Young Africans imetoka sare ya bao 1-1
dhidi ya wenyeji timu ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine
jijini Mbeya.
Young Africans wakati wakiingia
uwanjani washabiki wa Mbeya City walilirushia mawe na chupa za bia bus
la wachezaji hali iliyopelekea kuvunja kioo cha upande wa kulia mwa
dereva na kumjeruhi dereva Maulid Kiula aliyekua akiliendesha gari hilo.
Mara baada ya tukio hilo viongozi wa
timu ya Yanga walichukua jukumu la kuwatuliza wachezaji na kuendelea
kuwapa morali ambapo walituliza munkari wa kujeruhiwa na kuingia ndani
kujiandaa na mchezo wenyewe.
Dakika za mwanzo Said Bahanuzi na
Didier walishindwa kuzitumia nafasi za wazi na kiujumla hali ya mchezo
ilikua sawa kwa timu zote huku washabiki wakikosa radha ya mchezo
kutokana na ubovu wa uwanja.
Mbeya City walifanya mashambulizi
langoni mwa timu ya Yanga lakini umakini wa walinzi na mlinda mlango
Ally Mustapha 'Barthez' ulikuwa kikwazo kwa washambuliaji hao kuziona
nyavu za watoto wa Jangwani.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Mbeya City 0 - 0 Young Africans.
Kipindi cha pili kilianza kwa wenyeji
kufanya shambulizi langoni wa timu ya Yanga na dakika ya 46 ya mchezo
waliweza kujipatia bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji Paul Nonga kwa
kichwa aliyeukwamisha mpira wavuni kwa kichwa.
Kocha wa Yanga alifanya mabadiliko ya
kuwaingiza Jerson Tegete na Oscar Joshua waliongia kuchukua nafasi za
Said Bahanuzi na Nizar Khalfani ambao waliongeza nguvu na kubadili hali
ya mchezo.
Dakika ya 60 Didier Kavumbagu
aliipiatia Yanga bao la kusawazisha kufuatia golikipa wa Mbeya City
kuuchezea mpira na Didier kuukwamisha wavuni lakini katika haliya ajabu
mwamuzi alilikataa bao hilo.
Didier Kavumbagu aliipatia Young
Africans bao la kusawazisha dakika ya 71 kwa kifua akimalizia mpira
uliopigwa na mlinzi Mbuyu Twite na kumkuta mfungaji aliyeukwamisha
wavuni bila ajizi.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Young Africans 1 - 1 Mbeya City
Mara baada ya mchezo wakati timu
ikielekea hotelini washabiki wa timu ya Mbeya City wameendelea
kuzirushia mawe gari zilizokuwa katika msafara huo ambapo wamevunja vioo
vya bus kubwa tena na gari ndogo kioo cha nyuma chote.
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment