Siku
moja baada ya Rais Robert Mugabe na Zanu PF kutangazwa kushinda
uchaguzi Mkuu nchini humo,
baadhi ya wafuasi wa upinzani kutoka chama
cha MDC wanasema wameshambuliwa na wenzao wa ZANU PF.
Baadhi ya dola za Magharibi ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza, zimetilia shaka iwapo uchaguzi huo ulifanyika kwa uwazi.
Madai hayo yanakuja siku moja baada ya
matokeo rasmi ya uchaguzi uliofanyika Jumatano kutolewa na kumpa
ushindi rais Robert Mugabe. Chama chake Zanu-PF kilipata thuluthi tatu
ya viti vya bunge. (HM)
Watu 11 mjini Harare na wengine 20
kutoka mkoa wa Mashonaland, wanasema kuwa walishambuliwa na wafuasi wa
Zanu-PF wanaojulikana sana baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
Chama cha MDC kimesemna uchaguzi huo ulikumbwa na visa vya wizi wa kura.
Kiongozi wake Morgan Tsvangirai, ameahidi kuchukua hatua za kisheria kupinga matokeo ya uchaguzi.
Pia alisema kuwa chama chake cha MDC,
hakitashirikiana na kile cha Mugabe na kuwa kitasusia kushikilia nafasi
zozote katika taasisi za serikali.
Vyama hivyo viwili, vimekuwa wanachama
wa serikali ya Muungano tangu mwaka 2009,baada ya matokeo ya uchaguzi
mkuu wa mwaka 2008 kusababisha ghasia.
Watu 11 waliodai kushambuliwa katika
mtaa mmoja mjini Harare waliomba hifadhi katika makao makuu ya chama cha
MDC mnamo Jumapili, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Brian Hungwe.
Wanadai kuwa walishambuliwa na wafuasi
wa Zanu-PF waliokuwa wanakwenda nyumba hadi nyumba wakiwaamuru wafuasi
wa MDC kufunga virago vyao na kuondoka.
Kiongozi wa chama cha MDC, Morgan Tsvangirai alisema uchaguzi huo ulikumbwa na visa vya wizi.
Msemaji wa MDC, Douglas Mwonzora,
alisema kuwa mashambulizi hayo yalipangwa. Lakini msemaji wa chama cha
Zanu PF, Psychology Maziwisa, alikanusha madai kuwa wafuasi wa chama
walikuwa wanawashambulia wapinzani wao.
MDC kinaonya kuwa hakitaweza kuwadhibiti wafuasi wake ikiwa madai ya wao kushambuliwa yataendelea.
Chama hicho kimeomba muungano wa nchi
za Kusini mwa Afrika , Sadc, kuingilia kati na kuzuia hali kuzorota
zaidi kiasi cha kutoweza jkudhibitiwa.
Baadhi ya wakuu wa chama cha MDC,
wametoa wito kwa wafuasi wao kutoitii serikali na kutenga chama cha
Zanu-PF.
Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment