- Nape asema wazungu wanafadhili vurugu za CHADEMA
NI dhahiri, matukio ya kisiasa
yanayokwenda kinyume cha utamaduni mkongwe wa Watanzania yamezidi kuzusha
wasiwasi miongoni mwa raia nchini, kuhusu mwelekeo hasa wa nchi, angalau baada
ya miaka mitano ijayo, Raia Mwema, imeelezwa.
Kati ya vurugu za hivi karibuni kabisa
ni katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kikao kilichokuwa na
majukumu ya kujadili, kupitisha au kukataa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba, uliowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias
Chikawe.
Hata hivyo, mbali na vurugu hizo za
karibuni zinazozidi kuchepusha mweleko mzuri wa harakati za kisiasa uliokuwapo
kwa miongo kadhaa sasa, yamekuwapo matukio mengine kadhaa ya vurugu zisizo za
kistaarabu katika kuendesha siasa za nchi hasa mara baada ya kufanyika kwa
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Mlolongo wa matukio
Katika tukio hilo la Septemba 6, mwaka
2013 Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aligoma kutii
maelekezo ya Naibu Spika, Job Ndugai ambaye ndiye aliyekuwa akiongoza kikao
hicho na kutokana na kugoma huko, Ndugai baada ya kumsihi Mbowe mara tatu aketi
naye kugoma, aliamuru askari wa Bunge kumtoa nje ya ukumbi wa kikao lakini
Mbowe aligoma huku wabunge wenzake wa upinzani wakizuia askari hao kumtoa nje.
Katika purukushani hiyo, Mbunge wa
Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbai na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi, pamoja na wengine baadhi, ndiyo waliokuwa mstari wa mbele kuzuia
Mbowe asitolewe na askari ndani ya ukumbi wa Bunge na nguvu zaidi zilitumika
kumtoa Mbilinyi kwa kumbeba.
Hoja mbalimbali za utetezi wa pande
zote mbili ziliibuliwa dhidi ya tukio hilo, upande wa CHADEMA wakidai ni kwa
nini Naibu Spika hakumpa nafasi ya kuzungumza Mbowe na kama angefanya hivyo
hakuna vurugu zozote ambazo zingetokea lakini upande wa wanaomtetea Naibu Spika
Ndugai, wanasema Mbowe alipaswa kwanza kutii mamlaka ya kiti kwa kuketi na
zaidi ya hapo, aliingilia haki ya Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema,
ambaye tayari aliruhusiwa na Ndugai kuchangia hoja iliyokuwa mbele ya Bunge.
Na pande zote hizo katika utetezi wao
wanarejea kanuni za Bunge, upande wa Mbowe ukisisitiza kiongozi wao ambaye
ndiye Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni alipaswa kusikilizwa na
inapaswa kuwa hivyo kila anaposimama bungeni lakini upande wa Naibu Spika,
akiwamo spika wa zamani, Mzee Pius Msekwa akisema; “Ndugai (Spika) ndiye
anayeamua nani aseme, ndiye mwenye mamlaka hayo na ni jambo la kawaida,” na
kusisitiza vurugu hizo zimetokana na hisia za ujana zaidi.
Mbali na tukio hilo, matukio mengine
yanayoashiria kuyumba kwa mwenendo wa uendeshaji wa siasa nchini ni pamoja na
kuwahi kushambuliwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA, katika maandamano ya
Januari 5, mwaka 2011, mkoani Arusha na watu watatu kuuawa ikielezwa kuwa
walikuwa wakielekea kuvamia Kituo Kikuu cha Polisi mkoani Arusha. Katika tukio
hilo, wabunge kadhaa walijeruhiwa, sambamba na viongozi wengine wa CHADEMA.
Tukio jingine la kushtua ni la
kulipuliwa kwa bomu katika mkutano wa CHADEMA wa kufunga kampeni za udiwani wa
kata nne jijini Arusha, la Juni 6, mwaka huu viwanja vya Soweto pia kuchinjwa
kwa mmoja wa viongozi wa CHADEMA katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Msafiri
Mbwambo, katika uchaguzi mdogo wa ubunge, Aprili mwaka 2012.
Pamoja na hayo, tukio la mwaka 2012, la
kuuawa kwa mwanahabari Daudi Mwangosi aliyekuwa katika shughuli za kisiasa za
CHADEMA mkoani Iringa, ambako alikwenda kuripoti mwenendo wa shughuli hizo kwa
ajili ya kituo chake cha televisheni, Channel Ten. Wabunge wa CHADEMA, Highness
Kiwia wa Ilemela na Salvatory Machemli wa Ukerewe, wote kutoka jijini Mwanza
nao walishambuliwa katika harakati za kisiasa mwaka 2012, mjini Mwanza.
Lakini kwa upande wa CCM, kada wao
Mussa Tesha alimwagiwa tindikali wakati akibandika mabango ya kampeni za
aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM, Dk. Dalali Kafumu ambaye alishinda uchaguzi
mdogo wa ubunge jimboni Igunga.
Na kwa upande wa serikali, aliyekuwa
Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, alidhalilishwa na baadhi ya viongozi
wa CHADEMA akiwamo Mbunge, Sylvester Kasulumbai na Mbunge wa Vitimaalumu, Susan
Kiwanga ambao walipata kushitakiwa katika Mahakama mkoani Tabora kwa kosa hilo
la wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga uliotokana na kujiuzulu ubunge
kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Rostam Azizi.
Tukio jingine la Februari 5, mwaka huu,
linalowahusisha baadhi ya viongozi wa CCM, akiwamo Mbunge wa Tabora Mjini
Ismail Aden Rage, ambaye alijikuta katika ugomvi wa kugombea mlingoti wa
kupachikia bendera, kati yake na wenzake dhidi ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA
mkoani Dodoma. Katika tukio hilo, viongozi hao walipigana, wakifukuzana wakiwa
na mawe mkononi kwa ajili ya kujeruhiana.
Dk. Slaa: Ni ishara mbaya kwa utawala
Akizungumzia matukio
hayo na mengine ambayo hayajawekwa katika habari hii kutokana na nafasi ndogo
gazetini, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa, ambaye bado ana ushawishi
mkubwa katika siasa za Tanzania anasema, matukio hayo ambayo mengi yanahusu
kunyanyaswa kisiasa kwa CHADEMA, ni dalili za kuanguka kwa utawala wa sasa
chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM.).
Dk. Slaa anasema; “Ukitazama hali ya
matukio ya kisiasa ambayo yanathibitisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu,
kuna mambo makubwa mawili yanayojitokeza.
Kwanza, ni serikali pamoja na chama
tawala kuhamaki...wame-panic na ndiyo maana unaona wanaelekeza CHADEMA
kifanyiwe vurugu katika shughuli zake za kisiasa. Licha ya kwamba Mwenyekiti
wao (Rais Jakaya Kikwete) kuwaambia wasitegemee nguvu za polisi katika kuendesha
shughuli zao za siasa lakini wameshindwa kuheshimu agizo hilo.
“Pili, matukio haya yanayofanywa na
chama tawala na serikali dhidi ya uendeshaji siasa wa CHADEMA ni viashiria
vinavyojitosheleza kwamba ni anguko la utawala wao. Duniani popote, ishara ya
kuanguka utawala wowote ni kuwapo kwa matukio kama haya tunayoshuhudia sasa.
Kwa upande wetu hatutakata tamaa na mapambano ya kudai haki yataendelea.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kuna ushahidi
mkubwa unaothibitishwa na ripoti za serikali yenyewe ikiwamo ripoti ya Tume ya
Haki za Binadamu kuhusu vitendo vya kudhalilisha viongozi wa CHADEMA katika
shughuli za kisiasa unaofanywa na baadhi ya vyombo vya dola.Alipoulizwa kuhusu
vurugu zilizotokea bungeni mjini Dodoma kwamba anatafsiri vipi vurugu hizo za
baadhi ya wabunge wa CHADEMA kuondolewa kwa nguvu za polisi ndani ya ukumbi wa
Bunge wakati katika Bunge la tisa, akiwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani
hapakuwahi kuwa na matukio kama hayo, Dk. Slaa alijibu; “Kwanza ni makosa
kulinganisha matukio ya Bunge la wakati huu na Bunge la mwaka 2006.”
“Kila wakati unazo changamoto zake,
hata katika Bunge la tisa mimi nilikosana na Spika Samuel Sitta katika suala la
ufisadi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) Benki Kuu ya Tanzania. Alitishia
kunifikisha polisi kutokana na msimamo wangu kuhusu suala hilo lakini baadaye
waliona matokeo yake yalikuwa kwa manufaa ya nchi. Kwa hiyo kwa sasa, kuna
changamoto tofauti ndani ya Bunge.”
Nape ahusisha wazungu
Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi
katika mawasiliano yake na Raia Mwema, akilenga zaidi tukio la hivi karibunu
bungeni, anasema kinachowasumbua CHADEMA mpaka wanafanya yote waliyoyafanya
hasa ngumi na vurugu bungeni ni namna watakavyoeleza kwa waliowapa pesa za
kuvuruga mchakato wa Katiba nchini kwani wanatakiwa kupeleka mrejesho jinsi
walivyofanikiwa na jinsi walivyotumia mabilioni hayo.
"Wenzetu hawa nasikia wamepewa
mabilioni kutoka nje kwa kisingizio cha kushiriki mchakato wa Katiba, na kama
ilivyo kwa vibaraka wengine katika Bara la Afrika, lengo la mapesa hayo sio
kuwawezesha kushiriki bali kuanzisha fujo na vurugu ili mchakato usimalizike
salama iwe ajenda 2015 kwani kimsingi hawana ajenda mpya" anasema Nape na
kufafanua kwamba, mara tu baada ya rasimu ya kwanza ya Katiba Mpya kutoka,
Katibu Mkuu wa CHADEMA alikwenda nje ya nchi na akakaa kwa muda na aliporudi
tu, ndio CHADEMA wakapanga kuanza kuzunguka na helkopta.
"Babu (DK. Slaa)
atuambie alifuata nini nje? Na pesa za kuzunguka na misafara miwili tofauti ya
helkopta walitoa wapi? Na watwambie kama walisharudisha mrejesho kwa wafadhili
wao" anahoji Nape ambaye yuko katika ziara ya kisiasa na Katibu Mkuu wa
CCM, Abdurahaman Kinana, katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
"....hili walilofanya CHADEMA
bungeni ni jambo walilopanga katika mkakati wao wa 'civil disobidiency'
...machafuko ya umma dhidi ya dola, mkakati ambao unaratibiwa kutoka nje na
baadhi ya wale waliokuwa wakoloni katika nchi zetu za Afrika. Lengo ni
kusababisha machafuko na nchi kutotawalika"
“Ndio maana CCM ilisisitiza lazima
Bunge liendelee kuonyeshwa na televisheni ili kuonyesha yanayoendelea bungeni
kuwawezesha wananchi kuona kinachofanywa na wawakilishi wao."Bila shaka
wananchi mmeona kilichotokea bungeni kwa macho yenu, sina haja ya kuwaeleza.
Mmeona wabunge wa upinzani walichofanya, uchaguzi ujao tupunguze idadi ya
vichaa bungeni ili kodi zetu zitumike vizuri, kwani tuliwatuma wakajadili
maendeleo yetu wao wamegeuza Bunge uwanja wa masumbwi.
"Hoja iliyowafanya wapigane
bungeni haina mashiko, wanataka idadi iongezwe ya wabunge wa Bunge la Katiba
kutoka 357 mpaka 792. Hivi nani anabeba mzigo huu wa kuwalipa hawa wabunge kama
sio mwananchi wa kawaida? Halafu mnajiita watetezi wa wanyonge? Hamuoni
aibu?"
