SERIKALI ya Tanzania imeshitukia
mikakati ya baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC), ya kutaka kuharakisha Shirikisho. Akizungumza na waandishi wa
habari jana, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta,
alisema Kenya, Uganda na Rwanda zimeitenga Tanania katika masuala ya
Jumuiya.
Katika hili, alisema nchi hizo
zilikubaliana ifikapo Oktoba 15, Rasimu ya Kwanza ya Uundwaji Shirikisho
itolewe na ifikapo mwakani nchi hizo zianze kutumia viza moja.
Alifafanua,
kwamba kwa mujibu wa Ibara ya 7(E) ya Mkataba wa EAC, baadhi ya nchi
wanachama wana haki kukutana na kuharakisha zaidi katika mambo ya
ushirikiano, lakini mikutano na makubaliano vinatakiwa kupita kwenye
sekretarieti, ili nchi wanachama zielewe kinachoendelea, jambo ambalo
halifanyiki.
"Nchi mbili au tatu zinaruhusiwa kwenda kwa kasi zaidi katika mambo yanayohusu ushirikiano na hilo si jambo la ajabu. Kushirikiana katika miradi ya nchi tatu au nne si jambo la ajabu, lakini kufanya hivyo kwa kuitenga nchi iliyo kwenye Jumuia moja kwa moja, ni tatizo," alisema Sitta.

Kutengwa
Alisema Kenya, Rwanda na Uganda tayari zina makubaliano yao, mbali na
kuanza kutumia viza moja, bali Oktoba 15 waanze kutumia vitambulisho vya
Taifa, kuvuka mipakani. Alikiri kuwa katika mikutano iliyofanywa na
nchi hizo wanachama wa EAC iliyofikia uamuzi huo, Tanzania
haikushirikishwa.
"Suala
la viza moja hatuko tayari, kama wenzetu wanaona linawasaidia basi
waendelee, suala la kutumia vitambulisho vya Taifa katika kuvuka mipaka
hatuko tayari, wao wanaweza kuendelea na uharakishwaji wa kuunda
Shirikisho hatuko tayari," alisema.
Msimamo
"Kama msimamo wa wenzetu ni kuundwa kwanza kwa Shirikisho na matatizo
mengi yatatuliwe ndani, wao kama nchi wana uhuru wa kufanya hivyo na
tunachoomba ni kushirikishwa, ili kuona tunaingia vipi tukiwa tayari.
"Sisi
tuna uzoefu wa kuungana na kama hawataki kusikiliza, basi waendelee ...
hatutaki kuwa mbali na tutakapoona mambo mazuri ndani ya Shirikisho
hilo tutajiunga baadaye," alisema.
Alifafanua, kwamba katika kuhakikisha Shirikisho linakuwa endelevu, walikubaliana kukamilisha hatua tatu za utengamano; kwanza kabla ya Shirikisho, ambazo ni ushuru wa pamoja, soko la pamoja na mfumo wa sarafu moja.
Kwa mujibu wa Sitta, ukamilishaji wa hatua hizo, ndio utawapa wananchi kujiamini katika kuanzisha Shirikisho. Katika utekelezaji wa hatua za kwenda katika Shirikisho, Sitta alisema Tume ya Wataalamu iliundwa, kutafuta maoni ya wananchi kuhusu Shirikisho na muundo wake.
Pia katika kura ya maoni ya wananchi mwaka 2006 /2007, asilimia 84 ya Watanzania walisema hawapendi Shirikisho liharakishwe.

"Hiyo
Tume ya Wataalamu inayoundwa na wajumbe kutoka nchi zote za Jumuiya,
wanatakiwa kutoa taarifa kwa wakuu wa nchi Novemba, na tumetumia fedha
kufanywa utafiti huo," alisema.
Miradi hatarini Sitta alisema kutoshirikishwa kikamalifu kwa nchi moja au mbili katika mikutano na uamuzi, kunachangia utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa kwenye Jumuiya kutofanikiwa.
Miradi hatarini Sitta alisema kutoshirikishwa kikamalifu kwa nchi moja au mbili katika mikutano na uamuzi, kunachangia utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa kwenye Jumuiya kutofanikiwa.
"Mfano,
mwaka jana chini ya Rais Mwai Kibaki wa Kenya, kila nchi ilipeleka
miradi na tulikubaliana kusaidiana kutafuta fedha za kuikamilisha, mfano
ujenzi wa reli, na wa nguzo za umeme kwenda Kenya.
"Sasa wakifanya mikutano bila kushirikishana, tunaweza kuendelea na miradi ambayo sisi si kipaumbele chetu, ukiamini kuwa inachangia kwenye jumuiya kumbe wengine hawataki.
"Sasa wakifanya mikutano bila kushirikishana, tunaweza kuendelea na miradi ambayo sisi si kipaumbele chetu, ukiamini kuwa inachangia kwenye jumuiya kumbe wengine hawataki.
"Huwezi
ukaweka kipaumbele katika kujenga reli mpaka nchi jirani, wakati nchi
husika haitapitisha mizigo kwako, hapo kuna faida gani na hata kama
sehemu kubwa ya reli itasaidia usafiri nchini kwako?" Alihoji.
Baadhi ya miradi ya ushirikiano ambayo Tanzania ilitakiwa kuitekeleza ni ujenzi wa reli kutoka Isaka kwenda Rusumo mpakani na Rwanda na Uvinza hadi mpakani mwa Burundi na ujenzi wa nguzo za umeme wa kilowati 400 kupitia Namanga kwenda Kenya. Tanzania na Burundi ndizo nchi pekee ambazo hazijaalikwa kwenye mikutano ya uundwaji wa Shirikisho unaofanywa na Kenya, Rwanda na Uganda.

Hivi
karibuni, Tanzania na Rwanda ziliingia katika sintofahamu, baada ya
Rais Jakaya Kikwete, kwa nia njema, kumshauri Rais Paul Kagame akae meza
moja na waasi kuzungumzia amani akakataa na kumshutumu mshauri huyo.
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment