Ndugu zangu,
Imeripotiwa kwenye gazeti la
Mwananchi, leo Ijumaa Septemba 20,kuwa Waziri wa Sheria na Katiba,
Mheshimiwa Chikawe, amemwomba Rais Kikwete asaini Muswaada wa
Marekebisho ya sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa na Bunge
Septemba 6, mwaka huu. Kwamba Rais afanye hivyo ili kuepuka vurugu.
Hakika, huu ni wakati wa kuongozwa
zaidi na hekima na busara kuliko hisia na ushabiki na hususan wenye sura
za vyama na kuangalia maslahi ya muda mfupi na ya kibinafsi zaidi.
Rais wa Nchi anaongoza watu, na si
mawe. Msingi wa kukubalika kisiasa ni lazima utokane na kukubalika na
watu. Na wapinzani hao pia nyuma yao si mawe yaliyojipanga. Ni watu.
Hivyo basi, inahusu watu. Inahusu Wananchi. Katiba ni mkataba baina ya
watu katika jamii. Si miti na mawe.
Hivyo, ni muhimu sana watu kwa maana
ya wananchi wakasikilizwa. Kama kuna manung'uniko yatafutiwe majawabu
ili tufike salama kwenye kulifikia lengo kuu; Katiba ya Wananchi. Si ya
chama tawala wala vyama vya upinzani. Ni jambo litakalotupeleka hata
miaka 100 ijayo.
Maisha yetu hapa duniani ni mafupi
sana. Wengi wetu hatutakuwepo, hata pale nchi yetu itakapotimiza miaka
100 ya Uhuru. Desemba 9, 2061.
Na Waziri Chikawe asiwe na hofu.
Watanzania kwa desturi si wapenda vurugu. Hata katika hili la Katiba
hawatafanya vurugu. Ila wakipewa nafasi ya kuonyesha masikitiko yao,
basi, watayaonyesha, bila kufanya vurugu.
Maggid.
Iringa.
0754 678 252
Iringa.
0754 678 252
Comments!
Nelson Msita Mie
huwa najiuliza hivi hawa mawaziri wa chama tawala..huwa wanajiongoza
kwa akili zao au kwa akili za chama.!?na kama ni kwa akilo za chama je
chama kimetoa wapi akili hizo..:?
22 minutes ago via mobile · Like
Mtanzania Kihange Ni vyema Busara ikitumika na sio mitazamo ya watu binafsi
20 minutes ago via mobile · Like
Muhidin Thabeet Kiss Bado Naendelea Kuamini Matatizo Mengi Yanayoikumba Nchi Yetu Yanatokana na Kukosa Busara na Hekma Kwa Viongozi Wetu.
19 minutes ago · Like
Rashid Katakwa ni
vizuri tukakumbuka ya kwamba ktk serikali ya rais jk,hakuna hata
kiongozi mmoja aliyekuwa na wazo la katiba hata chama chake hakikuwa na
ajenda ya katiba,ni busara za rais jk za kuazisha mchakato wa katiba,kwa
busara hizo hizo naamini atatuvusha salama hao kina chikawe na wenzake
hawajui watendalo!
10 minutes ago · Edited · Like
Mtumishi Stanley Mngoni Rashid unasema ni busara za JK kuanzisha mchakato wa katiba una uhakika na kauli yako?
8 minutes ago · Like
Rashid Katakwa ndio!kwani ilikuwa ktk ilani ya chama chake?
7 minutes ago · Like
Rashid Katakwa katiba
haikuwa ktk ilani ya ccm!karibia vyama vyote vya upinzani walitaka
katiba mpya!shinikizo toka kwa vyama pamoja na asasi za kiraia kupiga
kelele ndio maana jk akatumia busara kusikiliza kelele za wengi!ni
busara tu ndugu yangu au ww busara unaitafsiri vp?@mngoni
No comments:
Post a Comment