Kweli sasa Tanzania tunastahili Tunzo, tunaanza kujulikana kimataifa
Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine.
Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong
Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya
zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa
katikati ya chuma cha mashine.
Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa
katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya
dola milioni 1.3 za Marekani.
Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa
wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa
hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.
Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment