WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, July 9, 2013

MWEZI UMEANDAMA






RAMADHANI NJEMA KWA WAISLAMU WOTE DUNIANI


images 1c4a0

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umeandama; kwa niaba ya uongozi wote wa Ukadirifu blog tunapenda kuwatakia waislamu wote toba na saumu njema;

Tunamuomba Allah Subhanahu Wataala awajalie fursa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  wa kutambua na kutenda kulingana na mafundisho ya Mtume;
 
Tukumbuke kuwa Saumu ni rehama na kuoneana huruma na kukamatana na kuzidisha udugu kwa kuhisi vipi watu wanaohitajia au waliofukuzwa makwao au wanaokosa chakula mwaka mzima. Vipi wanaweza kuishi ikiwa sisi tunaokosa chakula mchana wa ramadhani tu tuna kuwa kama hivi.

Weka azima kuwa mwezi wa ramadhani unaokuja uwe ndio mwezi bora utakaofunga kushinda miezi yote ya ramadhani iliyopita maishani mwako.

 Weka plan yenye uhakika itakayo kufanyisha uweze kufaulu katika mwezi huu. Mfano, andika baadhi ya vitu vya kheri ambavyo utaweza kuvifanya katika mwezi huu. Ujuwe ikiwa huweki plan ya kufaulu basi unaweka plan ya kutofaulu.

Na kwa ndugu zetu ambao sio waislamu katiak kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wawe ni chachu ya kuwasaidia  waislamu katika kutimiza ibada hii muhimu ya toba.

Ramadhani Kariimu
UKADIRIFU MANAJIMENT

No comments:

Post a Comment