Mbunge Vincent Nyerere alonga
Lakini kwa upande wake, Mbunge wa
Musoma Mjini, Vincent Nyerere ambaye ni mmoja wa wanafamilia katika familia ya
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, licha ya kutounga mkono vurugu za bungeni
za hivi karibuni ambazo anaamini zimesababishwa na Naibu Spika Ndugai kutompa
nafasi Mbowe kuzungumza, anasema kimsingi polisi wamevamia Bunge na ameshangaa
polisi hao kuamriwa na mtu asiye polisi na asiye na mamlaka ya kutoa amri.
“Kwa tafsiri, tukio lile linadhihirisha
kwamba polisi ndiyo waliowavamia wabunge. Huwezi kuingia bungeni kwa namna ile
bila kutengua kanuni za Bunge. Mtu asiye mbunge akiingia ndani ya Bunge lazima
kanuni zitenguliwe kwanza. Najua kuna askari wa kawaida wa Bunge hao wanaruhusiwa
kwa kazi maalumu lakini siku ile kulikuwa na watu wengine zaidi... ni makosa,”
anasema Vincent.
Ngwe ya kuhitimisha mwaka
Wakati matukio hayo yakijitokeza na
kuzidi kushangaza baadhi ya Watanzania, hasa kutokana na ukweli kwamba
wanaohusika ni baadhi ya viongozi waliochaguliwa kwa kura, Tanzania inaelekea
kuhitimisha mwaka 2013, kwa mtihani mzito.
Katika mtihani huo, Tanzania katika
historia yake itashuhudia mkutano wa Bunge la Katiba lenye kushirikisha idadi
kubwa zaidi ya Watanzania tofauti na ilivyowahi kutokea. Bunge hilo la Katiba
ambalo jukumu lake litakuwa ni kujadili rasimu ya Katiba Mpya kabla ya rasimu
hiyo kupigiwa kura za maoni na wananchi, linatarajiwa kuitishwa Novemba mwaka
huu, takriban siku zisizopungua 30 hadi kuhitimisha mwaka 2013.
Hata hivyo, mwaka 2014 pia unatarajiwa
kuanza kwa changamoto kwa upande wa siasa za Tanzania, kwani imepangwa kwa
mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Aprili mwaka huo wa 2014, nchi iwe
imepata Katiba mpya.
Source:
www.raiamwema.co.tz
Utawala unaanguka - Dk. Slaa
Toleo la 315
11 Sep 2013
- Nape asema wazungu wanafadhili vurugu za CHADEMA
NI
dhahiri, matukio ya kisiasa yanayokwenda kinyume cha utamaduni mkongwe
wa Watanzania yamezidi kuzusha wasiwasi miongoni mwa raia nchini,
kuhusu mwelekeo hasa wa nchi, angalau baada ya miaka mitano ijayo, Raia
Mwema, imeelezwa.
Kati ya vurugu za hivi karibuni kabisa ni katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kikao kilichokuwa na majukumu ya kujadili, kupitisha au kukataa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, uliowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe.
Hata hivyo, mbali na vurugu hizo za karibuni zinazozidi kuchepusha mweleko mzuri wa harakati za kisiasa uliokuwapo kwa miongo kadhaa sasa, yamekuwapo matukio mengine kadhaa ya vurugu zisizo za kistaarabu katika kuendesha siasa za nchi hasa mara baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Mlolongo wa matukio
Katika tukio hilo la Septemba 6, mwaka 2013 Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aligoma kutii maelekezo ya Naibu Spika, Job Ndugai ambaye ndiye aliyekuwa akiongoza kikao hicho na kutokana na kugoma huko, Ndugai baada ya kumsihi Mbowe mara tatu aketi naye kugoma, aliamuru askari wa Bunge kumtoa nje ya ukumbi wa kikao lakini Mbowe aligoma huku wabunge wenzake wa upinzani wakizuia askari hao kumtoa nje.
