WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, August 1, 2013

Kaseja ajazwa noti, asubiri ITC

Kipa namba moja wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Juma Kaseja
Kipa  namba moja wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Juma Kaseja, tayari kwa asilimia 99 ni mchezaji mpya wa klabu ya Lupopo inayoshiriki Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
"Bado sijasaini mkataba ila tayari nimekamilisha mazungumzo na wakala wa Lupopo," alisema Kaseja alipohojiwa jana jioni.

Akizungumza na NIPASHE jana, wakala wa wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kutoka DRC, Balanga Ismael, alisema kuwa tayari wameshakamilisha suala la kumsajili kipa huyo wa zamani wa Moro United, Yanga na Simba zote za Tanzania.

Balanga alisema wanachosubiri sasa ni kuanza taratibu za kupata uhamisho wa kimataifa (ITC) ili aweze kuitumikia klabu yake mpya bila matatizo.

"Tumekamilisha kila kitu na sasa tunachosubiri ni kupata kibali kwa sababu mwakani Lupopo inashiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho, wiki ijayo tutaondoka naye kurejea Kongo," alisema Balanga.
Aliongeza kuwa amefurahishwa na hatua ya kumpata Kaseja ambaye aliachwa na Simba.

Kabla ya kumfuata Kaseja, klabu hiyo ilivutiwa na kiwango cha kipa wa Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro, Hussein Shariff  'Casillas' lakini iliamua kuachana naye kutokana na klabu yake kutaka dau kubwa na pia kutaka kumruhusu kuichezea klabu hiyo kwa muda wa miezi minne.

Balanga pia alisema kuwa ameanza mazungumzo na wachezaji wengine wawili wa hapa nchini kwa ajili ya kwenda kujiunga na klabu za Kongo zinazosaka wachezaji wenye vipaji.

Hata hivyo, wakala huyo alikataa kutaja majina ya wachezaji hao huku akisema mmoja anatoka Yanga.
Katika ligi hiyo ya Kongo, Kaseja ataungana na Watanzania wenzake, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, ambao wote wanaichezea timu ya TP Mazembe.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment