura Bw. Mtove aliyekuwa anaiwakilisha CCM katika
ngazi ya udiwani
baadhi ya watu waliokuwa wanaelekea
katika kituo cha Godown ambapo ndipo ilikuwa sehemu kuu wanapotolea
matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo wa diwani wa Nduli
baadhi ya wanachama wa CHADEMA
waliokuwa karibu na eneo hilo wakiondoka na kutokomea sehemu nyingine.
wanachama hao wa CHADEMA hawakuonekana tena katika eneo hilo.
jeshi la polisi lililotakiwa kutuliza
amani na utulivu lilifanya kazi yake kama ilivyo takiwa na hakukuwa na
ugomvi wowote ule kwa kuwa hali ya ulinzi ilikuwa katika kiwango cha juu
furaha ilipitiliza mpaka wengine
wakachoka na kuishia kukaa chini kwani waliimba na kucheza sana baada ya
mwanachama wao kushinda nafasi hiyo ya udiwani
baadhi ya wanachama waliokuwa wakielekea katika kituo cha Godown ambapo matokeo yote yalikuwa yakitolewa kwa ujumla
kila mtu alishangilia kwa staili yake
kwani ilikuwa ni furaha iliyopitiliza na kila mtu alicheza na kuimba kwa
sauti; watu wa rika zote walikwepo kuanzia watoto mpaka watu wazima
mitaa ya kituo cha mabasi ya abiria
palikuwa ni kucheza tu kwani watu walijaa na kusherekea kwa furaha isiyo
kifani kutokana na ushindi wa CCM
mueshimiwa diwani alipobebwa na kundi
ka wanachama wa CCM waliokuwa na furaha na hata kujidai kwa jitihada za
chama chao; hivyo basi chama cha mapinduzi CCM ndicho kilichoibuka na
ushindi kupitia mgombea wake Bw. Bashiri Abdalah Mtove.
imeandikwa na Riziki Mashaka.
SOURCE: MJENGWA BLOG
No comments:
Post a Comment