Katika purukushani hiyo, Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbai na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, pamoja na wengine baadhi, ndiyo waliokuwa mstari wa mbele kuzuia Mbowe asitolewe na askari ndani ya ukumbi wa Bunge na nguvu zaidi zilitumika kumtoa Mbilinyi kwa kumbeba.
Hoja mbalimbali za utetezi wa pande zote mbili ziliibuliwa dhidi ya tukio hilo, upande wa CHADEMA wakidai ni kwa nini Naibu Spika hakumpa nafasi ya kuzungumza Mbowe na kama angefanya hivyo hakuna vurugu zozote ambazo zingetokea lakini upande wa wanaomtetea Naibu Spika Ndugai, wanasema Mbowe alipaswa kwanza kutii mamlaka ya kiti kwa kuketi na zaidi ya hapo, aliingilia haki ya Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema, ambaye tayari aliruhusiwa na Ndugai kuchangia hoja iliyokuwa mbele ya Bunge.
Na pande zote hizo katika utetezi wao wanarejea kanuni za Bunge, upande wa Mbowe ukisisitiza kiongozi wao ambaye ndiye Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni alipaswa kusikilizwa na inapaswa kuwa hivyo kila anaposimama bungeni lakini upande wa Naibu Spika, akiwamo spika wa zamani, Mzee Pius Msekwa akisema; “Ndugai (Spika) ndiye anayeamua nani aseme, ndiye mwenye mamlaka hayo na ni jambo la kawaida,” na kusisitiza vurugu hizo zimetokana na hisia za ujana zaidi.
Mbali na tukio hilo, matukio mengine yanayoashiria kuyumba kwa mwenendo wa uendeshaji wa siasa nchini ni pamoja na kuwahi kushambuliwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA, katika maandamano ya Januari 5, mwaka 2011, mkoani Arusha na watu watatu kuuawa ikielezwa kuwa walikuwa wakielekea kuvamia Kituo Kikuu cha Polisi mkoani Arusha. Katika tukio hilo, wabunge kadhaa walijeruhiwa, sambamba na viongozi wengine wa CHADEMA.
Tukio jingine la kushtua ni la kulipuliwa kwa bomu katika mkutano wa CHADEMA wa kufunga kampeni za udiwani wa kata nne jijini Arusha, la Juni 6, mwaka huu viwanja vya Soweto pia kuchinjwa kwa mmoja wa viongozi wa CHADEMA katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Msafiri Mbwambo, katika uchaguzi mdogo wa ubunge, Aprili mwaka 2012.
Pamoja na hayo, tukio la mwaka 2012, la kuuawa kwa mwanahabari Daudi Mwangosi aliyekuwa katika shughuli za kisiasa za CHADEMA mkoani Iringa, ambako alikwenda kuripoti mwenendo wa shughuli hizo kwa ajili ya kituo chake cha televisheni, Channel Ten. Wabunge wa CHADEMA, Highness Kiwia wa Ilemela na Salvatory Machemli wa Ukerewe, wote kutoka jijini Mwanza nao walishambuliwa katika harakati za kisiasa mwaka 2012, mjini Mwanza.
Lakini kwa upande wa CCM, kada wao Mussa Tesha alimwagiwa tindikali wakati akibandika mabango ya kampeni za aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM, Dk. Dalali Kafumu ambaye alishinda uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Igunga.
Na kwa upande wa serikali, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, alidhalilishwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA akiwamo Mbunge, Sylvester Kasulumbai na Mbunge wa Vitimaalumu, Susan Kiwanga ambao walipata kushitakiwa katika Mahakama mkoani Tabora kwa kosa hilo la wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga uliotokana na kujiuzulu ubunge kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Rostam Azizi.
Tukio jingine la Februari 5, mwaka huu, linalowahusisha baadhi ya viongozi wa CCM, akiwamo Mbunge wa Tabora Mjini Ismail Aden Rage, ambaye alijikuta katika ugomvi wa kugombea mlingoti wa kupachikia bendera, kati yake na wenzake dhidi ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA mkoani Dodoma. Katika tukio hilo, viongozi hao walipigana, wakifukuzana wakiwa na mawe mkononi kwa ajili ya kujeruhiana.
Dk. Slaa: Ni ishara mbaya kwa utawala
Akizungumzia matukio hayo na mengine ambayo hayajawekwa katika habari hii kutokana na nafasi ndogo gazetini, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa, ambaye bado ana ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania anasema, matukio hayo ambayo mengi yanahusu kunyanyaswa kisiasa kwa CHADEMA, ni dalili za kuanguka kwa utawala wa sasa chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM.).
Dk. Slaa anasema; “Ukitazama hali ya matukio ya kisiasa ambayo yanathibitisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, kuna mambo makubwa mawili yanayojitokeza.
Kwanza, ni serikali pamoja na chama tawala kuhamaki...wame-panic na ndiyo maana unaona wanaelekeza CHADEMA kifanyiwe vurugu katika shughuli zake za kisiasa. Licha ya kwamba Mwenyekiti wao (Rais Jakaya Kikwete) kuwaambia wasitegemee nguvu za polisi katika kuendesha shughuli zao za siasa lakini wameshindwa kuheshimu agizo hilo.
“Pili, matukio haya yanayofanywa na chama tawala na serikali dhidi ya uendeshaji siasa wa CHADEMA ni viashiria vinavyojitosheleza kwamba ni anguko la utawala wao. Duniani popote, ishara ya kuanguka utawala wowote ni kuwapo kwa matukio kama haya tunayoshuhudia sasa. Kwa upande wetu hatutakata tamaa na mapambano ya kudai haki yataendelea.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kuna ushahidi mkubwa unaothibitishwa na ripoti za serikali yenyewe ikiwamo ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu kuhusu vitendo vya kudhalilisha viongozi wa CHADEMA katika shughuli za kisiasa unaofanywa na baadhi ya vyombo vya dola.Alipoulizwa kuhusu vurugu zilizotokea bungeni mjini Dodoma kwamba anatafsiri vipi vurugu hizo za baadhi ya wabunge wa CHADEMA kuondolewa kwa nguvu za polisi ndani ya ukumbi wa Bunge wakati katika Bunge la tisa, akiwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani hapakuwahi kuwa na matukio kama hayo, Dk. Slaa alijibu; “Kwanza ni makosa kulinganisha matukio ya Bunge la wakati huu na Bunge la mwaka 2006.”
“Kila wakati unazo changamoto zake, hata katika Bunge la tisa mimi nilikosana na Spika Samuel Sitta katika suala la ufisadi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) Benki Kuu ya Tanzania. Alitishia kunifikisha polisi kutokana na msimamo wangu kuhusu suala hilo lakini baadaye waliona matokeo yake yalikuwa kwa manufaa ya nchi. Kwa hiyo kwa sasa, kuna changamoto tofauti ndani ya Bunge.”
Nape ahusisha wazungu
Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi katika mawasiliano yake na Raia Mwema, akilenga zaidi tukio la hivi karibunu bungeni, anasema kinachowasumbua CHADEMA mpaka wanafanya yote waliyoyafanya hasa ngumi na vurugu bungeni ni namna watakavyoeleza kwa waliowapa pesa za kuvuruga mchakato wa Katiba nchini kwani wanatakiwa kupeleka mrejesho jinsi walivyofanikiwa na jinsi walivyotumia mabilioni hayo.
"Wenzetu hawa nasikia wamepewa mabilioni kutoka nje kwa kisingizio cha kushiriki mchakato wa Katiba, na kama ilivyo kwa vibaraka wengine katika Bara la Afrika, lengo la mapesa hayo sio kuwawezesha kushiriki bali kuanzisha fujo na vurugu ili mchakato usimalizike salama iwe ajenda 2015 kwani kimsingi hawana ajenda mpya" anasema Nape na kufafanua kwamba, mara tu baada ya rasimu ya kwanza ya Katiba Mpya kutoka, Katibu Mkuu wa CHADEMA alikwenda nje ya nchi na akakaa kwa muda na aliporudi tu, ndio CHADEMA wakapanga kuanza kuzunguka na helkopta.
"Babu (DK. Slaa) atuambie alifuata nini nje? Na pesa za kuzunguka na misafara miwili tofauti ya helkopta walitoa wapi? Na watwambie kama walisharudisha mrejesho kwa wafadhili wao" anahoji Nape ambaye yuko katika ziara ya kisiasa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahaman Kinana, katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
"....hili walilofanya CHADEMA bungeni ni jambo walilopanga katika mkakati wao wa 'civil disobidiency' ...machafuko ya umma dhidi ya dola, mkakati ambao unaratibiwa kutoka nje na baadhi ya wale waliokuwa wakoloni katika nchi zetu za Afrika. Lengo ni kusababisha machafuko na nchi kutotawalika"
“Ndio maana CCM ilisisitiza lazima Bunge liendelee kuonyeshwa na televisheni ili kuonyesha yanayoendelea bungeni kuwawezesha wananchi kuona kinachofanywa na wawakilishi wao."Bila shaka wananchi mmeona kilichotokea bungeni kwa macho yenu, sina haja ya kuwaeleza. Mmeona wabunge wa upinzani walichofanya, uchaguzi ujao tupunguze idadi ya vichaa bungeni ili kodi zetu zitumike vizuri, kwani tuliwatuma wakajadili maendeleo yetu wao wamegeuza Bunge uwanja wa masumbwi.
"Hoja iliyowafanya wapigane bungeni haina mashiko, wanataka idadi iongezwe ya wabunge wa Bunge la Katiba kutoka 357 mpaka 792. Hivi nani anabeba mzigo huu wa kuwalipa hawa wabunge kama sio mwananchi wa kawaida? Halafu mnajiita watetezi wa wanyonge? Hamuoni aibu?"
Mbunge Vincent Nyerere alonga
Lakini kwa upande wake, Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere ambaye ni mmoja wa wanafamilia katika familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, licha ya kutounga mkono vurugu za bungeni za hivi karibuni ambazo anaamini zimesababishwa na Naibu Spika Ndugai kutompa nafasi Mbowe kuzungumza, anasema kimsingi polisi wamevamia Bunge na ameshangaa polisi hao kuamriwa na mtu asiye polisi na asiye na mamlaka ya kutoa amri.
“Kwa tafsiri, tukio lile linadhihirisha kwamba polisi ndiyo waliowavamia wabunge. Huwezi kuingia bungeni kwa namna ile bila kutengua kanuni za Bunge. Mtu asiye mbunge akiingia ndani ya Bunge lazima kanuni zitenguliwe kwanza. Najua kuna askari wa kawaida wa Bunge hao wanaruhusiwa kwa kazi maalumu lakini siku ile kulikuwa na watu wengine zaidi... ni makosa,” anasema Vincent.
Ngwe ya kuhitimisha mwaka
Wakati matukio hayo yakijitokeza na kuzidi kushangaza baadhi ya Watanzania, hasa kutokana na ukweli kwamba wanaohusika ni baadhi ya viongozi waliochaguliwa kwa kura, Tanzania inaelekea kuhitimisha mwaka 2013, kwa mtihani mzito.
Katika mtihani huo, Tanzania katika historia yake itashuhudia mkutano wa Bunge la Katiba lenye kushirikisha idadi kubwa zaidi ya Watanzania tofauti na ilivyowahi kutokea. Bunge hilo la Katiba ambalo jukumu lake litakuwa ni kujadili rasimu ya Katiba Mpya kabla ya rasimu hiyo kupigiwa kura za maoni na wananchi, linatarajiwa kuitishwa Novemba mwaka huu, takriban siku zisizopungua 30 hadi kuhitimisha mwaka 2013.
Hata hivyo, mwaka 2014 pia unatarajiwa kuanza kwa changamoto kwa upande wa siasa za Tanzania, kwani imepangwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Aprili mwaka huo wa 2014, nchi iwe imepata Katiba mpya.

No comments:
Post a Comment